Babu wa Loliondo atangaza watu kumiminika upya, Apata maono mengine.

Millard Ayo wa Clouds FM Alipokua akifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila maarufu kama Babu wa Loliondo
Hivi karibuni mtangazaji maarufu Millard
Ayo katika kipindi chake cha Ampifaya alifanya mahojiano na Mchungaji
Ambilikile Masapila na kuelezea kwa urefu mwanzo wa huduma yake ya
kikombe, changamoto, walioiga kutoa vikombe, vipingamizi pamoja na
waliokufa, ambao hawakupona hawakufuata masharti ya dawa.
Mwishoni mwa mahojiano Babu wa Loliando akasema kuhusu mafuriko mapya yatakayotokea hivi karibuni huko Samunge, alizungumza hivi
“Siwezi kusema moja kwa moja kwamba
ni mwezi wa tatu, ingekuwa pengine mpaka sasa tungeanza kupata watu
wengi, na inawezekana ikawa mwezi huo wa tatu, au kabla au baada, mimi
siwezi kusema moja kwa moja kwasababu kuna vipingamizi vingi tu, ambavyo
Mungu anasubiri vitimie ndipo kazi hiyo ianze, Kuna miujiza mingi
imeandikwa ndani ya biblia kitabu cha Mwanzo, Zaburi, Ezekiel, Ufunuo
yapo maajabu mengi ambayo Mungu ameyaandika hayakutimia katika nchi ya
Israel yatatimia hapa, Samunge, kwahiyo mafuriko ya watu watakaokuja si
kwa ajili ya kunywa dawa tu lakini ni kwa ajili ya mambo mbali mbali
kuja kuona miujiza ya Mungu itakayofanyika“
Alipoulizwa ni maajabu gani yatakayofanyika akasema
“Si vizuri, sijamwambia mtu yeyote ba
hata hapa kwako sitasema, isipokuwa mimi nimeyaona mengi tu nimeyaona
tayari lakini Mungu hajaniambia tangaza napewa (Maono) kila wakati
linakuja hili, linakuja hili napewa kila wakati lakini si zaidi ya labda
nusu mwaka sasa“
Ili kulinganisha habari ndipo mtangazaji Millard Ayo alipomuuliza Mchungaji Onesmo Ndegi ni maajabu gani hayo ya kwenye biblia
Mchungaji akasema “Hakuna muujiza
ambao haujatendeka zaidi ya ule muujiza wa unyakuo, miujiza mingine yote
iliyotabiliwa ilishatendeka kwa mfano ukisoma muujiza mkubwa sana ambao
Mungu aliuzungumza kutoka Mwanzo 3:15 biblia inasema hivi nami nitaweka
uadui kati yako na huyu mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake huo
utakuponda kichwa na wewe utauponda kisigino, sasa hapa alikuwa
anazungumzia juu ya ujio wa Kristo na ushindi wa Kristo dhidi ya nguvu
za giza au shetani na ilishatokea na tunaishi katika kipindi hicho, Yesu
Kristo alishakuja akazaliwa, na uwezo wake ukadhibitika ushindi dhidi
ya shetani ulionekana pale msalabani, kwa hiyo hakuna muujiza mwingine
ambao utasema kuanzia mwanzo haujatimia sasa kuna mtu anataka
kuutimiliza, hakuna muujiza wa namna hiyo“
Babu wa Loliondo alipoulizwa tena ana ushauri gani kwa Serikali juu ya maajabu hayo makubwa yatakayotokea hivi karibuni akajibu
“Nilitaka kusema kwa upande wa
Serikali, nitasema ya kwamba Serikali iwe makini kupokea watu
watakaokuja maana ni wengi, ni mafuriko kwa hiyo wawe makini”
Hata hivyo babu amewasamehe watu wote waliomsema vibaya “Kisasi ni kwa Bwana” alisema
–Millard Ayo
No comments:
Post a Comment