Katibu wa Baraza la Jumuiya za Kiislamu Ponda Issa Ponda alikamatwa
siku ya Jumanne kwa tuhuma za kuchochea ghasia na kuvunja amani jijini
Dar es Salaam, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam Suleiman Kova. Ponda aliitisha maandamano dhidi ya ardhi
iliyonunuliwa kutoka Baraza la Waislamu Tanzania na Kampuni ya
Agritanza.
Ponda pia anatuhumiwa kuchochea vurugu kufuatia mvulana mmoja kuikojolea Qu'ran
mapema wiki hii. Vile vile anatuhumiwa kuchochea maandamano haramu
miongoni mwa wafuasi wake juu ya kiwanja kilichouzwa kihalali, lakini
anasema lazima kibakie mikononi mwa Waislamu.
Idadi kubwa ya polisi wa Dar es Salaam walipelekwa katika wilaya ya
kibiashara katikati ya mji kuwadhibiti waandamanaji waliokerwa na
kukamatwa kwa Ponda. Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi walitumia
gesi za machozi na magari ya maji kutawanya umati wa watu.
Mjini Zanzibar, vijana walitaka kujua taarifa za Sheikh Farid Hadi
Ahmed, kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu visiwani humo, ambaye alitoweka
siku ya Jumanne.
Polisi hawajui alipo na wanachunguza kutoweka kwake, alisema kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini/Magharibi Said Juma. Aliongeza kwamba
vijana wanaoandamana wameziba mitaa kwa mawe, taka na matairi
yaliyochomwa moto na wameunguza majengo.
ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania
Friday, October 19, 2012
Monday, October 15, 2012
TUMUENZI NYERERE KWA VITENDO
Wakati watanzania jana oktoba 14, wakijivunia kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wito watolewa juu ya namna bora ya kumuenzi .
Mmoja ya wanafamilia ya Mwalimu ndugu Vicent Nyerere yeye anasema " KILA
mtu utamsikia akisema anamuenzi baba wa taifa Mw.Julius Kambarage
Nyerere, kama tunamuenzi Mwalimu tumuenzi kwa vitendo kwa kufuata yale
aliyokuwa akielekeza,"
Ni kweli tunavingi vya kujivunia na kumuenzi leo inapotimia miaka 13 tangu
Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa taifa hili
kufariki dunia October 14,1999 kwenye hospitali ya mtakatifu Thomas mji wa London nchini
Uingereza alikokwenda kutibiwa kansa ya damu (leukemia).
Ama kwa hakika huu ni wakati wa huzuni kumkumbuka katika
bara lote la Afrika na ulimwengu kwa ujumla, kutokana na jitihada zake za kutafuta uhuru, amani na mshikamano, taifa la Tanzania limepoteza kiongozi
mwenye bidii na shupavu mwenye huruma
Tukikumbuka
kifo cha baba wa Taifa letu la Tanzania,tunamkumbuka mwalimu kama mtu
aliyejitahidi kutafuta amani katika ulimwengu mzima.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumatatu ambapo Tanzania ilizizima baada ya mh
Raisi wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa kuutangazia umma akisema “ ndugu yetu,mpendwa wetu, baba yetu
mwalimu wetu Julius kambarage Nyerere amefariki dunia”.
Vilio vilisikika kila mahala katika miji na
vijiji vya Tanzania
wakimlilia mkombozi wa nchi ya Tanzania
kutoka katika makoloni ya kijerumani mnamo mwaka 1961
Siku tatu baadae watu walikusanyika Katika uwanja wa ndege wa taifa jijini Dar-es-salam ili
kushuhudia kile walichokisikia kwani ilikuwa ni ngumu kuamini kilichosika mpaka mwili huo uliposhushwa toka nchini
uingereza kwa ndege amambayo ilibeba mwili wa marehemu baba wa Taifa.
Tukimfananisha
mwalimu na viongozi wengine wa leo ni nanani anayeweza kuikemea nchi kama
Uingereza ama Marekani, akasikilizwa, achilia mbali mashirika ya kifedha ya
kimataifa, kama Benki ya Dunia (WB) na IMF?.
Nikinukuu toka katika gazeti la Raia mwema toleo no 156 la
octoba 20,2010 mfano mmoja ni mwaka
1982, wakati Mwalimu aliposhikana shati na IMF akipinga shinikizo la shirika hilo kwa Tanzania
kuridhia masharti na sera za kurekebisha uchumi (SAPs), ikiwa ni pamoja na
kupunguza thamani ya fedha yake.
Kiongozi walioonja hasira ya Mwalimu
baada tu ya Uhuru mwaka 1961, alikuwa waziri wa sheria wa enzi hizo, Chifu
Abdallah Fundikira aliyetuhumiwa kupokea rushwa. Hivyo, alifukuzwa uwaziri
sawia.
Mwaka 1981, Mwalimu hakuweza kumwonea
haya waziri wa mawasiliano, Augustine Mwingira, ilipobainika kuwa alinunua
ndege mbovu kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), kutoka kwa
mfanyabiashara wa Kipalestina, George Hallack; na kwamba ndege hiyo
haikustahili bei iliyonunuliwa. Alimfukuza kazi, pamoja na meneja mkuu wa ATC,
Lawrence Mmasi. Magofu ya ndege hiyo yanaonekana hadi leo uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Vivyo hivyo, mwaka huo, Mwalimu hakuweza
kumvumilia Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Meli Tanzania (TSC)
George Mbowe, ilipobainika kuwa alishiriki kumuuzia mfanyabiashara wa Kihindi,
Akberali Rajpar, meli ya Shirika la Meli za Mwambao (TACOSHIL) – MV Jitegemee”,
kwa bei ya kutupa na kwa mazingira ya kutatanisha.
Mbowe na meneja mkuu wa shirika hilo, Gideon Tibesigwa,
walifukuzwa kazi; ambapo Rajpar alitiwa kizuizini kwa kipindi kwa tuhuma za
kuhujumu uchumi.
Na aliyekuwa meneja mkuu wa Shirika la
Vifaa vya Elimu (TES), Gervas Chilipweli, na mdhibiti wake wa fedha, Mujibur
Rahman, walipumzishwa kazi baada ya kugunduliwa kwa hujuma na ubadhirifu mkubwa
wa fedha katika shirika hilo.
Katika
kipindi hicho hicho, Mwalimu alimfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abdulnuru
Suleimani, kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya kukithiri kwa rushwa
katika uongozi wa mkoa.
Hebu tujiulize Leo, ni kiongozi gani mwenye ujasiri kama wa Mwalimu Nyerere, aliye tayari kusafisha nyumba
yake kwa manufaa ya wanyonge na kuipatia heshima serikali yake?
Tangu
awamu ya pili hadi ya nne ya uongozi wa nchi yetu, ni kiongozi gani ameweza
kufumbia macho utajiri umpite kando na kujitoa mhanga kwa ajili ya
anaowaongoza?.
Leo Tanzania, utajiri unanunua uongozi na uongozi unanunua
utajiri; viongozi wa leo ni sehemu ya tabaka la matajiri wakubwa nchini,
tofauti na enzi za uongozi wa Mwalimu Nyerere. Kitendo cha kuhalalisha
“takrima” katika kampeni za kupata viongozi ni ushahidi tosha kwamba masikini
hataweza tena kupata uongozi nchini kama hali
hii itaendelea
Alikuwa kiongozi wa kanuni
na mwenye msimamo usioyumba.
Kwa wakati huo watanzania walikuwa na
imani kubwa na mwalimu kwa msimamo wake na vilevile sokoine kwa kuwa walikuwa
ni wazalendo na nchi yao
pia na huruma dhidi ya wananchi wanaowaongoza,ni kiongozi yupi leo, aliye
tayari kwenda vijijini kuchanganyika na watu shambani, akawafundisha kilimo
bora na jinsi ya kupambana na malaria?
Mwalimu
aliweza kufanya hivyo; lakini “shangingi” za viongozi wa leo zinaogopa tope
kuwafikia wanaovuja jasho mashambani. Kwa kifupi, Tanzania haijatoa kiongozi shupavu,
mwadilifu na mahiri aina ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Tunapoelekea kupata katiba mpya ya Tanzania, tuna kila
sababu ya kujiuliza katika harakati za kujihakikishia uongozi bora: Nani kama
Mwalimu Julius K. nyerere.
ambae mwishoni
mwa maisha yake ataishi kama mkulima
wa kawaida kama alivyo fanya kama mwalimu huko kijijini kwake Butiama. Tuesday, October 9, 2012
Mtoto amtaka Rais Kikwete kuueleza umma > Asema kwa nini alitoa rambirambi kweye msiba wa Kanumba na msiba wa Mwangosi hajatoa kitu? > Nasari awaasa Polisi
| Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiendelea kukusanyika katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
| Joshua Nasari akiwa juukwanii akisubiri muda wake wa kuhutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa. |
| Kushoto ni Mch. Peter Msigwa akimkaribisha Joshua Nasari akikari kulia katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
| Kushoto Ally Bananga, katikati ni Mch. Peter Msigwa na Kulia ni Joshua Nasari |
| Baadhi ya vijana wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali katika viwanja vya mkutano Mwembetogwa. |
| Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (Dogo janja) akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa. |
| Wanafunzi wa shule mbalimbali wakioneshwa vifaa vya elimu walivyopewa na Mbunge wao wakati wa Mkutano katika viwanja vya Mwembetogwa. |
| Mamia ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiwa kwenye mkutano. |
| Mtoto Cleopasha Witodi Zombe aliyemuuliza Mbunge swali |
Mototo wa miaka 12 Cleopasha Witodi Zombe aliyehitimu elimu ya msingi katika shule ya Wilolesi mwaka huu amemuuliza Mbunge wa Jimbo la Iringa Mch. Peter Msigwa (CHADEMA) juu ya Rais Jakaya Kikwete
kutoonesha hisia zake katika mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi kama ilivyo katika misiba mingine.
“Mheshimiwa Mbunge, kwa nini Rais Kikwete alitoa shilingi milioni kumi katika msiba wa Steven Kanumba lakini hajatoa kitu chochote katika msiba wa mwandishi wetu Daud Mwangosi aliyeuawa na polisi?” aliuliza
mtoto huyo.
Swali hilo aliliuliza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge huyo na kufanyika jana katika viwanja vya Mwembetogwa ndani ya Manispaa ya Iringa.
Wakati huo huo Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (CHADEMA) amewataka polisi kuwaonesha watuhumiwa wa Mauaji wa mwanachama wa Chadema wanaodaiwa kutoroka mahabusu huko Arusha vinginevyo patachimbika.
Tamko hilo alilitoa jana alipokuwa akiwahutumia mamia ya wakazi wa Iringa katika Viwanja hivyo na kuwataka polisi wasiendelee na udanganyifu wa kuwaficha watuhumiwa hao.
“Haiwezi kuingia akilini polisi kuueleza umma kuwa watuhumiwa wametoroka mahabusu, ninawaagiza kuwa lazima watuhumiwa hao waonekane vinginevyo patachimbika” alisema Nasari.
Alisema uchunguzi umebaini kuwa watuhumiwa hao walitumwa na na baadhi ya vigogo kufanya mauaji na hivyo zimefanyika njama za kuwatorosha ili wasiwataje waliowatuma.
“Uchunguzi umebaini kuwa watuhumiwa hao walitumwa na baadhi ya vigogo fulani kumuua mwanachama wetu kwa hiyo polisi wamefanya njama za kuwatorosha ili vigogo hao wasitajwe; nasema hivi, kutokupatikana kwa watuhumiwa hao Tanzania itawaka moto” alisema.
Sanjari na hayo Nasari alisema nchi inapelekwa pabaya kwa sababu ya kukosa vionozi wenye upeo wa kufikiri na kupokea ushauri.
“Nchi hii inapelekwa pabaya kwa sababu ya kukosa viongozi wenye upeo wa kufikiri. Nchi haiwezi kujengeka kwa kuwa na viongozi ombaomba hata siku moja; tabia ya viongozi wetu kuendekeza kuomba wakati nchi ina kila aina ya utajiri, ni ufinyu wa mawazo, ni aibu kwa watanzania na ni fedheha kubwa” alisema.
Amemtaka Rais Kikwete kutopuuza ushauri na mawazo ya watu wanaojitolea kwa ajili ya kulijena taifa na kurudisha heshima ya nchi.
“Kikwete, mimi na mheshimiwa Lema tulikuandikia waraka No. 3 ambao pia tuliuweka kwenye mtandao wa Jamii Forum tukakwambia unakoipeleka Tanzania siko lakini ukayapuuza hayo sasa nchi hii inapotea kwa sababu yako” alisema.
Aliwataka polisi kuacha tabia ya kutumwa kuwaua wananchi wasio na hatia na badala yake wafanye kazi yao kwa kufuata maadili.
“Tabia ya polisi kutii amri kuwaua wananchi wasio na hatia ife kabisa vinginevyo wananchi watakata tama na kuvua vurugu baina yao nawananchi” alisema.
Alisema polisi wamshauri Rais kutokununua silaha za kivita na badala yake anunue mahitaji ya wananchi kwa kuwa nchii haina vita.
“Nawaagiza polisi mkamwambie Rais kuwa, tabia ya kununua maji ya kuwasha wakati wananchi hawana maji ya kunywa aache, tabia ya kununua baari ya polisi yanayotumika kuwaua wananchi wakati wananchi hawana magari ya wagojwa aache, tabia ya kununua bunduki na mabomu wakati hospitali na zahanati za wananchi hazina dawa aache” alisema.
Hata hivyo amewataka wakazi wa Iringa kutowasikiliza wanaombeza Mbune wao Msigwa na badala yake wamhukumu mtu kwa kuangalia mavazi bali hoja zake.
“Msimhukumu mtu kwa kuangalia mavazi bali kwa hoja zake anazozitoa. Wapo watu wanaombeza Msigwa kwa kigezo tu cha upinzani bila kuwa na hoja ya msingi, wapuuzeni hao na kumpa ushirikiano Mbunge wenu kwa ajili ya maendeleo” alisema.
Kwa upende wake Ally Bananga alisema kukichagua Chama cha Mapinduzi CCM nikuendelea kuandaa maisha magumu kwa vizazi vijavyo.
“Mkiichagua CCM tena, nawaambieni kuwa safari ya ahela imeiva, huo siyo utani wala siyo kejeli kwa sababu maisha haya ni mwanzo tu mkitaka zaidi ya haya endeleeni kuichagua CCM” alisema bananga.
Naye Mch. Peter Msigwa aliwataka wananchi kutodanganywa na mtu badala yake watumie uwezo wao kwa kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuzijua haki zao na kuzidai.
“Asiwajaze mtu upepo katika vichwa vyenu, tumieni uwezo wenu katika kufanya maamuzi na kuchambua mambo pamoja na kuzijua haki zenu na kuzidai” alisema.
Katika mkutano huo Msigwa aligawa vifaa mbalimba vya elimu yakiwemo madaftari, kalamu, rula kwa kila mwanafunzi aliyefika katika mkutano huo ambavyo vilikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.
Wakati huo huo Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM katika tawi la Nduli kata ya Nduli Deosdedit Kapugi na Mwenyekiti wa tawi la Mgongo kata ya Nduli Halid Omari Mfumbi wamerudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo, wakuu wa idara mbalimbali walialikwa katika mkutano huo ili kujibu kero mbalimbali za wananchi lakini hakufika hata mmoja
Saturday, October 6, 2012
UMEWAHI KUONA SIGARA YA KUCHAJI KWENYE UMEME?????
Kazi kwenu wavuta sigara
Inaitwa T-FUMO, Material yake ni ya Plastic
Ukiiona inafanana na sigara ya kawaida
Ndani ina Tobacco, na Filter kama kawaida
Hicho kitundu hapo nyuma ndio ukivuta moshi unatokea hapo
Unai charge kwenye laptop au kwenye gari au sehemu yoyote inayoweza kuingia USB Charger
Unabandua filter ya nyuma unachomeka hiko kidude cheusi, kisha unaingiza kwenye Laptop
Ukimaliza unarudishia filter unaendelea kuvuta
Filter ndio iliobeba Tobacco, na zpo za ladha mbalimbali
Ya Chocolate, ya Vanilla, ya Cafe na Mint
The choice is yours.
Inasemekana pia kuwa inasaidia kupunguza uvutaji wa Sigara
Friday, October 5, 2012
Monday, October 1, 2012
Mmiliki wa blog ndugu Kizito Galus ugulumu akiwa na kaka yake Dr Enock Ugulumu wakiwa kwenye kikao cha TEOSA kilichofanyika kitaifa Mkoani Morogoro hivi karibuni.
Moja ya mambo ambayo mmiliki wa mtandao huu wa www.kizitogalus.blogspot.com ni ushirikiano na mahusiano mazuri kwa ndugu jamaa na marafiki hasa katika kujengeana mambo ambayo kimsingi yana maslahi kwa taifa na kwa jamii inozunguka maeneo hayo.Namshukuru mungu kwa kunipa kipaji cha ubunifu wa mambo mbalimbali ikihusisha tafiti(Research) za mambo kadha wa kadha, ushauri wangu ni kwako mdau msomaji wa blog hii jitume na ongeza maarifa utafanikiwa
Moja ya mambo ambayo mmiliki wa mtandao huu wa www.kizitogalus.blogspot.com ni ushirikiano na mahusiano mazuri kwa ndugu jamaa na marafiki hasa katika kujengeana mambo ambayo kimsingi yana maslahi kwa taifa na kwa jamii inozunguka maeneo hayo.Namshukuru mungu kwa kunipa kipaji cha ubunifu wa mambo mbalimbali ikihusisha tafiti(Research) za mambo kadha wa kadha, ushauri wangu ni kwako mdau msomaji wa blog hii jitume na ongeza maarifa utafanikiwa
WADAU DADA ZETU KATIKA FACEBOOK WAMEANZA KUFUNGUKA KUHUSU MAVAZI YASIO NA HESHIMA
Kampeni ya mavazi katika mtandao wa face book
imeendelea kuwafungua mabinti wengi ambao baadhi yao walikuwa ktk
ndoto ya kuja kuiga kuvaa vibaya na baadhi yao wao walikuwa wakiona
sawa kupiga picha za nusu uchi na kuziweka ktk kurasa zao za fb .
Kiukweli kwa siku mbili hizi kurasa za fb zimeanza kuvutia kutazamwa
na watoto na watu wenye heshima zao baada ya akina dada wengi kufunguka
na kuanza kutokelezea kwa mavazi ya heshima .
pichani ni dada Lily Lulandala ambae yeye ameamua hata kubadili picha
yake ktk mwonekano wa ukurasa wake wa fb kutoka ile ya awali ambayo ipo
hapo juu ya pili na kutokelezea vingine kwa kuweka picha hii hapa chini
ya mwisho .
Mtandao huu unaungana na wadau wote wasiopenda picha za nusu uchi iwe
kwa akina dada na akina kaka kuwapongeza waliofunguka na kuvaa kwa
heshima zaidi ombi kwa wadau wote waliopo ktk fb na blog kutozipa
nafasi picha za nusu uchi ili wanaopenda kupiga picha hizo waziweke ktk
albam zao chumbani kwao
Subscribe to:
Posts (Atom)





