ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Friday, September 28, 2012


FARM INPUT PROMOTION’s  AFRICA  - FIPS Africa Mkombozi wa mkulima mdogo vijijini



 Wakulima kutoka katika wilaya ya Kongwa,Kilombero,Mvomero na Kiteto wakifuatilia kwa karibu mafunzo ya wakulima wakufunzi ngazi ya kijiji (VBAA)

“Mmekuwa mkilima kwa muda mrefu bila kupata mafanikio kutokana na kulima kilimo cha mazoea lakini sasa kupitia kwa maafisa ugani wa  mradi  mmefundishwa mbinu bora za kilimo na matumizi ya mbolea na mbegu za kisasa zitakazoongeza uzalishaji” Hayo yalisemwa na ndugu Abel Mngale Meneja katika mradi wa Nafaka wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wakulima kutoka katika wilaya za kongwa, kiteto,Kilombero na Mvomero katika chuo cha LITI mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki  iliyopita.

FIPS Africa  ni taasisi isiyo ya kiserikali  chini ya ufadhili  wa serikali ya watu wa Marekani katika kupunguza umasikini na  kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na lishe

Mafunzo hayo yaliyoshirikisha watoa mada kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula,wadau kutoka makampuni ya mbolea na mbegu na watafiti wa mazao kutoka katika vituo vya kilimo vilivyopo nchini katika kuhakikisha kuwa wakulima wahamasishaji 107 kutoka wilaya hizo wanapatiwa mafunzo ya kuwa mawakala na wasambazaji wa mbolea na mbegu katika ngazi ya vijiji ili kuweza kuwafikia wakulima wengi na kuwapunguzia gharama za usafiri kufuata mawakala wa mbegu.

“Mbinu husishi za kuboresha na kuhifadhi rutuba ya udongo zinajumuisha matumizi ya mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya kurutubisha udongo ambavyo wakulima mnao  uwezo wa kuvipata kwa urahisi na vinapatikana kwenye mazingira yane, kama vile mbolea za asili na zile za viwandani” alisema Dr Choloba Mkangwa mtoa mada kutoka chuo cha utafiti Ilonga- Kilosa  Mkoani hapa .

Aidha wakala mhamasishaji kutoka wilaya ya Mvomero ndugu Hassan Songoro aliuomba mradi na serikali kwa ujumla kuhakikisha kuwa pembejeo za kilimo zinawafikia wakulima katika wakati unaofaa ili kuendana na msimu wa upandaji kwani wamekuwa wakiletewa mbegu kwa kuchelewa.

Akifunga mafunzo hayo DALDO wa wilaya ya Kongwa aliwapongeza wakulima wahamasishaji hao kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mafunzo hayo yatakayowapa fursa ya kuwa mawakala wa pembejeo za kilimo vijijini ili kupunguza mzigo kwa wakulima wenye kipato kidogo kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi.

  

No comments:

Post a Comment