Mtoto amtaka Rais Kikwete kuueleza umma > Asema kwa nini alitoa rambirambi kweye msiba wa Kanumba na msiba wa Mwangosi hajatoa kitu? > Nasari awaasa Polisi
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiendelea kukusanyika katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
Joshua Nasari akiwa juukwanii akisubiri muda wake wa kuhutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa. |
Kushoto ni Mch. Peter Msigwa akimkaribisha Joshua Nasari akikari kulia katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
Kushoto Ally Bananga, katikati ni Mch. Peter Msigwa na Kulia ni Joshua Nasari |
Baadhi ya vijana wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (Dogo janja) akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa. |
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakioneshwa vifaa vya elimu walivyopewa na Mbunge wao wakati wa Mkutano katika viwanja vya Mwembetogwa. |
Mamia ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiwa kwenye mkutano. |
Mtoto Cleopasha Witodi Zombe aliyemuuliza Mbunge swali |
Mototo wa miaka 12 Cleopasha Witodi Zombe aliyehitimu elimu ya msingi katika shule ya Wilolesi mwaka huu amemuuliza Mbunge wa Jimbo la Iringa Mch. Peter Msigwa (CHADEMA) juu ya Rais Jakaya Kikwete
kutoonesha hisia zake katika mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi kama ilivyo katika misiba mingine.
“Mheshimiwa Mbunge, kwa nini Rais Kikwete alitoa shilingi milioni kumi katika msiba wa Steven Kanumba lakini hajatoa kitu chochote katika msiba wa mwandishi wetu Daud Mwangosi aliyeuawa na polisi?” aliuliza
mtoto huyo.
Swali hilo aliliuliza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge huyo na kufanyika jana katika viwanja vya Mwembetogwa ndani ya Manispaa ya Iringa.
Wakati huo huo Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (CHADEMA) amewataka polisi kuwaonesha watuhumiwa wa Mauaji wa mwanachama wa Chadema wanaodaiwa kutoroka mahabusu huko Arusha vinginevyo patachimbika.
Tamko hilo alilitoa jana alipokuwa akiwahutumia mamia ya wakazi wa Iringa katika Viwanja hivyo na kuwataka polisi wasiendelee na udanganyifu wa kuwaficha watuhumiwa hao.
“Haiwezi kuingia akilini polisi kuueleza umma kuwa watuhumiwa wametoroka mahabusu, ninawaagiza kuwa lazima watuhumiwa hao waonekane vinginevyo patachimbika” alisema Nasari.
Alisema uchunguzi umebaini kuwa watuhumiwa hao walitumwa na na baadhi ya vigogo kufanya mauaji na hivyo zimefanyika njama za kuwatorosha ili wasiwataje waliowatuma.
“Uchunguzi umebaini kuwa watuhumiwa hao walitumwa na baadhi ya vigogo fulani kumuua mwanachama wetu kwa hiyo polisi wamefanya njama za kuwatorosha ili vigogo hao wasitajwe; nasema hivi, kutokupatikana kwa watuhumiwa hao Tanzania itawaka moto” alisema.
Sanjari na hayo Nasari alisema nchi inapelekwa pabaya kwa sababu ya kukosa vionozi wenye upeo wa kufikiri na kupokea ushauri.
“Nchi hii inapelekwa pabaya kwa sababu ya kukosa viongozi wenye upeo wa kufikiri. Nchi haiwezi kujengeka kwa kuwa na viongozi ombaomba hata siku moja; tabia ya viongozi wetu kuendekeza kuomba wakati nchi ina kila aina ya utajiri, ni ufinyu wa mawazo, ni aibu kwa watanzania na ni fedheha kubwa” alisema.
Amemtaka Rais Kikwete kutopuuza ushauri na mawazo ya watu wanaojitolea kwa ajili ya kulijena taifa na kurudisha heshima ya nchi.
“Kikwete, mimi na mheshimiwa Lema tulikuandikia waraka No. 3 ambao pia tuliuweka kwenye mtandao wa Jamii Forum tukakwambia unakoipeleka Tanzania siko lakini ukayapuuza hayo sasa nchi hii inapotea kwa sababu yako” alisema.
Aliwataka polisi kuacha tabia ya kutumwa kuwaua wananchi wasio na hatia na badala yake wafanye kazi yao kwa kufuata maadili.
“Tabia ya polisi kutii amri kuwaua wananchi wasio na hatia ife kabisa vinginevyo wananchi watakata tama na kuvua vurugu baina yao nawananchi” alisema.
Alisema polisi wamshauri Rais kutokununua silaha za kivita na badala yake anunue mahitaji ya wananchi kwa kuwa nchii haina vita.
“Nawaagiza polisi mkamwambie Rais kuwa, tabia ya kununua maji ya kuwasha wakati wananchi hawana maji ya kunywa aache, tabia ya kununua baari ya polisi yanayotumika kuwaua wananchi wakati wananchi hawana magari ya wagojwa aache, tabia ya kununua bunduki na mabomu wakati hospitali na zahanati za wananchi hazina dawa aache” alisema.
Hata hivyo amewataka wakazi wa Iringa kutowasikiliza wanaombeza Mbune wao Msigwa na badala yake wamhukumu mtu kwa kuangalia mavazi bali hoja zake.
“Msimhukumu mtu kwa kuangalia mavazi bali kwa hoja zake anazozitoa. Wapo watu wanaombeza Msigwa kwa kigezo tu cha upinzani bila kuwa na hoja ya msingi, wapuuzeni hao na kumpa ushirikiano Mbunge wenu kwa ajili ya maendeleo” alisema.
Kwa upende wake Ally Bananga alisema kukichagua Chama cha Mapinduzi CCM nikuendelea kuandaa maisha magumu kwa vizazi vijavyo.
“Mkiichagua CCM tena, nawaambieni kuwa safari ya ahela imeiva, huo siyo utani wala siyo kejeli kwa sababu maisha haya ni mwanzo tu mkitaka zaidi ya haya endeleeni kuichagua CCM” alisema bananga.
Naye Mch. Peter Msigwa aliwataka wananchi kutodanganywa na mtu badala yake watumie uwezo wao kwa kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuzijua haki zao na kuzidai.
“Asiwajaze mtu upepo katika vichwa vyenu, tumieni uwezo wenu katika kufanya maamuzi na kuchambua mambo pamoja na kuzijua haki zenu na kuzidai” alisema.
Katika mkutano huo Msigwa aligawa vifaa mbalimba vya elimu yakiwemo madaftari, kalamu, rula kwa kila mwanafunzi aliyefika katika mkutano huo ambavyo vilikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.
Wakati huo huo Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM katika tawi la Nduli kata ya Nduli Deosdedit Kapugi na Mwenyekiti wa tawi la Mgongo kata ya Nduli Halid Omari Mfumbi wamerudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo, wakuu wa idara mbalimbali walialikwa katika mkutano huo ili kujibu kero mbalimbali za wananchi lakini hakufika hata mmoja
No comments:
Post a Comment