ADVERT 1

Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania
Saturday, September 29, 2012
Wameasi dini lakini maadili yako wapi
NIANZE makala hii kwa kurejea simulizi moja ambayo nimeshawahi kusimulia katika makala zilizopita.
Kati ya mambo yaliyonishangaza sana baada ya kuwasili hapa Uingereza kwa mara ya kwanza, takriban muongo mmoja uliopita, ni jinsi Ukristo ulivyopoteza nguvu miongoni mwa Waingereza wengi.
Licha ya ‘kutolewa ushamba’ kwa kushuhudia vitu mbalimbali ambavyo kabla ya kuja hapa vilikuwa ni vya kufikirika tu kama si kuviona kwenye filamu na runinga, kilichoniacha mdomo wazi zaidi ni pale nilipoona jengo ambalo zamani lilikuwa kanisa limegeuzwa klabu ya anasa za usiku (night club).
Kwa Mndamba mie niliyezaliwa sehemu (Ifakara) ambayo ina historia ya karibu na umisionari, kuona ‘nyumba ya Bwana’ imegeuzwa ukumbi wa anasa lilikuwa jambo la kushangaza mno. Na kadri nilivyozidi kuielewa nchi hii ndivyo nilivyozidi kutambua kuwa idadi kubwa tu ya Waingereza haina muda na Mungu au dini kwa ujumla.
Kila nilipopata wasaa wa kudadisi sikusita kuuliza swali hili, “hivi imekuwaje ninyi mliotuletea Ukristo huko Afrika leo hii mnaonekana hamna habari na dini hiyo ilhali dini inazidi kupamba moto huko kwetu?”
Majibu ya swali hilo yalikuwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine, lakini jibu lililojitokeza mara nyingi zaidi ni kuwa imani ya kiroho haina nafasi muhimu katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
Kimsingi, katika Jumapili ya kawaida, makanisa mengi ya Uingereza hujaza ‘wageni’ (kwa maana ya wakazi wenye asili ya nje ya nchi hii, hususan Waafrika na Wakritso kutoka Ulaya ya Mashariki).
Katika siku za kati ya wiki, mengi ya makanisa hayo yamekuwa kama vivutio vya utalii hasa ikizingatiwa kuwa mengi ya majengo hayo ya ibada yana sehemu muhimu katika historia za sehemu yaliyopo.
Lakini ukidhani kufifia huko kwa ‘dini ya nchi hii’ (kimsingi Uingereza ni nchi ya Kikristo na Malkia anaendelea kuwa ‘mkuu wa heshima’ wa Kanisa la Anglikana duniani) kunawafanya Waingereza kutokuwa watu wa kufuata maadili, basi ukienda sehemu mbalimbali za huduma (kama vile kwenye benki, maduka makubwa nk) au ofisini utakumbana na picha tofauti kabisa.
Kwanza, kwa kiasi kikubwa hakuna njia za mkato za kupata fedha katika nchi hii pasipo kuwajibika. Pili, Waingereza wengi wanachukulia shughuli zao kwa uzito na umuhimu mkubwa. Lakini jingine kubwa ni jinsi serikali na taasisi za utawala zinavyojibidisha kutengeneza mazingira mazuri ya kumwezesha kila anayejituma ‘avune matunda ya jasho lake.’
Kuna suala la haki na wajibu. Kwa kiwango kikubwa, wengi wa Waingereza wanatambua wajibu wao wa kulipa kodi, na wajibu huo unawapatia haki ya kupatiwa huduma ambazo kwa kiasi kikubwa zinakidhi matakwa yao.
Kadhalika, taasisi mbalimbali za hapa zinatambua wajibu wao wa kutoa huduma zinazoendana na matakwa ya wahitaji huduma hizo.
Kwa hiyo, licha ya nafasi ya Mungu na Ukristo (au dini kwa ujumla) kufifia miongoni mwa Waingereza wengi, bado kwa kiasi kikubwa jamii hii inafanya ‘mema’ mengi zaidi ya akina sie huko nyumbani tusiokosekana kwenye nyumba za ibada.
Binafsi, licha ya kutopendezwa kuona watu waliotuletea Ukristo huko nyumbani ‘wakiupiga teke,’ wengi wa Waingereza wanaendelea kunivutia jinsi wanavyoendesha maisha na shughuli zao kwa uadilifu mkubwa.
Japo Waingereza wengi ni kama hawana dini lakini wengi wao hawapo tayari kuona mwanadamu mwingine ananyimwa haki zake za msingi, na ndiyo maana nchi hii imetokea kuwa kimbilio kubwa kwa mamilioni ya wakimbizi ambao miongoni mwao ni wale walionyanyaswa na kuteswa na nchi zao aidha kwa imani au itikadi zao, jinsia zao, kutetea wanyonge na kadhalika.
Kwa hali hii, yayumkinika kuhitimisha kuwa bora kuwa ‘mpagani’ mtenda mema kuliko mcha-Mungu fisadi. Ndiyo, dini imepoteza umuhimu wake kwa wengi wa wenzetu hawa lakini wengi wao wameendelea kuwa ‘watu wema’ kuliko mamilioni ya wacha-Mungu huko Afrika.
Yawezekana kabisa ‘wapagani’ hawa kwenda mbinguni kutokana na kumpendeza Mungu kwa matendo yao huku washika dini wetu wakigeuzwa kuni za kuchochea washiriki wao katika kukandamiza, kuibia, kunyanyaswa na kufanya kila baya kwa wanadamu wenzao.
Ni katika mazingira haya ya ‘Uingereza ninayoipenda licha ya wengi wa watu wake kumpa kisogo Mungu’ ndipo nilijikuta nikishtushwa na habari katika gazeti moja la huko nyumbani kuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diane Louise Corner, “amesifu serikali kwa kukuza demokrasia kutokana na uhuru unaovipa vyombo vya habari kuujuza umma kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo matumizi ya umma yanayofanywa na serikali.”
Awali, naomba niseme bayana kuwa hadi muda huu bado nina wasiwasi iwapo Balozi Corner alinukuliwa sahihi (yaani, iwapo kweli alitoa kauli hiyo).
Sitaki kabisa kuamini kuwa Balozi huyo hana taarifa kuhusu unyanyasaji mkubwa unaofanywa na serikali dhidi ya vyombo vya habari binafsi huko nyumbani (ukiweka kando gazeti hilo la serikali liloandika habari hiyo).
Hivi inawezekana Balozi Corner hajawahi kusikia manyanyaso yaliyowakumba wamiliki wa jukwaa huru la mtandaoni la Jamii Forums ambalo kwa hakika limekuwa chanzo kikubwa cha kufichua maovu katika jamii?
Inawezekana Balozi huyo hajawahi kusikia tukio la kumwagiwa tindikali kwa mwandishi wa habari Said Kubenea ambaye serikali inayosifiwa na Balozi huyo imejipa jukumu la kudumu kumdhibiti mhariri huyo na gazeti lake ambalo kwa sasa limefungiwa kwa muda usiojulikana?
Ni demokrasia ipi anayozungumzia mwanadiplomasia huyo ambayo kwa upande mmoja inaruhusu mikutano ya chama tawala CCM katika kampeni za uchaguzi huko Zanzibar lakini si tu inapiga marufuku hata mikutano ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia inapelekea Jeshi la Polisi kunyanyasa wananchi wasio na hatia ambao ‘kosa’ lao pekee ni kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia ya kukusanyika (freedom of association)?
Hivi kweli Balozi Corner hana taarifa kuwa Jeshi la Polisi limeshafanya unyanyasaji mkubwa dhidi ya wafuasi wa CHADEMA na kupelekea vifo vya wananchi wasio na hatia huko Arusha, Morogoro na kubwa zaidi ni kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi huko Iringa hivi karibuni?
Ninasema sitaki kuamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari au demokrasia ninayoshuhudia hapa Uingereza ina tafsiri tofauti na hiyo anayosifia Balozi huyo huko nyumbani.
Niwe mkweli, moja ya sababu ninazoona kuwa zinachangia sana ukosefu wa utawala bora katika nchi zinazoendelea (ikiwamo Tanzania) ni tabia ya nchi zilizoendelea kama Uingereza kuendeleza tabia ya kufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu ambao hauna nafasi kabisa katika ‘jamii zao za kistaarabu.’
Hivi majuzi tu, serikali ya Uingereza kupitia Waziri Mkuu David Cameron imeomba msamaha kuhusiana na maafa ya Hillsborough yaliyotokea mwaka 1989 ambapo mashabiki kadhaa wa soka waliopoteza maisha.
Je, Balozi Corner anafahamu kuwa hadi leo serikali anayoisifia kwa kukuza demokrasia haijaomba msamaha kwa japo kifo cha mwandishi Mwangosi zaidi ya kuunda tume ambayo tayari imeanza kuhujumiwa huku baadhi ya wajumbe wake wakilalamikiwa kuwa na utendaji kazi wenye mushkeli?
Kama Mtanzania ninayeishi katika nchi ambayo huko nyuma ilitutawala kwa mabavu lakini ninaiheshimu na kuipenda kwa mengi inayofanya kwa utu wa mwanadamu pasi kujali ni Mwingereza au ‘mgeni,’ nimeshitushwa sana na kauli ya Balozi Corner ambayo kimsingi inaweza kutumika kama sababu tosha kwa watawala wetu kuendelea kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu kwa ujumla kwa kigezo cha kupewa ‘seal of approval’ na mwakilishi wa taifa kubwa na linaloaminika kwa kuenzi haki hizo muhimu za binadamu.
Kuna nyakati ninapata shida sana kuyaelewa haya mataifa makubwa kama Uingereza katika uhusiano wao na nchi ‘zinazojikongoja.’ Wao ndio wafadhili wetu wakubwa, na asilimia ya kutosha ya fedha za walipakodi wao ndizo zinachangia uhai na ustawi wa nchi masikini (japo zina utajiri unaofilisiwa kila kukicha) kama Tanzania.
Lakini cha kushangaza, hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa nao angalau kuwabana mafisadi wanaokwiba fedha zao (ambazo kimsingi zinatolewa kwa minajili ya kumsaidia kila Mtanzania).
Sana sana ni utitiri wa sifa zinazomwagwa kwa watawala wetu (kama hizo za kukuza demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari), sifa ambazo zinawapa motisha mafisadi kuendelea kuitafuna nchi yetu.
Je, ‘upole’ huo wa wafadhili wetu unachangiwa na hisia kuwa fedha za mafisadi huishia kuhifadhiwa katika mabenki yaliyopo huku? Au inawezekana bado mentality ileile iliyoleta ukoloni (na hata Ukristo) kwamba sisi tulikuwa hatujastaarabika vya kutosha na ilikuwa muhimu kwa wakoloni kujipa jukumu hilo, hadi sasa tunapaswa kuwa na demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari pungufu na tunayoshuhudia hapa Uingereza?
Nimalizie kwa kumkumbusha Balozi Corner kauli ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown katika harakati zake za kuisaidia Afrika.
Alisema (namnukuu katika tafsiri hii isiyo rasmi) “pasipo kuongeza jitihada za kusaidia, itazigharimu baadhi ya nchi za Afrika zaidi ya miaka 150 kufikia tulipofikia sisi (Waingereza).”
Lakini kwa mwenendo huu wa ‘sifa tusizostahili’ basi yayumkinika kubashiri kuwa inaweza kutuchukua hata milele kufikia demokrasia ya kweli yenye kuruhusu uhuru wa kweli wa vyombo vya habari.
Waandishi na serikali: Nani anaingilia mahakama
NIMEKUWA nikieleza na hata kuelekeza, tofauti na baadhi ya wenzangu katika uandishi, kwamba jambo lililoko mahakamani linaweza kuandikwa. Kwa nini?
Kwamba jambo liko mahakamani, hakuzuii mambo mengine kutendeka juu ya hilohilo na nje ya mahakama. Dunia haisimami kwa kuwa jambo liko mahakamani.
Mwenendo wa kilichosababisha kuwa mahakamani hausiti au kufutika eti kwa kuwa tayari kuna shauri mahakamani. Hamu na haki ya kujua haviondoki eti kwa kuwa jambo liko mahakamani. Hapana!
Sheria haikuzuii na hasa haipaswi kukuzuia kuandika mlolongo wa matukio nje ya mahakama unaohusu watu wenye shauri lililoko mahakamani.
Matukio nje ya mahakama yaweza kutoa nuru zaidi juu ya wahusika katika shauri na hata juu ya shauri lenyewe. Taarifa juu ya matukio haya zaweza kuwa za msaada kwa wakili wa utetezi na wakili wa upande wa mashitaka.
Wakati (taarifa hizo) zinaweza kumpa mmoja nuru zaidi juu ya kilichotendeka, zaweza pia kumpa mwingine nuru juu ya kujenga ngome.
Hakimu au jaji anahitaji hoja mshibano na ushahidi mwanana (kama inavyowasilishwa mahakamani na siyo kama inavyosimuliwa nje). Uamuzi wake haupaswi kuongozwa au kutawaliwa au kufungwa na taarifa za magazeti, redio, televisheni au chombo chochote kile cha kutoa taarifa au habari.
Umadhubuti wa hakimu au jaji; hekima, uaminifu wake kwake binafsi na kwa kazi yake juu ya kesi iliyoko mbele yake, havipaswi kupanguliwa na taarifa za nje ya hoja zilizoko mahakamani kwa madai kuwa "zimeathiri maamuzi."
Tuna ushahidi ambako baadhi ya mahakimu na majaji madhubuti wamepuuza na kutupilia mbali madai ya kuathiriwa na vyombo vya habari wakiuliza, "Una uhakika na unaamini kuwa mimi siwezi kufanya kazi hii; siwezi kuwa na maoni na siwezi kuona haki mpaka niambiwe na vyombo vya habari?"
Hili lina maana kwamba kupogoka; kuangalia sheria kwa makengengeza na hata kutoa upendeleo wa waziwazi na uliofichika, ni shabaha, tena ya makusudi, ya hakimu au jaji na siyo kuathiriwa na taarifa za chombo cha habari.
Twende kwa serikali. Taarifa ya serikali ambayo iliahidiwa (juu ya mgomo wa madaktari); kama ingekuwepo, isingeingilia shauri lililoko mahakamani.
Haikuwepo au kuna kilichoingia katikati na kusababisha wasiitoe, ambacho ni wao pekee wanaokijua. Kwamba serikali haitatoa taarifa kwa kuwa imegundua shauri lake na madaktari liko mahakamani, ni sababu ya kizembe mno kutolewa na mamlaka.
Na kama serikali inaweza kusahau ilichofanya juzi tu, basi hii ni barua kwa umma ya kuomba kuaga ikulu.
Sheria haizuii wala kufunga, kwa mfano serikali, kutoka na taarifa inayosema: "Tumepata fedha za kutosha. Sasa madaktari watalipwa nusu ya wanachodai. Hapa tutapata pa kupumulia na kuendelea na majadiliano."
Sheria ipi itazuia hili. Sheria yaweza kununa iwapo serikali itatoka na kusema, "Mtakoma. Msimamo wetu ni uleule, liwalo na aliwe!"
Hili halikubaliki mbele ya hekima, achilia mbali mahakama. Huwezi kwenda mahakamani kuomba nafuu; ukarudi kesho yake kukaza nguvu ya amri ya kukupa nafuu; na kesho yake ukatoka kifua mbele, kwa kutumia nafuu ileile, kuwakomalia wale uliozuia, na isivyo haki, lakini ilivyo halali kisheria.
(Hapa) utakuwa umetumia nguvu ya mahakama kujinufaisha binafsi na utakuwa unajigamba kana kwamba umeweka "mahakama mfukoni."
Inawezekana serikali "imegundua kweli" kuwa inakwenda kufanya madudu. Ikaacha kutoa taarifa. Imejichanganya kwa kuwa imechanganyikiwa.
Hiyo ilikuwa Alhamisi 28 Juni 2012, wakati nikijadili mtandaoni. Lakini nililoandika la kutumia “nguvu ya mahakama kujinufaisha binafsi…kana kwamba umeweka ‘mahakama mfukoni,” ndilo lilitokea baadaye.
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imekwenda mahakamani. Ikaomba nafuu. Ikapewa. Ikatoka mbele. Ikawakomalia madaktari. Ikaanza kuwashambulia. Kuwafukuza kazi kabla ya kile ilichoita “shauri kuu kusikilizwa na kumalizwa.”
Haya basi, siyo matumizi sahihi ya nafuu ya mahakama. Serikali ilikuwa na uwezo wa kufanya iliyofanya bila kutumia nguvu ya mahakama. Haikuhitaji ruhusa ya mahakama kufukuza madaktari.
Kwahiyo, serikali imeonyesha jinsi ilivyohitaji mahakama kufunga mikono, miguu na midomo ya madaktari, ili yenyewe (serikali) ipate nafuu na kuweza kuwacharaza wagomvi wao. Huku ndiko kuingilia mahakama.
Hapa ndipo vyombo vya habari vinajikuta vimetwishwa jukumu la kupaza sauti za wananchi na madaktari; na hata sauti ya mahakama – kupinga matumizi mabaya ya mhimili mwingine wa dola (mahakama); tena kwa sababu dhaifu.
HISTORIA ya mabunge duniani inaliumbua bunge la Jamhuri. Ni kwa sababu, bunge hili limegeuza taasisi ya Bunge kuwa sehemu ya kuminya demokrasia. Limejisahau. Limejifunga mnyororo.
Ni tofauti na Bunge lililopita lililokuwa chini ya Spika Samwel Sitta.
Ni jambo la kusikitisha kuona ushahidi ukijionesha kiwango cha uwajibikaji serikalini kikishuka, Bunge likitumika kuiokoa.
Hakuna asiyejua kuwa serikali imeshindwa kuafikiana na madaktari. Bunge linagoma kujadili suala hilo. Kiongozi wa madaktari ametekwa, kujeruhiwa na sasa yuko kwenye matibabu nje ya nchi, bunge linafungwa mdomo kujadili.
Mauaji ya ovyo ya raia yanazidi kuonge; Bunge halijadili. Utawala bora unatukanwa, huku wawekezaji na matajiri wakitwaa ardhi ya wananchi, bunge linafungwa mdomo. Huu ni uzembe.
Ndiyo maana tunashuhudia utamaduni mpya ukiibuka bungeni; ili hoja ya mbunge ijadiliwe inategemea ni mbunge gani, na hasahasa, wa chama gani.
Kama ni asiyependeza kiti, hapewi nafasi. Kama alipewa kwa kutegwa kwa kuwa spika hakujua atakachokisema, akiibuka mbunge wa watawala na kumhoji, anaridhiwa. Yule anaambiwa “huna hoja.”
Waongoza bunge wametafuta lugha wanazoona nzuri kumbe wanakandamiza haki za wabunge kusema bungeni. Wanataka wabunge wakasemee wapi?
Kisingizio cha kuingilia mahakama hakina nguvu. Kutaja tukio ambalo limefika kwenye mahakama hakuna maana kuwa unaingilia uhuru wa bunge.
Tunasihi waongoza bunge warudi kwenye mstari. Wakiamini hawajakosea wala hawajaudhi au kuwaangusha Watanzania, basi hiyo ni hatari.
Tanzania ipo ndani ya mfumo wa vyama vingi ambao una utamaduni wake. Chini ya mfumo huu, bunge lazima kuwa wazi na huru.
Tungependa waongoza bunge watumie mamlaka waliyonayo kuiwajibisha serikali iliyoamua kukataa kuwajibika. Kama yenyewe haitaki, inalindwa vipi?
Aliyemteka Ulimboka huyu hapa

Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 July 2012
- Ni Ighondu wa Usalama wa Taifa

Afisa huyo, licha ya kutambuliwa na Dk. Ulimboka mwenyewe, ndiye simu yake ilitumika kuandaa kikao ambako daktari alitekwa.
Ni afisa huyohuyo wa usalama ambaye alikutana na Dk. Ulimboka dakika chache kabla ya kutekwa.
Uchunguzi umegundua kuwa Ramadhani Ighondu (34), ni mfanyakazi wa ikulu aliyekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka.
Ni mfanyakazi huyuhuyu ambaye Dk. Ulimboka amenukuliwa akisema, “...alinipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa.”
Nyaraka nyeti ambazo mwandishi ameona zinaonyesha kuwa Ramadhani ndiye pia huitwa “Rama” – jina ambalo hutumia katika kujitambulisha na katika baadhi ya mawasiliano.
Rekodi katika simu ya Dk. Ulimboka: Na. 0713731610 zinaonyesha Rama ndiye alifanya mawasiliano ya mwisho na daktari huyo muda mfupi kabla ya kutekwa.
Aidha, ni Rama ambaye alikutana na kiongozi huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, maeneo ya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kutekwa.
Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa 26 Juni, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno; na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.
Rama alifanya mawasiliano ya mwisho na Dk. Ulimboka saa 5: 52 kupitia simu yake Na. 0713 760473. Dokta alitekwa “muda mfupi” baadaye.
Rais Jakaya Kikwete aliliambia taifa kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni, kuwa serikali yake haihusiki na kuteka, kutesa na kutupa daktari porini.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia bunge kuwa serikali yake haihusiki na utekaji na utesaji; na kuuliza, “...serikali imteke ili iweje?”
Mawasiliano katika simu ya Dk. Ulimboka yanaonyesha mtiririko wa simu za Rama wa ikulu hadi muda wa kutekwa katika eneo la Leaders Club.
Vyanzo vya taarifa ndani ya idara ya usalama wa taifa vinasema, kwa sasa Rama “amehifadhiwa” kwenye jengo moja la kificho linalotumiwa na idara hiyo lililopo eneo la Ada Estate, Kinondoni, Dar es Salaam.
MwanaHALISI limeweza kuthibitisha, kupitia vyanzo vya taarifa na nyaraka mbalimbali kuwa, simu Na. 0713 760473 iliyokuwa ikifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka, ni mali ya Rama.
Huyo ndiye Ramamadhani Ighondu (Rama). Mzaliwa wa Makole, Dodoma. Mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Idara hii iko chini ya Ofisi ya Rais (Utawala Bora) inayoongozwa na Rashid Othman.
Gazeti hili limepitia nyaraka mbalimbali, likiwamo daftari la kudumu la wapigakura lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kupata fununu zaidi juu ya tuhuma za Dk. Ulimboka kwa Rama.
Katika daftari hilo ambalo limetumika kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Rama anaonekana kujitambulisha kama ifuatavyo:
Ramadhani Ighondu,
Nickname: Rama
Born: 28.08.1978
Place: Makole – Dodoma
Voter Registration Card: 49406879
Mobile Number: 0713 760473
Dk. Ulimboka ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, amethibitishia MwanaHALISI kuwa mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara na kumuita kwenye mkutano maeneo ya Leaders Club, 26 Juni 2012, anatumia simu Na. 0713 760473.
Akizungumza kwa kujiamini Dk. Ulimboka amesema, “Ndiyo. Hiyo namba naikumbuka vizuri. Ni 0713 760473. Mwenye namba hiyo alikuwa akijitambulisha kwangu kwa jina la Abeid. Huyo bwana ndiye niliyekutana naye Leaders Club muda mfupi kabla ya kutekwa.”
Alipoulizwa anawezaje kukumbuka namba iliyokuwa inafanya mawasiliano na yeye wakati kipigo alichokipata kutoka kwa watekaji kilikuwa kikubwa hadi kupoteza fahamu, Dk. Ulimboka alisema:
“Ninafahamu ninachokisema. Huyo bwana nilikuwa ninawasiliana naye mara nyingi na niliwahi kukuta naye katika mgogoro ule wa kwanza wa madaktari.”
Kauli hii ya Dk. Ulimboka inafanana na ile aliyoitoa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, 30 Juni 2012.
Katika mahojiano yake yanayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Dk. Ulimboka anasema, “Huyu bwana kwa muda wa siku tatu mfululizo alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumuona.
“Nilishawahi kukutana naye kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course (mara hii) alikuwa serious (makini) akinitafuta…Huyu bwana anafanyakazi ikulu.”
Katika mahojiano hayo, Dk. Ulimboka anasisitiza kuwa wakati anatekwa alikuwa na akili timamu na hivyo anamfahamu aliyemteka kuwa ni mtu kutoka ikulu.
Dk. Ulimboka anasimulia “mtu wa ikulu” alivyoingia kwa gari pale walikomwambia wameketi na kumuuliza iwapo alikuwa na Deo (Dk. Deogratias Michael) na kwamba walianza majadiliano yaliyohusu hali ya mgomo na jinsi wao walivyokuwa wakiona unaweza kutatuliwa.
“Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu; akawa anaandika… kwa hiyo pia alikuwa very busy communicating, (akionekana kujishughulisha zaidi na mawasiliano ya simu). Unaona?”
MwanaHALISI limegundua kabla ya Dk. Ulimboka kutekwa, Rama alianza kufanya mawasiliano naye saa 12: 25 jioni. Mawasiliano hayo yaliendelea 3:29 usiku, saa 4: 52, saa 5: 27, saa 5:40 na mwisho ilikuwa saa 5:52 usiku.
Haya ndiyo mawasiliano ambayo Dk. Ulimboka aliishasimulia kuwa yalielekea katika kukutana kwake na mwenye simu Na. 0713 760473. Ni mwenye simu hii aliyeandaa mkutano, anakumbuka Dk. Ulimboka.
Kabla simu ya Rama kumwita Dk. Ulimboka kwa mara ya kwanza siku hiyo, saa 12:25, ilifanya mawasiliano na Buruani Ntilongwa, mmiliki wa simu Na. 0712 359533.
Mawasiliano hayo yalifanyika kati ya saa 2: 08 na 2: 24 usiku.
Aidha, nyaraka zinaonyesha kila pale Rama alipowasiliana na Dk. Ulimboka, alifanya mawasiliano pia na
Moshi Marungu Shabani anayemiliki simu Na. 0761 132663 na 0655 162663.
“Nakwambia ndugu yangu, kila pale ambapo Rama alifanya mawasiliano na Dk. Ulimboka, utaona hapohapo alifanya mawasiliano na Abdallah Kunja na Ntilongwa. Hawa ni watu muhimu sana kwenye sakata hili,” taarifa zimeeleza.
MwanaHALISI limegundua kuwa siku mbili kabla ya Dk. Ulimboka kufanyiwa unyama huo (24 Juni 2012), simu ya Rama iliingizwa salio la Sh. 252,849. Hili ni salio kubwa pekee kuingizwa kwenye simu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu.
Nyaraka zinaonyesha tarehe 4 Mei 2012 simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio kabisa hadi kufikia kiwango cha Sh. 1.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo zilizosambazwa na kituo cha sheria na haki za binadamu sehemu mbalimbali duniani, Rama kila alipomaliza kumuita Dk. Ulimboka, haraka alipiga simu kwa Kunja, Ntilongwa na Marungu.
Wengine ambao walikuwa na mawasilino ya mara kwa mara na Rama kabla ya kutekwa kwa Dk. Ulimboka ni:
Mohammed Hassan Na. 0655 524444 Shomari Kondo Na. 0714 666304
Optat Jacob Marandu Na. 0716 611625 Mbega Hisbert Na. 0715 222778.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo kwenye daftari la wapigakura la NEC, Mohammed Hassan, ni mkazi wa Ilala, Dar es Salaam. Amezaliwa 12 Agosti 1980. Mbali na kumiliki namba hiyo, anatumia pia namba nyingine: 0717 242789.
Naye Shomari Kondo amezaliwa 1 Januari 1976. Ni mkazi wa Dar es Salaam. Anamiliki simu nyingine Na. 713 671640.
Marandu ametambuliwa kwenye daftari hilo kuwa amezaliwa 1979 mkoani Dodoma; huku Mbega akionyeshwa kuzaliwa 16 Mei 1978 na mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam.
Taarifa nyingine kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa zinasema, tangu 26 Juni 2012, pale jaribio la kumteka Dk. Ulimboka lilipofanikiwa, Rama aliacha kutumia simu yake hiyo.
Alianza kutumia tena simu yake, tarehe 1 Julai kwa kutuma ujumbe mfupi (sms). Namba alizokuwa anatumia sana kuwasiliana kuanzia 1 Julai 2012 ni:
0714 293425
0717 030405
0713 510585 na
0715 466995.
Toleo lililopita la gazeti hili lilimnukuu mtoa taarifa akisema, “Wakati wakimtesa Ulimboka, ni Rama aliyekuwa akisisitiza kuelezwa kama Ulimboka ametumwa na CHADEMA na kwamba ni nani hasa katika CHADEMA anayemtumia.”
Mmoja wa watoa taarifa wa ndani ya idara ya usalama anasema, “Wazo lililopo Usalama wa Taifa ni kuwa Ulimboka anatumiwa na Mnyika pamoja na Dk. Slaa.”
Wengine ambao ni maswahiba wa Rama aliowasiliana nao mara nyingi katika kipindi hicho ni:
Abdi Abdi Na. 0713 229919
Najma Damian Na. 0712 704908
Spa Wilson I. Sima Na. 0712 540502 na
Zulfa Swalehe Na. 0719 496505.
Katika daftari la wapigakura, Abdi Abdi anaonyesha amezaliwa 1977; Spa Wilson I. Sima amezaliwa mwaka 1960 na Zulfa Swalehe amezaliwa mwaka 1950.
Rama ni mfanyakazi wa idara ya usalama wa taifa aliyepo chini ya naibu mkurugenzi wa idara ya usalama anayeshughulikia siasa, Jack Zoka.
Anadaiwa kushiriki kikamilifu kumtesa Dk. Ulimboka katika moja ya majumba ya kificho na hatimaye kumtelekeza msituni Mabwepande, nje ya jiji la Dar es Salaam.
Uchunguzi huu unakuja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Zoka, ndiye mtuhumiwa Na. 1 kwenye sakata la utekaji na utesaji wa Dk. Ulimboka.
Zoka anatajwa pia katika kilichoitwa “…njama za kutaka kuangamiza” maisha ya katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mbunge wa Ubungo, John Mnyika na wengine waliopachikwa jina la “wakosoaji wakuu wa serikali.”
Taarifa mpya za uchunguzi juu ya maandalizi na kutekwa kwa Dk. Ulimboka, zinakuja wiki moja tangu Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova atangaze kufikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai amekiri kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka.
Kova aliwaambia wandishi wa habari kuwa polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kuteka na kutesa Dk. Ulimboka. Amedai kuwa mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es Salaam.
Lakini tayari mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima amekana kauli ya Kova juu mtuhumiwa wake na kusema, “Serikali lazima ieleze vizuri.”
Mchungaji Gwajima amewaambia waamini wake, “Kwanza huyo mtu hajaja kwetu kutubu...kama kutubu, basi mtu huyo angetubu huko kwao Kenya na kuhoji, “…kwani kwao Kenya hakuna Mungu?”
Taarifa za kuaminika zinasema, polisi hawajawahi kuwahoji Dk. Deogratias Michael aliyeshuhudia Dk. Ulimboka akitekwa; Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba wala Onesmo ole Ngurumwa, mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini waliokwenda kumchukua polisi Bunju
Yanayoendelea Kutokea hivi sasa huko Somalia hususani kwa waandishi wa Habari
Watu wasiojuilikana wakiwa na silaha walimpiga risasi na kumuua mwandishi wa habari Ahmed Abdulahi Fanah siku ya Ijumaa wakati mwili uliokatwa kichwa wa mwandishi wa michezo Abdirahman Mohamed Ali uligunduliwa katika wilaya ya Huriwa ya Mogadishu hapo AlhamisI (tarehe 27 Septemba), na kufanya idadi ya waandishi wa habari wa Kisomali waliouawa katika mwezi wa Septemba kufikia saba.
Fanah, mwandishi wa habari aliyekuwa na umri wa miaka 32 aliyekuwa akifanyia kazi shirika la habari la Yemen, alipigwa risasi katika wilaya ya Dharkenely mjini Mogadishu hapo Ijumaa asubuhi, uliripoti mtandao wa habari wa Halgan wa Somalia.
Watu wenye silaha walimteka Ali, aliyekuwa akiufanyia kazi mtandao wa habari za michezo Ciyaaraha Maanta, akitokea nyumba moja karibu na soko la nyama hapo Alhamisi na kisha kuutelekeza mwili wake, uliripoti mtandao wa Hiraan Online wa Somalia.
Katika taarifa iliyochapishwa Ijumaa, Ciyaaraha Maanta ilisema waandishi wa habari wataendelea kufanya kazi yao na hawatasitishwa na mauaji hayo. "Hatutasimamisha mbele ya watu walioamua kuwaua waandishi wa habari wanaofanya kazi mjini Mogadishu. Tutaendelea kuripoti michezo kila siku," ilisema taarifa hiyo.
Ali alizikwa siku ya Ijumaa katika makutano ya Kilometre 4 mjini Mogadishu.
Wauaji wawili wa kujitoa mhanga waliwaua kiasi cha watu 14, wakiwemo waandishi watatu wa habari, na kuwajeruhi wengine 20 katika mgahawa mmoja mjini Mogadishu wiki iliyopita. Mwandishi wa nne aliuawa masaa 24 baadaye baada ya kufanya kazi ripoti kuhusu mashambulizi ya kujito mhanga.
Siku ya tarehe 16 Septemba, mpiga picha wa kujitegemea, Zakariye Mohamed Mohamud Moallim aliuawa mjini Mogadishu na watu wenye silaha wasiojuilikana.
Friday, September 28, 2012
FARM INPUT PROMOTION’s AFRICA - FIPS Africa Mkombozi wa mkulima mdogo vijijini
Wakulima kutoka katika wilaya ya Kongwa,Kilombero,Mvomero na
Kiteto wakifuatilia kwa karibu mafunzo ya wakulima wakufunzi ngazi ya kijiji
(VBAA)
“Mmekuwa mkilima kwa muda mrefu bila kupata mafanikio kutokana na kulima kilimo cha mazoea lakini sasa kupitia kwa maafisa ugani wa mradi mmefundishwa mbinu bora za kilimo na matumizi ya mbolea na mbegu za kisasa zitakazoongeza uzalishaji” Hayo yalisemwa na ndugu Abel Mngale Meneja katika mradi wa Nafaka wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wakulima kutoka katika wilaya za kongwa, kiteto,Kilombero na Mvomero katika chuo cha LITI mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.
FIPS Africa ni taasisi isiyo ya kiserikali chini ya ufadhili wa serikali ya watu wa Marekani katika kupunguza umasikini na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na lishe
Mafunzo hayo yaliyoshirikisha watoa mada kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula,wadau kutoka makampuni ya mbolea na mbegu na watafiti wa mazao kutoka katika vituo vya kilimo vilivyopo nchini katika kuhakikisha kuwa wakulima wahamasishaji 107 kutoka wilaya hizo wanapatiwa mafunzo ya kuwa mawakala na wasambazaji wa mbolea na mbegu katika ngazi ya vijiji ili kuweza kuwafikia wakulima wengi na kuwapunguzia gharama za usafiri kufuata mawakala wa mbegu.
“Mbinu husishi za kuboresha na kuhifadhi rutuba ya udongo zinajumuisha matumizi ya mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya kurutubisha udongo ambavyo wakulima mnao uwezo wa kuvipata kwa urahisi na vinapatikana kwenye mazingira yane, kama vile mbolea za asili na zile za viwandani” alisema Dr Choloba Mkangwa mtoa mada kutoka chuo cha utafiti Ilonga- Kilosa Mkoani hapa .
Aidha wakala mhamasishaji kutoka wilaya ya Mvomero ndugu Hassan Songoro aliuomba mradi na serikali kwa ujumla kuhakikisha kuwa pembejeo za kilimo zinawafikia wakulima katika wakati unaofaa ili kuendana na msimu wa upandaji kwani wamekuwa wakiletewa mbegu kwa kuchelewa.
Akifunga mafunzo hayo DALDO wa wilaya ya Kongwa aliwapongeza wakulima wahamasishaji hao kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mafunzo hayo yatakayowapa fursa ya kuwa mawakala wa pembejeo za kilimo vijijini ili kupunguza mzigo kwa wakulima wenye kipato kidogo kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi.
VIFO VYA MAPEMA BARANI AFRIKA! KWA NINI?

Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani.
Tangu
mwaka 2008, hili limefanyika mara kumi na tatu kote duniani -lakini
kumi kati ya viongozi hao wamekuwa marais wa nchi za afrika.
Kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?
Makundi
makubwa ya watu walikusanyika kushuhudia jeneza la hayati waziri mkuu
wa Ethiopia meles Zenawililipokuwa likipitishwa katikati mwa mji mkuu
Addis Ababa, mnamo siku ya Jumanne wiki iliyopita. Alifariki akiwa na
umri wa miaka 57, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mapema
mwezi huu, maelfu ya wananchi wa Ghana walihudhuria mazishi ya hayati
rais, John Atta Mills, aliyefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 68.
Miezi
minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini
Malawi kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais
Bingu wa Mutharika, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na
mshtuko wa moyo.
Na
mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha,
alifariki katika hospitali ya kijeshi mjini paris baada ya kuugua kwa
muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.
Kwa
hivyo viongozi wanne wa Afrika wamefariki mwaka huu pekee . Bila shaka
ni pigo kwa nchi husika na huzuni kubwa kwa familia za viongozi hao.
Lakini je mwandishi wa habari atafsiri vipi matukio haya?
"Kila
usiku Napata simu nyingi kutoka kwa watu wengi kuniambia rais wa
Afrika ameaga dunia" anasemaSimon Allison, mwandishi habari wa mtandao
wa habari wa Daily Maverick nchini Afrika Kusini. "Kwa nini viongozi
wengi wa Afrika wanafariki sana wakati huu? anahoji Simon.
Swali hili bila shaka linasababisha tathmini ya maisha ya viongozi hao.
"
Ukitafakari kidogo orodha ya viongozi wa Afrika waliofariki bila shaka
ni ndefu'' anasemaAllison. Tangu mwaka 2008, viongozi 10 wa Afrika
wamefariki wakiwa madarakani.
Viongozi
wengine wa Afrika waliofariki wakiwa madarakani ni pamoja na Muammar
Gaddafi akiwa na miaka 69. Aliauawa wakati wa mapinduzi ya kiraia nchini
Libya Oktoba mwaka 2011
Aliyekuwa
rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua aliaga akiwa na miaka 58 mwezi Mei
mwaka 2010 kutokana na maradhi ya figo pamoja na moyo.
Omar Bongo wa Gabon akiwa na miaka 73 alifariki mwaka 2009
Raia wa Guinea Bissau president, J B Vieira umri wa miaka 69 aliuawa mwezi Machi mwaka 2009
Rais wa Guinea Lansana Conte aliaga akiwa na miaka 74 mwaka 2008, kutokana na sababu zisizojulikana.
Aliyekuwa rais wa Zambia , Levy Mwanawasa akiwa na miaka 59 mwaka 2008, kutokana na kiharusi.
Bila
shaka ni kweli kuwa viongozi wengi wa Afrika wanaaga dunia wakiwa
wangali madarakani kuliko katika bara lengine lolote duniani. Katika
kipindi hicho ni viongozi watatu pekee waliofariki wakiwa wangali
madarakani kwingineko duniani.
Kim
Jong Il wa Korea kaskazini , rais wa Poland, Lech Kaczynski,
aliyefariki katika ajali ya ndege na David Thomson wa Barbados,
aliyefariki kutokana na saratani.
Jibu
la wazi ni kuwa marais wa Afrioka ndio wakongwe zaidi kuliko marais wa
mabara mengine.Tathmini inayotolewa hapa ni kuwa waafrika wanapenda
wenyewe kuwa na viongozi wazee kwani kulingana na utamaduni , wanapata
heshima kubwa kutoka kwa jamii.
Muda
mrefu zaidi ambao marais wa Afrika wanaweza kuishi inakadariwa kuwa
miaka 61 sawa na bara Asia. Viongozi wa bara la Afrika, umri wao
unakakadiriwa kuwa miaka 55 wakati barani Afrika rais mkongwe zaidi
anakadiriwa kuwa na miaka 59.
Lakini
kitu kingine cha kutafakari ni umri mrefu zaidi wanaoishi watu wa bara
hilo ikikadiriwa kuwa chini sana barani Afrika ikilinganishwa na
mabara mengine kama Uropa, Amerika ya kusini na barani Asia.
Sababu
kuu hapa ikiwa ni janga la ukimwi, na pia miundo msingi duni ya afya
ambayo inachangia idadi kubwa ya vifo hasa miongoni mwa watoto
wachanga.
Lakini
umaskini katika maisha ya ujana na kwa watoto wachanga pia zinaathiri
kubwa katika umri wa mtu kulingana na daktari George Leeson wa chuo
kikuu cha Oxford.
"marais
wa Afrika kabla ya kuchaguliwa huenda waliishi maisha ambayo sio
mazuri sana na bila shaka hilo litaathiri maisha yao uzeeni'' anasema
daktari Leeson.
Kwa
hivyo wakati wanapoingia madarakani, licha ya kuwa sasa wanaishi
maisha ya kifahari zaidi kuliko siku zao za utotoni, bado athari za
maisha duni walipokuwa wachanga huwaandama
Lakini
hii haimaanishi kuwa viongozi wote wa Afrika waliishi maisha duni
walipokuwa wadogo. Kuna mambo mengine chungu nzima ya kuzingatia.
Mfano, siasa, dhana kwamba, viongozi wa afrika wanapenda kung'ang'ania
madarakani, hadi watapofariki. Lakini dhana hii ingali kuthibitishwa.
Lakini
kunao viongozi waliong'ang'ania madaraka hadi wakafa, kama vile Omar
Bongo, Conte na Gaddafi, kulingana na tathmini mbali mbali. Lakini
wengine kama Meles Zenawi waligandia tu madarakani , kwa sababu kama
Zenawi, alikuwa na miaka 57 pakee.
Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa tathmini hii ni ya viongoiz tu waliofariki wakiwa ofisini tangu mwaka 2008.
SOURCE: BBC
VIDEO: THE BEST OF WAKAZI FREESTYLE VOL. 1...!!!
Kwa hisani ya jestinageorge.blogspot.com
A compilation of Wakazi Freestyles over the years Part 1. Check it out below:
Part 2 comin' soon.
You might also like:
LEWIS HAMILTON TO REPLACE MICHAEL SCHUMACHER AS HE QUITS MCLAREN & JOINS MERCEDES...!!!
LEWIS HAMILTON has quit McLaren and joined Mercedes in a £60million deal.
The
Brit replaces Michael Schumacher — whose second retirement from F1 will
be confirmed by the German car giant at its Stuttgart HQ later today.
Hamilton
said: “It is now time for me to take on a fresh challenge and I am very
excited to begin a new chapter racing for the Mercedes Formula One
Team.
“Mercedes-Benz has such an incredible heritage in motorsport, along with a passion for winning, which I share.
“Together,
we can grow and rise to this new challenge. I believe that I can help
steer the Silver Arrows to the top and achieve our joint ambitions of
winning the world championships.”
The
27-year-old will link up with boss Ross Brawn, who guided Schuey to
seven world titles and was also behind Jenson Button’s 2009 world crown.
Brawn said: “I am delighted to welcome Lewis Hamilton to our team.
“The
arrival of a driver of Lewis’ calibre is a testament to the standing of
Mercedes-Benz in Formula One and I am proud Lewis shares our vision and
ambition for the success of the Silver Arrows.
“I
believe the combination of Lewis and Nico (Rosberg) will be the most
dynamic and exciting pairing on the grid next year and I am looking
forward to what we can achieve together."
Culled from The Sun
Labels:
Lewis Hamilton,
McLaren,
Mercedes,
sports
Reactions: |
FLOYD MAYWEATHER & RAY-J MAKE IT RAIN AT DIAMONDS STRIP CLUB IN ATLANTA...!!!
WARNING!!! RACHETNESS INSIDE!!!
So you thought the Money Team came to an end??? Well you were wrong, in fact they are just getting started.
Original
members Ray-J and Floyd Mayweather Jr. (sans 50 Cent being as though he
is with Team Manny Pacquiao) hit up the strip club Diamonds in Atlanta,
Georgia last night.
It was reported the 2 spent $50,000 on entertainment with bottles of Patron and Grey Goose on deck
Labels:
ATLANTA,
Diamonds Strip Club,
Floyd Mayweather,
Ray j,
Showbiz
Reactions: |
SUPER SPORT YAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KATIKA MEDANI YA MICHEZO KWA KUZINDUA WIKI YA SOKA TANZANIA...!!!
Meneja
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akifafanua ujio wa Super
Sport nchini Tanzania na kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano na
kuwa Chaneli hiyo itaonyesha mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia leo
Ijumaa Septemba 28 hadi Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012.
Mkuu
wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake
kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa
kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi
katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha
kiwango chake cha soka Kimataifa.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga akitoa
nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka
vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha
kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani
wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama timu
zenye upinzani mkali.
Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akifurahi jambo na
watangazaji wa kipindi cha Africa Soccer Show wakati wa halfa hiyo.
CLICK HERE TO READ MORE / ENDELEA KUSOMA
Labels:
sports,
Super Sports
Reactions: |
MAONYESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRIKA YAENDELEA KURINDIMA NEW WORLD CINEMA DAR...!!!
"Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania".
Trade
Marketing Supervisor wa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO ambao ndio
wadhamini wakuu wa maonyesho ya 'Sarakasi ya Mama Afrika' yanayoendelea
katika viwanja vya New World Cinema Bw. Gaudens Mushi akiwakaribisha
wageni waliohudhudhuria onyesho hilo. kushoto ni Afisa Mahusiano wa
TIGO.
Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya 'Mama Africa Circus'.
CLICK HERE TO READ MORE / ENDELEA KUSOMA
Labels:
Mama Africa Circus,
sports
Reactions: |
MSAADA WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KWA HAWA WATOTO...!!!
Elia na Elisha ni watoto mapacha na wana umri wa mika 12 na wanasoma darasa la 3shule
ya Msingi Katanini iliyopo Moshi vijijini karibu na shamba la TPC
mkoani Kilimanjaro, Watoto hawa wanaishi na bibi na babu yao mtaa wa Matindigani kata ya Pasua mjini Moshi-Kilimanjaro. Hawa watoto walitelekezwa na wazazi wao wakiwa tangu wadogo sana baada ya kutokea kutokuelewana kwa wazazi wao.
Elia
na Elisha wanaishi kwenye mazingira hatarishi sana, (hawapati mlo
kamili, hawana mavazi, hawana vifaa vya shule) Tangu wameanza darasa la kwanza hawajawahi kulipa ada na wanasoma kwa fadhila za walimu wa shule ya msingi Katanini. Mwaka huu wamepata msaada wa sare za shule ila bado wanamahitaji yaViatu vya shule, begi la shule, soksi za shule na wanahitaji mtu angalau wakuwalipia masomo ya ziada kwa kuwa wako nyuma kidogo ya wenzao.
Elia na Elisha hawapati chakula nyumbani kwa sababu bibi na babu hawafanyi kazi na wana mtoto mgonjwa wa muda mrefu hivyo chochote kidogo kinachopatikana hupelekwa kwa huyo mgonjwa. Kwa kutambua hilo shule ya msingni katanini wamekuwa wakiwapa mlo wa mchana na uji wa saa 4 asubuhi ambapo uji huo ni kwa ajili ya watoto wa darasa la kwanza na pili.
Natoa wito kwa yeyote mwenye aliyeguswa na matatizo ya watoto hawaanaweza kuwasaidia. Mahitaji muhimu kama:
· Chakula.
· Mavazi.
· Viatu vya shule.
· Ada ya masomo ya ziada. (Tuition)
· Begi la shule.
· Soksi za shule.
· Mavazi.
· Viatu vya shule.
· Ada ya masomo ya ziada. (Tuition)
· Begi la shule.
· Soksi za shule.
Unaweza kutoa chochete kati ya vilivyotajwa hapo juu na si lazima utoe fedha. Pia kama una kitu chochote ambacho wewe hauna matumizi nacho mfano nguo ambazo hauzitumii tena badala ya kuzichoma au kuzitupa tafadhali naomba tuzikusanye ili tuwape watu wenye uhitaji.
Unaweza kupiga namba hizi 0754 090699 au 0712 492131 (John Kessy)
Mwanyekiti wa mtaa 0755 707347 (Renata)
Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wana haki sawa na watoto wengine.
Source: www.kingjofa.blogspot.co.uk
You might also like:
YUMMY MUM TO BE JESSICA SIMPSON IN DOLCE & GABBANA SEQUINED ...
MH. GODBLESS LEMA AKIKAGUA MOJA WAPO YA VITENDEA KAZI VYA ...
JG'S SHOE PICK OF THE DAY: CHRISTIAN LOUBOUTIN'S TECH ...
BREAKING NEWS: HATIMAYE MH. JOSEPH MBILINYI aka SUGU & RUGE ...
FISTULA INATIBIKA.TOA KWA MOYO KUOKOA MAISHA YA MAMA...!!!
#INSTAFASHIONISTA OF THE DAY: JACKIE CLIFF...!!!
Fabulous #instafashionsita of the day
Jackie Cliff is a model, fashionista and owner of a Cosmo Mix Beauty Shop located in Baraka Plaza Dar es Salaam Tanzania.
Subscribe to:
Posts (Atom)