Yanayoendelea Kutokea hivi sasa huko Somalia hususani kwa waandishi wa Habari
Watu wasiojuilikana wakiwa na silaha walimpiga risasi na kumuua mwandishi wa habari Ahmed Abdulahi Fanah siku ya Ijumaa wakati mwili uliokatwa kichwa wa mwandishi wa michezo Abdirahman Mohamed Ali uligunduliwa katika wilaya ya Huriwa ya Mogadishu hapo AlhamisI (tarehe 27 Septemba), na kufanya idadi ya waandishi wa habari wa Kisomali waliouawa katika mwezi wa Septemba kufikia saba.
"Umoja wa Waandishi wa Habari wa Somalia (NUSOJ) umelaani vikali mauaji haya ya kikatili wa kumkata kichwa Abdirahman Mohamed Ali kama kitendo cha ukatili wa hali ya juu na unyama," ilisema taarifa ya NUSOJ.
Fanah, mwandishi wa habari aliyekuwa na umri wa miaka 32 aliyekuwa akifanyia kazi shirika la habari la Yemen, alipigwa risasi katika wilaya ya Dharkenely mjini Mogadishu hapo Ijumaa asubuhi, uliripoti mtandao wa habari wa Halgan wa Somalia.
Watu wenye silaha walimteka Ali, aliyekuwa akiufanyia kazi mtandao wa habari za michezo Ciyaaraha Maanta, akitokea nyumba moja karibu na soko la nyama hapo Alhamisi na kisha kuutelekeza mwili wake, uliripoti mtandao wa Hiraan Online wa Somalia.
Katika taarifa iliyochapishwa Ijumaa, Ciyaaraha Maanta ilisema waandishi wa habari wataendelea kufanya kazi yao na hawatasitishwa na mauaji hayo. "Hatutasimamisha mbele ya watu walioamua kuwaua waandishi wa habari wanaofanya kazi mjini Mogadishu. Tutaendelea kuripoti michezo kila siku," ilisema taarifa hiyo.
Ali alizikwa siku ya Ijumaa katika makutano ya Kilometre 4 mjini Mogadishu.
Wauaji wawili wa kujitoa mhanga waliwaua kiasi cha watu 14, wakiwemo waandishi watatu wa habari, na kuwajeruhi wengine 20 katika mgahawa mmoja mjini Mogadishu wiki iliyopita. Mwandishi wa nne aliuawa masaa 24 baadaye baada ya kufanya kazi ripoti kuhusu mashambulizi ya kujito mhanga.
Siku ya tarehe 16 Septemba, mpiga picha wa kujitegemea, Zakariye Mohamed Mohamud Moallim aliuawa mjini Mogadishu na watu wenye silaha wasiojuilikana.
No comments:
Post a Comment