USHUHUDA WA MWAKASEGE UNAGUSA SANA
![]() |
Mwalimu Christopher Mwakasege |
Mwalimu Christopher Mwakasege alitoa ushuhuda huo katika semina iliyokuwa ikifanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Semina hiyo iliyokuwa somo linaloitwa namna ambavyo Roho Mtakatifu awezavyo kukusaidia ili upokee kile unachokiomba.
Alisema Roho mtakatifu akwambiavyo omba hiyo haina
MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa
gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni
ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi
hayo.
Roho mtakatifu anapokupa mzigo wa kuombea jambo anakupa na
muda ukizembea muda huo ukipita kinakuwa ni kiporo, na kiporo kinaweza
kikalika na kipo ambacho hakiliki. “Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia
kisha akaanza kuumwa madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia
tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara niko pale
Hospitali wakasema kwa nini usikae tu Hotelini kisha ukawa unapiga simu
kuulizia hali ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa
suala la kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi Arusha kisha nikawa
napiga simu.
Suala hapa ni kuwa nilikuwa naenda kila mara kwa ajili
ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kandokando ya Bahari ya Galilaya
nafanya maombi juu ya Sedikia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako
wa ajabu sana kIsha napanda Taxi kuelekea
Hospitali. Nikifika
Hospitali madactari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda
moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kIsha naingia ICU
alikolazwa.
Nikifika nambana Mungu kwa maswali Mengi namuuliza
Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu muda wote huo si urudi? na kisha
namuuliza Yesu, hivi Yesu si unafahamu kuwa Sedekia anamke
ukimchukua mkewe atamuachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mkono juu yake.
Nilipokuwa nikiweka mkono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa. Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena
kumuuliza Mungu hivi Mungu kama basi husikii maombi yangu sikia maombi
ya watanzania kwa kuwa saa hiyo nilijua watanzania wengi wanamuombea
Sedekia.
Inafikia wakati nakata tamaa lakini ndani yangu najisemea
Mwakasege haiwezekani jitie moyo kisha nabadili aina ya maombi, kwa kuwa
nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa naviweka kati
kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku
nazunguka nguo zake na paspot yake huku nikifanya maombi.
Taratibu
Mungu akaanza kuniambia kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi na
familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika nchini Uingereza
wakati wa skukuu ya Chrismass, na booking mpaka ya Hotel tulikuwa
tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje
kupumzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ikapita na mwaka mpya pia
kisha Sedekia akafariki.
Baada ya kifo hicho sikuchoka nkarudi tena
kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi
mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.
Kila siku
mimi ni mgeni katika maombi namhitaji ROHO anifundishe kwa upya kwa
kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu anabaki kuwa Mungu
kwa kuwa hufanya atakavyo”
Ushuhuda huu umeandikwa kwenye facebook na Francisco. Unaweza kumfuatilia kwenye facebook hapa.
---------------------------------------------------------------------------------
Kama
una ushuhuda na ungetamani tuwashirikishe na wengine kupitia blogu
yako ya Kikristo isiyofungamana na dhehebu lolote usiache kuwasiliana
nasi kwenye facebook au tutumie kupitia ushuhudainjili@gmail.com
Mungu
akubariki sana kwa kufuatana nasi.
No comments:
Post a Comment