ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Tuesday, November 12, 2013


Kitunguu dawa tosha kwa wanaotokwa na damu kwa njia ya haja kubwa

 

 


Katika makala ya leo nawaeleza faida za juisi ya kitunguu maji katika mwili wako, ikiwemo uwezo wake wa kuzuia na kutibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana kwa kutumia dawa za hospitali.

Tunapaswa kutambua kwamba viungo vingi tunavyotumia jikoni kwenye vyakula vyetu kila siku vina uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa yanayotusumbua. Sina shaka kama kuna mtu ambaye hakijui kitunguu, nyanya, au kitunguu saumu.

Kitunguu maji ni kiungo cha mboga, ambacho aghalabu hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha katika chakula na wakati mwingine hutumika kutengenezea kachumbari. Baadhi ya watu hawapendi kula kachumbari kwa kutokujua umuhimu wake mwilini.

KITUNGUU KINATIBU YAFUATAYO
Katika orodha ndefu ya magonjwa yanayotibika PASIPO SHAKA kwa kutumia juisi ya kitunguu, ni pamoja na ugonjwa unaowasumbua watu wengi wa kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisadidia.

Ugonjwa huu, ambao kwa kitaalamu unajulikana kama ‘hemorrhoids’ au ‘Piles’, unawatokea watu wengi ambao kama mtu hukupata nafuu kwa kula vidonge, suluhisho la mwisho huwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo katika njia ya haja kubwa, upasuaji ambao huambatana na maumivu makali.

Kwa wale ambao wameshakutwa na tatizo hili au wanalo hadi sasa, dawa kama vile ANUL SUPPOSITORIES, SECNIDAZOLE, n.k zinajulikana sana kwao, kwa sababu ndiyo dawa zinazopendekezwa na madaktari wengi kutumiwa ili kutibu PILES. Unaweza ukapona kwa muda na tatizo likajirudia baadaye au unaweza usipone na ukalazimika kufanyiwa upasuaji.

Lakini kwa kutumia juisi ya kitunguu, unaweza ukapona kabisa na inawezekana tatizo lisijirudie, kwani mzizi wa tatizo huondoka kabisa kutoka tumboni.

SIFA YA KITUNGUU
Kitunguu kina virutubisho vyenye uwezo wa kuua bakteria (antibacterial) na fangasi mwilini. (anti fungus). Pia kina virutubisho vyenye uwezo wa kuzuia wadudu wanaosababisha magonjwa nyemelezi (anti free radicals) na magonjwa ya uvimbe (anti informatory).

Mbali na sifa hizo, kitunguu kina kiwango kikubwa cha madini kama vile ‘calcium’, ‘magnesium’, ‘sodium’, ‘potassium’, ‘selenium’, ‘phosphorus’ na bila kusahauu kiasi kidogo cha aina fulani ya mafuta ambayo huimarisha kinga ya mwili.
JINSI YA KUJITIBU ‘HEMORRHOIDS.’

Kama nilivyoanza kusema awali, pamoja na magonjwa mengine yanayotibika kwa kitunguu, leo tutaanza kwanza na ugonjwa huu unaosumbua watu wengi. Dawa hii ni ya uhakika kwa mtu atakayeweza kuitumia kama inavyotakiwa.

Kunywa juisi ya kitunguu kila siku asubuhi kwa muda wa siku saba hadi siku 14, ikitegemea na ukubwa wa tatizo lako. Juisi hiyo lazima uinywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote (on empty stomach) na utaruhusiwa kunywa kifungua kinywa chako saa moja baada ya kunywa juisi hiyo.

Dozi hii ni maalum kwa ajili ya kutibu ‘hemorrhoids’, ingawa wakati ukitibu tatizo hilo, matatizo mengine yaliyomo mwilini yatakuwa yakijiondoa, kama tutakavyoona katika makala haya wiki ijayo. Napenda kukuhakikishia kuwa tiba hii ni ya uhakika na haina madhara yoyote.

TAHADHARI
Mara baada ya kuinywa juisi hii kwa mara ya kwanza na siku chache zitakazofuata, utajisikia vibaya na tumbo kuchafuka. Hali hii ni ya kawaida, unachotakiwa kufanya mara baada ya kunywa, ni kukaa au kulala kwa muda, baada ya muda hali yako itarejea kama kawaida. Baada ya siku tatu, ukinywa mwili utaizoea na utajisikia kawaida tu.

MSIBA MKUBWA TANZANIA DR MVUNGI AFARIKI DUNIA

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Edmund Mvungi (katikati) akibadilishana mawazo na Makamishina wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC), Dkt. Juma Ngasongwa (kulia) na Mhe. Othman Masoud, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mara baada ya JFC kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wao uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Mvungi Wafanyakazi -
Jumatano Januari 9, 2013: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi (katikati) akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam leo kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.

Na Mwandishi Wetu
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo..

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.

“Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini,” amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali na kuongeza:

“Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013),” ameongeza.
 

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.

Na Omega S. Ngole
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (0) 757 500800,
Website: www.katiba.go.tz
Facebook:www.facebook.com/people/Omega-Ngole
Twitter: https://twitter.com/OmegaNgole


Fahamu Utamaduni Mila na Desturi ya Mtanzania

Watanzania wana simulizi za kusisimua kuhusu asili yao.  Hapo zamani za kale, kutokana na uso wa ardhi kutokuwa mgumu, ardhi ilipasuka na kusababisha Bonde la Ufa ambalo linatanda kuanzia kusini mwa Yemen kupitia nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania, hadi Ziwa Nyasa na kugawanyika magharibi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.  Moja ya sehemu mashuhuri sana katika Bonde hilo ikatokea ndiyo chimbuko la binadamu.  Binadamu wa awali anafanana na nyani na kwamba fuvu lake na nyayo ziligunduliwa na familia ya Leakeys hapo mwaka 1959 na 1979.  Ushahidi huu ambao ni matokeo ya uvumbuzi wa elimukale kuhusu binadamu wa kwanza ulipatikana katika Bonde la Olduvai na Laetoli.  Maeneo hayo yalikuwa baadhi ya makazi ya ukoo safu wa kisasa (homo habilis na homo sapiens), wazee wa kitanzania ambao waliweza kufikiri na kutengeneza vifaa vinavyotokana na mawe.  Mabaki muhimu ya vifaa na mifupa vilivyoachwa na aina ya binadamu, vinakadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni moja na sabini na tano elfu.  Aidha, ushahidi kamahuo umechimbuliwa kwenye maeneo ya kihistoria huko Isimila katika Nyanda za Juu za Kusini ambako vifaa vya kale, vijulikanavyo kama shoka vinaweza kuonekana leo.  Michoro kwenye mapango ya Kondoa-Irangi iliyochorwa na babu zetu hao na dalili za shughuli za uhunzi na umwagiliaji maji mashamba ni ushahidi mwingine wa kuwepo kwa dalili za mtu wa kwanza katika Tanzania kwa wakati wa kale.  Ni vyema kusadiki na kukubali kutoka hapo ni kwamba baadhi ya wazao walitawanyika duniani kote na baadaye kurejea Tanzania kujiunga na dada na kaka zao waliobaki hapa nchini.  Hao sasa walirejea kama wapiganaji wakulima, wachungaji walowezi, wavamizi, wakimbizi, wakoloni, wafanyabiashara, wavumbuzi, wamisionari au watafuta watumwa.  Idadi kubwa ya watu hao ndiyo wanaunda jamii ya watanzania wa leo ikiwa ni pamoja na makabila makubwa (asilimia 99) bila kuwajumuisha makundi madogo kutoka  Ulaya na Asia (asilimia 1).  Kutokana na kukosekana kwa hali ya utulivu kama kawaida na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za jirani hivi sasa na hata hapo zamani, Tanzania imekuwa ni mahala pa makimbilio kwa wahamiaji.  Wakimbizi kutoka makutano ya Benini-Benne Africa magharibi, Bahr el Ghazal nchini Sudan na maeneo ya Shunygwaya nchini Kenya wote walihamia Tanzania kati ya karne ya tatu na kumi na tatu.  Hii leo Tanzania bado anapokea na kuwahudumia maelfu ya wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda, Somalia na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.  Hali hii inaleta mgongano mkubwa kwa idadi ya watu nchini, rasilimali na mazingira.  Idadi ya wakimbizi hao inakadiriwa kuwa kati ya 500,000 hadi 1,000,000.  Wakimbizi wamesababisha athari kubwa kwa nchi hii.  Kutokana na mahitaji ya chakula, maji na kuni, karibu vyanzo vyote vya maji na mimea ya asili ya sehemu husika na jirani ya kambi hizo za wakimbizi zimeharibiwa.  Matokeo yake ni  kwamba maeneo hayo yamegeuzwa kuwa maeneo yasiyokuwa na kitu, maeneo yaliyo katika hali ya jangwa.
 
Mauaji, wizi  na aina nyingine za maovu yamefanywa na baadhi ya wakimbizi na hivyo kusababisha usumbufu kwa jamii na kutoweka kwa amani kwa baadhi ya raia wa Tanzania.  serikali ya Tanzania, Umoja wa Nchi za Afrika (OAU), Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia  wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF) wanajitahidi kuwarekebisha wakimbizi hao ili wakati muafaka ukifika warejeshwe makwao.
 
Kwa jumuiya ya kimataifa suala la wakimbizi ni eneo lingine ambalo linahitaji msaada zaidi kwa Tanzania ili kuiwezesha kuwasaidia wakimbizi hao kuishi kama binadamu wengine pamoja na kusaidia kuleta amani kwenye nchi zao ili ziweze kuwa mahala pa kuishi.
 

Utamaduni, mila na desturi

Hali ya mvuto wa mfumo ya jamii wa Tanzania ni kivutio kikubwa kwa masuala ya utamaduni, uchumi na utalii.  Hadithi za watu wa kale, ngoma za asilia na aina ya ngoma zinatofautiana kati ya kabila na kabila.  Wanapocheza, Wamakonde kuchezesha viuno vyao kwenda sambamba na ngoma ya “sindimba”, Wazaramo humezwa na maandamano ya “mdundiko”.  Wamaasai huruka kwa mpangilio maalum huko wakitoa  sauti nzito ambazo zinaweza kumwogofya simba dume!  Matumizi ya nyoka hai na kucheza na nyoka wakubwa kama chatu kunakofanywa na Wasukuma wakati wanacheza ngoma ya “Bugobogobo” hakuwezi kusahaulika kwa mgeni.  Kila kabila kati ya  makabila 120 ya Tanzania ina ngoma yake na staili zake za uchezaji ambazo zinapumbaza kwa kukazia macho zinafurahisha na kuvutia kijinsia.
 
Aina mbalimbali ya mavazi pia hutoa mvuto  wa aina yake kwa mgeni.  Wanaume wa Kimasai huvaa vazi ambalo halifuniki mwili wote huku wakitembea na mikuki, virungu na visu vikubwa.  Kwa upande wao, wanawake wa Kimasai hujaza tele shingo zao, mikono, miguu na masikio yao na vitu vya thamani vikiwemo shanga na hadi aina nyingine za madini.  Wanaume wa Kimasai hupakaza miili yao na udongo mwekundu uliochanganywa na mafuta yatokanayo na wanyama na husuka nywele zao.

Wamakonde nao huchonga meno yao na kuchanja nyuso na miili yao taaluma inayotamanisha.  Wamakonde ni wataalam wa kuchonga vinyago vinavyoonyesha matatizo ya binadamu, mapambano, mapenzi, tamaa, wema, ubaya na mshikamano vitu ambavyo vinavutia sana na kuamsha fikra.
 
Wakazi wa pwani na visiwani hupamba mikono, miguu, midomo na kucha kufuatana na tukio shughuli ambayo huleta mvuto mkubwa.
 
Kati ya makabila ya namna ya pekee ni makundi ambayo yanakadiria kutoweka yaishiyo kati ya Tanzania.  Makabila  haya ni ya Wasandawe (wanahusiana na Waethopia) ambao jirani zao ni wa Iraqw gorowa na burungi na Wadzapi ambao pia hujulikana kama Watindiga na Wakangeju na Wahontetot - wanaohusiana na kabila la Khosa la Afrika Kusini ambao huzungumza lugha za “click”.  Wandorobo pia wanazungumza lugha hiyo lakini wameiga zaidi utamaduni wa nje ya mazingira yao.  Watanzania hao ni wa kuhamahama, wachumaji matunda, wawindaji wakusanyaji chakula, na wavuvi waishio katika eneo linalozunguka Ziwa Eyasi ambalo liko kilomita chache kutoka bonde maarufu la Ngorongoro.  Inasemekana kwamba idadi ya watu hawa kwa sasa haifikii 500 wakati mwaka 1965 walikuwa zaidi ya 30,000.

Wito hapa ni kuisaidia Serikali ya Tanzania kuwaokoa watu hao wasifikie ukingo wa kutoweka.  Kwa maana hiyo, maeneo yanayozunguka Ziwa Eyasi ni bora kabisa ya kufanyia utafiti wa kisayansi wa elimu ihusuyo habari za asili na maendeleo ya  binadamu kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye.  Kinachojitokeza ni kwamba ni vyema kutambua kuwa huu ni wakati muafaka wa kufanya uchunguzi ama vile watu hao watakuwa wametoweka kabisa.

 JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Na; Ugulumo Natharine - Morogoro
KAMA WEWE NI MVIVU KUNYWA MAJI BASI ANZA KUJIFUNZA KWA KUNYWA KINYWAJI HIKI KILICHOKAMILIKA KISHA POLE POLE UTAANZA KUYAPENDA MAJI
MAHITAJI
450 grams Nanasi
 50 grams Tangawizi fresh osha vizuri menya
1 Carrot, 
 
JINSI YA KUANDAA FUATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15 
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya wanywaji : watu wawili
Tunda la nanasi na karoti vinachangia sana sukari yote ambayo juisi inatakiwa iwenayo. Tangawizi inaweka uwiano sawa wa ladha kati ya nanasi na karoti, kama sio mpenzi wa tangawizi sio lazima kuitumia, lakini kama ni mpenzi wa nanasi au karoti unaweza kuzidisha  kimojawapo ili upate ladha halisi ya unachokipenda.
Tangawizi: Inategemea na ubora wa tangawizi, unaweza kuhitaji nyingi zaidi au wastani cha msingi uweze kupata harufu mwanana katika juisi yako.

Menya vizuri nanasi yako kisha katakata vipande vidogo kama inavyoonekana 

Chukua vipande vya nanasi, karoti na tangawizi kisha saga kwenye blenda.

Saga vizuri kisha chuja vizuri kwa chujio iliyo safi.

Baada ya kuchuja kama haijachujika vizuri, basi ongeza maji baridi na safi kiasi tu kisha chuja tena na kisha utapata juisi safi kabisa laini

Kwa sasa ipo tayari waweza kumpatia mnywaji ikiwa ya baridi. Kinywaji safi kabisa kwa majira ya joto yanayokuja hivi karibuni. Waandalie familia yako waweze kufurahia na nakuwajengea tabia ya kuzoea kunywa maji.




Kilio cha Wajasiriamali kutangaza kazi zenu itakuwa ni katika Magazeti na Majarida kutoka Nauhacha Media Company Ltd.

Na: Mwandishi Maalum - Morogoro

Mmiliki wa blogu hii ya  ugulumo junior  bwana Natharine Gallus Ugulumo ambaye ni mwandishi wa habari na Afisa habari katika mradi mmoja wa kimarekani  nchini Tanzania ambao makao makuu yake yapo jijini Dar Es Salaam anatarajia kuzindua kampuni yake binafsi iitwayo NAUHACHA Media Co Ltd ambayo makao makuu yake yatakuwa jijini Dar es salaam, ikitoa gazeti la kila siku na Jarida ambalo litakuwa likitoka kila mwezi.

Kati ya machapisho hayo makubwa mawili, yatawapa fursa wajisiriamali wadogo na wakubwa kutangaza kazi zao kwa urahisi lakini pia kupata taarifa mbalimbali za nchi na dunia kwa ujumla, lakini pia mambo ya kijamii hayatasahaulika katika machapisho hayo.

Akiongea na waandishi wa habari Mkoani Morogoro, bwana Ugulumo alisistiza kuwa machapisho hayo yatajikita moja kwa moja kwa jamii katika kupaza sauti za watu wasiokuwa na sauti kupitia chombo chake "Kilio cha wajasiriamali, wanafunzi, na jamii yote kwa ujumla kitamalizika na NAUHACHA Company, lakini pia makala za kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali kama vile mila potofu katika jamii, kilimo, mapambo, na mengineyo yatakuwa katika majarida hayo, kaeni mkao wa kula kupata kisima cha burudani," alisema Ugulumo.

Hata hivyo bwana Ugulumo aliwaomba ushirikiano kwa  wanahabari wote  katika kufanikisha kazi ya kuihudumia jamii, katika mambo yote hususani yale yanayoonesha kuiharibu na kuiingiza jamii katika msimamo ambao ni hatarishi kwa vijana wetu wa kitanzania.


Monday, November 11, 2013


 Yaliyojiri siku ya wakulima wa kilimo cha Mpunga Dakawa Morogoro

Na, Kizito Ugulumo, Dakawa Morogoro

Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika maadhimisho ya siku ya wakulima(Field Day) iliyofanyika tarehe 22 July 2013 katika mashamba ya washirika wa kilimo cha umwagiliaji (WAWAKUDA) Dakawa – Mvomero.

 Mmiliki wa kampuni ya Tanseed Int Ltd Ndugu Mashauri akitoa utambulisho wa wageni waalikwa


Wali huu ni alama ya uzalishaji wa chakula bora ambao umepikwa vizuri kwa mafiga matatu ikiwa ni Tanseed Int, Wawakuda na Nafaka feed the future


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akipata maelezo juu ya mbegu aina ya TXD 306 “SARO 5” inavyozalishwa na inavyotoa mazao mengi kwa ekari. Mkuu wa mkoa huo aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa kushuhudia tukio hilo la mazao bora kutoka katika shamba lililolimwa na kupandwa kitaalamu kwa  mbegu bora ya TXD 306 kutoka Tanseed International Ltd.

Tuesday, April 16, 2013

MAZISHI YA JENERALI MAKAME RASHIDI ALIYEKUWA MKUU WA JKT

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin William Mkapa akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davies Mwamunyange akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa  marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Jeneza likiwekwa sehemu maalum kwa ajili ya heshima za mwisho.
Ndugu wa Marehemu wakiwa ni wenye majonzi na huzuni kubwa ya kuondokewa na Mpendwa wao.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Toka kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),Luteni Jenerali,Samuel Ndomba,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,Kamishna Jenerali John Minja wakiwa kwenye msiba wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.Picha na OMR.