ADVERT 1

Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania
Tuesday, November 12, 2013
Kilio cha Wajasiriamali kutangaza kazi zenu itakuwa ni katika Magazeti na Majarida kutoka Nauhacha Media Company Ltd.
Na: Mwandishi Maalum - Morogoro
Mmiliki wa blogu hii ya ugulumo junior bwana Natharine Gallus Ugulumo ambaye ni mwandishi wa habari na Afisa habari katika mradi mmoja wa kimarekani nchini Tanzania ambao makao makuu yake yapo jijini Dar Es Salaam anatarajia kuzindua kampuni yake binafsi iitwayo NAUHACHA Media Co Ltd ambayo makao makuu yake yatakuwa jijini Dar es salaam, ikitoa gazeti la kila siku na Jarida ambalo litakuwa likitoka kila mwezi.
Kati ya machapisho hayo makubwa mawili, yatawapa fursa wajisiriamali wadogo na wakubwa kutangaza kazi zao kwa urahisi lakini pia kupata taarifa mbalimbali za nchi na dunia kwa ujumla, lakini pia mambo ya kijamii hayatasahaulika katika machapisho hayo.
Akiongea na waandishi wa habari Mkoani Morogoro, bwana Ugulumo alisistiza kuwa machapisho hayo yatajikita moja kwa moja kwa jamii katika kupaza sauti za watu wasiokuwa na sauti kupitia chombo chake "Kilio cha wajasiriamali, wanafunzi, na jamii yote kwa ujumla kitamalizika na NAUHACHA Company, lakini pia makala za kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali kama vile mila potofu katika jamii, kilimo, mapambo, na mengineyo yatakuwa katika majarida hayo, kaeni mkao wa kula kupata kisima cha burudani," alisema Ugulumo.
Hata hivyo bwana Ugulumo aliwaomba ushirikiano kwa wanahabari wote katika kufanikisha kazi ya kuihudumia jamii, katika mambo yote hususani yale yanayoonesha kuiharibu na kuiingiza jamii katika msimamo ambao ni hatarishi kwa vijana wetu wa kitanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment