Shalom!
Wapendwa naomba tusimame katika kuomba
huruma ya Mungu na atupe Roho wake Mtakatifu tuogope kabisa kumfanyia
Mungu mzaha. Tuko katika wakati mgumu sana nyakati hizi za mwiso, wapo
“watumishi wa mungu” wanaohubiri kwa kutumia Maandiko Matakatifu/Biblia
lakini nguvu wanazotumia ni za kununua/za giza! Wameusoma upepo uliopo
sasa kuwa watu wamejawa na matatizo mengi na tabu nyingi, sasa mahubiri
yanayohubiriwa yamebakia kuwa ya upande mmoja tu! MAZURI. Watu
wanahubiriwa kupata nyumba, magari, biashara kubwa, watoe/wapande mbegu
wapate baraka tele za kusukwa sukwa (mtu kabeba chuki na mtu moyoni
mwake miaka hajaachilia) nk. Mambo mengine ya msingi kama kusamehe
waliokukosea, kupenda na kuwaombea maadui, kutoa kwa makundi mbalimbali
ya wahitaji nk hayaelezwi. Jinsi ya kujenga uhusiano mzuri na Mungu ili
kuweza kukabiliana na mitihani ama changamoto mbalimbali za maisha ya
ndoa, kazi, imani nk havifundishwi.
Watu wanapatwa na changamoto hizi kwa
vile watumishi wa Mungu hawafundishi waumini wao namna ya kukabiliana na
mateso mbalimbali kadiri ya maandiko na mifano mbalimbali ya watu
walivyoshinda changamoto katika Biblia kwa kumtegemea Mungu. Kwa sababu
yakutokufundishwa hayo utakuta watu wana giveup na kuona suluhu ni
kuhamahama makanisa kutafuta watakapopata miujiza ama suluhu ya matatizo
yao na bado hawapati. Na watu wakipata utajiri ama mazuri wanarudi
kumsifu na kumshukuru/kumsifu mtumishi na mtumishi anakuwa “very proud”
kwa sifa hizo. Haturudishi Sifa Shukrani na Utukufu kwa Mungu.
Kwa kweli Tunahitaji kuomba, kanisa
limeyumba! Halina baba mlezi wa kukemea mambo, sasa kuanzisha makanisa
imekuwa kama kuanzisha biashara. Kila leo kanisa jipya na kila mmoja
anasema kwake ndiko bora. Hebu tuombe kwa ajili ya wimbi hili wapendwa!
No comments:
Post a Comment