Yaliyojiri siku ya wakulima wa kilimo cha Mpunga Dakawa Morogoro
Na, Kizito Ugulumo, Dakawa Morogoro
Mheshimiwa Joel
Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika maadhimisho ya siku ya
wakulima(Field Day) iliyofanyika tarehe 22 July 2013 katika mashamba ya
washirika wa kilimo cha umwagiliaji (WAWAKUDA) Dakawa – Mvomero.
Mmiliki wa kampuni ya
Tanseed Int Ltd Ndugu Mashauri akitoa utambulisho wa wageni waalikwa
Wali huu ni alama ya
uzalishaji wa chakula bora ambao umepikwa vizuri kwa mafiga matatu ikiwa ni
Tanseed Int, Wawakuda na Nafaka feed the future
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro akipata maelezo juu ya mbegu aina ya TXD 306 “SARO 5” inavyozalishwa
na inavyotoa mazao mengi kwa ekari. Mkuu wa mkoa huo aliongozana na kamati ya
ulinzi na usalama mkoa kushuhudia tukio hilo la mazao bora kutoka katika shamba
lililolimwa na kupandwa kitaalamu kwa
mbegu bora ya TXD 306 kutoka Tanseed International Ltd.
No comments:
Post a Comment