ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Friday, October 5, 2012



Mmiliki wa blog hii www.kizitogalus.blogspot.com akiwa anarejea kutoka mkoani Manyara akiwa na ziara ya kuzunguka kanda ya kati na pwani katika kuhakikisha taratibu za taasisi zisizo za kiserikali zinatakeleza majukumu yake kikamilifu katika kuboresha maisha ya Mtanzania

Monday, October 1, 2012

 Mmiliki wa blog ndugu Kizito Galus ugulumu akiwa na kaka yake Dr Enock Ugulumu wakiwa kwenye kikao cha TEOSA kilichofanyika kitaifa Mkoani Morogoro hivi karibuni.

Moja ya mambo ambayo mmiliki wa mtandao huu wa www.kizitogalus.blogspot.com ni ushirikiano na mahusiano mazuri kwa ndugu jamaa na marafiki hasa katika kujengeana mambo ambayo kimsingi yana maslahi kwa taifa na kwa jamii inozunguka maeneo hayo.Namshukuru mungu kwa kunipa kipaji cha ubunifu wa mambo mbalimbali ikihusisha tafiti(Research) za mambo kadha wa kadha, ushauri wangu ni kwako mdau msomaji wa blog hii jitume na ongeza maarifa utafanikiwa

WADAU DADA ZETU KATIKA FACEBOOK WAMEANZA KUFUNGUKA KUHUSU MAVAZI YASIO NA HESHIMA

.
Kampeni ya mavazi katika mtandao  wa face book  imeendelea  kuwafungua mabinti wengi ambao baadhi yao  walikuwa ktk ndoto ya kuja kuiga kuvaa vibaya na baadhi  yao wao  walikuwa  wakiona  sawa  kupiga picha za nusu uchi na  kuziweka ktk kurasa  zao za fb .
Kiukweli kwa  siku mbili hizi  kurasa za fb zimeanza  kuvutia kutazamwa na watoto na watu wenye heshima  zao baada ya akina dada wengi kufunguka na kuanza kutokelezea kwa mavazi ya heshima .
pichani ni dada Lily Lulandala ambae yeye ameamua hata kubadili picha yake ktk mwonekano wa ukurasa wake wa fb kutoka ile ya awali ambayo ipo hapo juu ya pili na kutokelezea vingine kwa kuweka picha hii hapa chini ya mwisho .
Mtandao  huu  unaungana na wadau wote  wasiopenda picha za nusu uchi iwe kwa akina  dada na akina kaka  kuwapongeza  waliofunguka na kuvaa kwa heshima  zaidi ombi kwa wadau  wote  waliopo ktk fb na blog kutozipa nafasi picha za nusu uchi ili wanaopenda kupiga picha hizo  waziweke ktk albam zao chumbani kwao

Saturday, September 29, 2012

Mhalifu anapopigiwa saluti haki yaweza kupatikana kweli?

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda 

Ninaamini - na ushahidi uko upande wangu - Kamanda Kamuhanda alipaswa kusimamishwa kazi mara moja, kushtakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa vyeo vyake ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine (wale waliompiga Mwangosi wanatakiwa pia wawemo).

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda anastahili kutiwa pingu na kufikishwa mahakamani akiunganishwa na mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya Daud Mwangosi yaliyotokea siku kadhaa zilizopita.

Kushindwa kuchukuwa hatua mara moja dhidi ya Kamuhanda na uongozi wa jeshi hilo na uongozi wa kisiasa nchini ni dalili mbaya zaidi ya kuvunjika kwa mfumo wa utawala wa sheria.

Hili linanikumbusha kisa cha Ukiwaona Ditopile wa Mzuzuri (sasa marehemu) na jinsi uongozi wa kisiasa ulivyojikuta unaweweseka katika kuamua mizani ya haki iende vipi. Hata hivyo, ninaamini kuna sababu kubwa mbili za kwanini kumchukulia hatua Kamanda Kamuhanda kumechelewa, pengine kumetoa nafasi ya kuchezea ushahidi (tampering with evidence), kutishia mashahidi (intimidation of witnesses) na kwa namna yoyote kupindisha mwenendo wa uchunguzi na hivyo kuharibu mchakato wa kupata haki (obstruction of justice).

Kwenye nchi ambayo inaheshimu utawala wa sheria kwa vile Kamanda Kamuhanda alikuwa ni shuhuda wa tukio (material witness) hakupaswa kuwa sehemu ya uchunguzi na kwa hakika hakupaswa kuendelea na wadhifa wake wakati uchunguzi wa mauaji yaliyotokea mbele yake na kwa sababu yake unafanyika.

Kumwacha aendelee na nafasi yake ni mojawapo ya uvunjaji mkubwa wa haki ambao serikali imeruhusu na wanasiasa wetu wanavumilia. Sababu za kwanini Kamuhanda asimamishwe kazi na kufunguliwa mashtaka (asili ya mashtaka sitaki kuhisi sana lakini itakuwa ni kati ya matumizi mbaya ya madaraka hadi mauaji) ni hizi zifuatazo. a. Hakuwa na sababu ya kuvunja shughuli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo ilikuwa inafanyika kwa mujibu wa sheria.

Kwa wale walioona video ya mazungumzo yaliyotangulia vurumai kati ya Kamuhanda na wandishi wa habari, hoja kubwa ilikuwa kama mkutano wa CHADEMA ulikuwa ni "mkutano wa ndani" (internal meeting) au ulikuwa ni mkutano uliokatazwa.

Wandishi wa habari - hasa marehemu Mwangosi - walisikika wakimpa nafasi nyingi Kamuhanda kubadilisha njia. Kwamba maana ya "internal meeting" si sawasawa na "inside meeting". Kwa maana ya kawaida ya lugha ya Kingereza mkutano unaweza kuwani "internal" bila kuwa "inside". Kwa kauli yake mwenyewe Kamanda Kamuhanda alifanya makosa zaidi pale alipodai kuwa yeye ana haki ya kutafsiri sheria zote na si kipengele kimoja.

Kwa kweli yeye si mtafsiri wa sheria na kama angekuwa na hekima (na ushahidi unaonyesha kuwa hana) alipaswa kuuliza mwanasheria wa serikali au mwanasheria mwingine kama mkutano ule ambao ulikuwa ni "internal meeting" unalindwa na haukuwa sehemu ya mikutano iliyopigwa marufuku. Kwa kutoa agizo la kuuvunja mkutano ule Kamanda Kamuhanda - japo inaweza kuwa ni katika bona fide - alivunja na kuingilia kati shughuli halali ya chama cha siasa kikifanya mambo yake ya ndani.

Hakuwa na mamlaka, wala sababu ya kuingilia mkutano wa ndani na alikuwa na nafasi ya kutosha kuweza kujihakikishia kuwa agizo lake lilikuwa halali.

Kinyume cha watu wengine ambao wanataka kuwa CHADEMA walipaswa kutii amri ya Polisi, binafsi naamini hawakutakiwa kutii amri hiyo ya kuwataka waondoke kwa sababu haikuwa amri halali, haikuwahusu na kwa hakika ilitolewa na mtu ambaye alitumia madaraka yake vibaya.

b. Wakati tukio la kuanza kumpiga mwandishi Mwangosi limeanza Kamanda Kamuhanda alikuwa na haki na uwezo wa kuhakikisha haki za raia zinalindwa.

Polisi wote wanajifunza sheria hii ambayo nimeweka hapo juu ambayo inaelekeza wazi kuwa polisi wanapomkamata mtu au kumzuia mtu asiwatoroke hawapaswi kutumia nguvu zaidi ya inayohitajika.

Yeye kama Kamanda wa Polisi wa Mkoa aliona nguvu ya Jeshi la Polisi iliyokuwapo pale na kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa ni tishio kwa jeshi hilo. Lakini zaidi ni kuwa walipomkamata Daud Mwangosi hakuwa na kitu kingine chochote cha kutishia polisi zaidi ya kamera na laptop yake. Wingi wa polisi waliomzunguka - picha na video zinashuhudia - unathibitisha pasipo shaka kuwa kama polisi waliamini (kwa sababu yoyote ile) kuwa Mwangosi amefanya kosa na anastahili kuwekwa chini ya ulinzi, polisi walikuwa na uwezo na nguvu ya kuweza kumdhibiti bila kumpiga.

Lakini kwa polisi kumkamata, kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa inathibitisha tu kuwa kamanda huyu hafai kuongoza hata chipukizi!

Alitakiwa avuliwe vyeo vyake na kuwekwa kizuizini mara baada ya mauaji yale ya Songea ambayo nayo yalitokea katika mazingira ya kutatanisha. Lakini badala yake magenius wetu wa Taifa wakaona akajaribu kuongoza Jeshi la Polisi kule Iringa.

Pamoja na hayo utaona kuwa hoja yangu inategemea sana kuwa kilichokiukwa ni kifungu hicho cha 21 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Kifungu hicho hata hivyo kinahusiana na tu na pale ambapo polisi wanajaribu kumkatama mtu au kuzuia mtu asiwatoroke. Ukiangalia tukio la mauaji ya Mwangosi ni wazi kuwa kilichotokea ni zaidi ya jaribio la kumuweka mtu kizuizini au chini ya ulinzi.

Mahali ambapo pamezungukwa na polisi wa kila namna na wakiwa na silaha ni mhalifu mjinga kabisa ambaye atajaribu kukimbia au ambaye hatotii amri ya kuambiwa yuko chini ya ulinzi.

Picha za tukio lile zinaonyesha pasi ya shaka kuwa Mwangosi hakuwa kwa namna yoyote ile ni mhalifu anayetaka kukimbia au ambaye ameamuriwa kuwa chini ya ulinzi na akabisha.

Maelezo ya mashuhuda wote waliokuwapo kwenye tukio yanadai kuwa kilichotokea kabla ya mauaji ni Mwangosi kupigwa kwanza na kundi la polisi na kwa dakika kadhaa kabla ya kufyatuliwa bomu.

Kama hili ni kweli – na sidhani kama lina utata sana – mauaji ya Mwangosi yanavuka maelekezo ya Kifungu hicho cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa sababu kundi la polisi wakitumia madaraka wasiyo nayo walianza kumpiga raia ambaye hakudaiwa uhalifu wowote na walifanya hivyo mbele ya kiongozi mkuu wa polisi mkoani humo ambaye hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza na kusema kuwa alijaribu kuzuia asipigwe!

Hii inanifanya niamini – na ninaomba msomaji ukubaliane nami – kilichotokea pale ni kitendo cha uhalifu wa ugangwe wa kundi la polisi ambao wakitumia silaha, sare na nafasi zao waliamini wanaweza wakampiga raia yeyote bila kuulizwa.

Na uwepo wa kamanda Kamuhanda pale na ambaye alisababisha mtafaruku ule kwa kutoa amri isiyo halali na kushindwa kwake kuingilia kati kuhakikisha anaokoa maisha ya raia ni dalili kuwa kamanda huyo ni mshirika wa uhalifu (criminal accomplice) na kumwacha aendelee kupigiwa saluti, kushiriki vikao na kuendelea kuongoza Jeshi la Polisi mkoani Iringa ni ucheleweshaji mkubwa wa haki, ni kukejeli akili za Watanzania na kubeza kila namna ya kipimo cha utawala bora. Ni kumlinda mhalifu.

Je atafikishwa mahakamani? Kwa jinsi Polisi walivyochukulia hili na zaidi wanasiasa wetu (wa chama tawala) walivyokubali hili ni wazi kuwa Kamuhanda zaidi atakachofanywa ni kuhamishwa na kupelekwa mkoa mwingine (ningependa binafsi aletwe Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Suleiman Kova).

Kumshtaki mtu mkubwa kama huyu ambaye ushahidi dhidi yake ni mkubwa kuliko ule wa Abdallah Zombe na kesi ya wauza madini utatikisa Jeshi la Polisi. Na kwa vile jeshi hili ni la kulindana (IGP Mwema ndiye aliyemuhamisha kutoka Ruvuma!) ni wazi kuwa njia pekee ya kuja kumshughulikia ni uongozi wa CHADEMA kuweka rekodi ya watendaji hawa ili watakapoingia madarakani iwe ni watu wa kwanza kushughulikiwa. Ikumbukwe mauaji hayana muda wa kukoma kuchunguzwa.

Ili kesi hii ionekane ina mfanano wa kudai haki kwa marehemu ni lazima askari wote walioshiriki katika kumpiga marehemu (naweza kujenga hoja kuwa yawezekana walimuua kabla ya bomu kulipuliwa!), baada ya askari mlipuaji bomu kufikishwa mahakamani, sasa afuatie Kamanda Kamuhanda ili kuonyesha kwamba Tanzania kuna mkono wa sheria usio na macho ya upendeleo.

Lakini kwa vile tunajua hili ni gumu kufanyika – kama litafanyika litazungushwa hadi kuondoa maana ya haki – basi Watanzania wajiwekee dhamira kuwa hawa wote waliohusika siku moja watalipishwa.

Na watalipishwa pia wale wengine ambao wataendelea kutoa maisha ya wananchi kwa nguvu ili kujitafutia sifa kwa watawala.

Wameasi dini lakini maadili yako wapi

NIANZE makala hii kwa kurejea simulizi moja ambayo nimeshawahi kusimulia katika makala zilizopita.

Kati ya mambo yaliyonishangaza sana baada ya kuwasili hapa Uingereza kwa mara ya kwanza, takriban muongo mmoja uliopita, ni jinsi Ukristo ulivyopoteza nguvu miongoni mwa Waingereza wengi.

Licha ya ‘kutolewa ushamba’ kwa kushuhudia vitu mbalimbali ambavyo kabla ya kuja hapa vilikuwa ni vya kufikirika tu kama si kuviona kwenye filamu na runinga, kilichoniacha mdomo wazi zaidi ni pale nilipoona jengo ambalo zamani lilikuwa kanisa limegeuzwa klabu ya anasa za usiku (night club).

Kwa Mndamba mie niliyezaliwa sehemu (Ifakara) ambayo ina historia ya karibu na umisionari, kuona ‘nyumba ya Bwana’ imegeuzwa ukumbi wa anasa lilikuwa jambo la kushangaza mno. Na kadri nilivyozidi kuielewa nchi hii ndivyo nilivyozidi kutambua kuwa idadi kubwa tu ya Waingereza haina muda na Mungu au dini kwa ujumla.

Kila nilipopata wasaa wa kudadisi sikusita kuuliza swali hili, “hivi imekuwaje ninyi mliotuletea Ukristo huko Afrika leo hii mnaonekana hamna habari na dini hiyo ilhali dini inazidi kupamba moto huko kwetu?”

Majibu ya swali hilo yalikuwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine, lakini jibu lililojitokeza mara nyingi zaidi ni kuwa imani ya kiroho haina nafasi muhimu katika zama hizi za sayansi na teknolojia.

Kimsingi, katika Jumapili ya kawaida, makanisa mengi ya Uingereza hujaza ‘wageni’ (kwa maana ya wakazi wenye asili ya nje ya nchi hii, hususan Waafrika na Wakritso kutoka Ulaya ya Mashariki).

Katika siku za kati ya wiki, mengi ya makanisa hayo yamekuwa kama vivutio vya utalii hasa ikizingatiwa kuwa mengi ya majengo hayo ya ibada yana sehemu muhimu katika historia za sehemu yaliyopo.

Lakini ukidhani kufifia huko kwa ‘dini ya nchi hii’ (kimsingi Uingereza ni nchi ya Kikristo na Malkia anaendelea kuwa ‘mkuu wa heshima’ wa Kanisa la Anglikana duniani) kunawafanya Waingereza kutokuwa watu wa kufuata maadili, basi ukienda sehemu mbalimbali za huduma (kama vile kwenye benki, maduka makubwa nk) au ofisini utakumbana na picha tofauti kabisa.

Kwanza, kwa kiasi kikubwa hakuna njia za mkato za kupata fedha katika nchi hii pasipo kuwajibika. Pili, Waingereza wengi wanachukulia shughuli zao kwa uzito na umuhimu mkubwa. Lakini jingine kubwa ni jinsi serikali na taasisi za utawala zinavyojibidisha kutengeneza mazingira mazuri ya kumwezesha kila anayejituma ‘avune matunda ya jasho lake.’

Kuna suala la haki na wajibu. Kwa kiwango kikubwa, wengi wa Waingereza wanatambua wajibu wao wa kulipa kodi, na wajibu huo unawapatia haki ya kupatiwa huduma ambazo kwa kiasi kikubwa zinakidhi matakwa yao.

Kadhalika, taasisi mbalimbali za hapa zinatambua wajibu wao wa kutoa huduma zinazoendana na matakwa ya wahitaji huduma hizo.

Kwa hiyo, licha ya nafasi ya Mungu na Ukristo (au dini kwa ujumla) kufifia miongoni mwa Waingereza wengi, bado kwa kiasi kikubwa jamii hii inafanya ‘mema’ mengi zaidi ya akina sie huko nyumbani tusiokosekana kwenye nyumba za ibada.

Binafsi, licha ya kutopendezwa kuona watu waliotuletea Ukristo huko nyumbani ‘wakiupiga teke,’ wengi wa Waingereza wanaendelea kunivutia jinsi wanavyoendesha maisha na shughuli zao kwa uadilifu mkubwa.

Japo Waingereza wengi ni kama hawana dini lakini wengi wao hawapo tayari kuona mwanadamu mwingine ananyimwa haki zake za msingi, na ndiyo maana nchi hii imetokea kuwa kimbilio kubwa kwa mamilioni ya wakimbizi ambao miongoni mwao ni wale walionyanyaswa na kuteswa na nchi zao aidha kwa imani au itikadi zao, jinsia zao, kutetea wanyonge na kadhalika.

Kwa hali hii, yayumkinika kuhitimisha kuwa bora kuwa ‘mpagani’ mtenda mema kuliko mcha-Mungu fisadi. Ndiyo, dini imepoteza umuhimu wake kwa wengi wa wenzetu hawa lakini wengi wao wameendelea kuwa ‘watu wema’ kuliko mamilioni ya wacha-Mungu huko Afrika.

Yawezekana kabisa ‘wapagani’ hawa kwenda mbinguni kutokana na kumpendeza Mungu kwa matendo yao huku washika dini wetu wakigeuzwa kuni za kuchochea washiriki wao katika kukandamiza, kuibia, kunyanyaswa na kufanya kila baya kwa wanadamu wenzao.

Ni katika mazingira haya ya ‘Uingereza ninayoipenda licha ya wengi wa watu wake kumpa kisogo Mungu’ ndipo nilijikuta nikishtushwa na habari katika gazeti moja la huko nyumbani kuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diane Louise Corner, “amesifu serikali kwa kukuza demokrasia kutokana na uhuru unaovipa vyombo vya habari kuujuza umma kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo matumizi ya umma yanayofanywa na serikali.”

Awali, naomba niseme bayana kuwa hadi muda huu bado nina wasiwasi iwapo Balozi Corner alinukuliwa sahihi (yaani, iwapo kweli alitoa kauli hiyo).

Sitaki kabisa kuamini kuwa Balozi huyo hana taarifa kuhusu unyanyasaji mkubwa unaofanywa na serikali dhidi ya vyombo vya habari binafsi huko nyumbani (ukiweka kando gazeti hilo la serikali liloandika habari hiyo).

Hivi inawezekana Balozi Corner hajawahi kusikia manyanyaso yaliyowakumba wamiliki wa jukwaa huru la mtandaoni la Jamii Forums ambalo kwa hakika limekuwa chanzo kikubwa cha kufichua maovu katika jamii?

Inawezekana Balozi huyo hajawahi kusikia tukio la kumwagiwa tindikali kwa mwandishi wa habari Said Kubenea ambaye serikali inayosifiwa na Balozi huyo imejipa jukumu la kudumu kumdhibiti mhariri huyo na gazeti lake ambalo kwa sasa limefungiwa kwa muda usiojulikana?

Ni demokrasia ipi anayozungumzia mwanadiplomasia huyo ambayo kwa upande mmoja inaruhusu mikutano ya chama tawala CCM katika kampeni za uchaguzi huko Zanzibar lakini si tu inapiga marufuku hata mikutano ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia inapelekea Jeshi la Polisi kunyanyasa wananchi wasio na hatia ambao ‘kosa’ lao pekee ni kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia ya kukusanyika (freedom of association)?

Hivi kweli Balozi Corner hana taarifa kuwa Jeshi la Polisi limeshafanya unyanyasaji mkubwa dhidi ya wafuasi wa CHADEMA na kupelekea vifo vya wananchi wasio na hatia huko Arusha, Morogoro na kubwa zaidi ni kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi huko Iringa hivi karibuni?

Ninasema sitaki kuamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari au demokrasia ninayoshuhudia hapa Uingereza ina tafsiri tofauti na hiyo anayosifia Balozi huyo huko nyumbani.

Niwe mkweli, moja ya sababu ninazoona kuwa zinachangia sana ukosefu wa utawala bora katika nchi zinazoendelea (ikiwamo Tanzania) ni tabia ya nchi zilizoendelea kama Uingereza kuendeleza tabia ya kufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu ambao hauna nafasi kabisa katika ‘jamii zao za kistaarabu.’

Hivi majuzi tu, serikali ya Uingereza kupitia Waziri Mkuu David Cameron imeomba msamaha kuhusiana na maafa ya Hillsborough yaliyotokea mwaka 1989 ambapo mashabiki kadhaa wa soka waliopoteza maisha.

Je, Balozi Corner anafahamu kuwa hadi leo serikali anayoisifia kwa kukuza demokrasia haijaomba msamaha kwa japo kifo cha mwandishi Mwangosi zaidi ya kuunda tume ambayo tayari imeanza kuhujumiwa huku baadhi ya wajumbe wake wakilalamikiwa kuwa na utendaji kazi wenye mushkeli?

Kama Mtanzania ninayeishi katika nchi ambayo huko nyuma ilitutawala kwa mabavu lakini ninaiheshimu na kuipenda kwa mengi inayofanya kwa utu wa mwanadamu pasi kujali ni Mwingereza au ‘mgeni,’ nimeshitushwa sana na kauli ya Balozi Corner ambayo kimsingi inaweza kutumika kama sababu tosha kwa watawala wetu kuendelea kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu kwa ujumla kwa kigezo cha kupewa ‘seal of approval’ na mwakilishi wa taifa kubwa na linaloaminika kwa kuenzi haki hizo muhimu za binadamu.

Kuna nyakati ninapata shida sana kuyaelewa haya mataifa makubwa kama Uingereza katika uhusiano wao na nchi ‘zinazojikongoja.’ Wao ndio wafadhili wetu wakubwa, na asilimia ya kutosha ya fedha za walipakodi wao ndizo zinachangia uhai na ustawi wa nchi masikini (japo zina utajiri unaofilisiwa kila kukicha) kama Tanzania.

Lakini cha kushangaza, hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa nao angalau kuwabana mafisadi wanaokwiba fedha zao (ambazo kimsingi zinatolewa kwa minajili ya kumsaidia kila Mtanzania).

Sana sana ni utitiri wa sifa zinazomwagwa kwa watawala wetu (kama hizo za kukuza demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari), sifa ambazo zinawapa motisha mafisadi kuendelea kuitafuna nchi yetu.

Je, ‘upole’ huo wa wafadhili wetu unachangiwa na hisia kuwa fedha za mafisadi huishia kuhifadhiwa katika mabenki yaliyopo huku? Au inawezekana bado mentality ileile iliyoleta ukoloni (na hata Ukristo) kwamba sisi tulikuwa hatujastaarabika vya kutosha na ilikuwa muhimu kwa wakoloni kujipa jukumu hilo, hadi sasa tunapaswa kuwa na demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari pungufu na tunayoshuhudia hapa Uingereza?

Nimalizie kwa kumkumbusha Balozi Corner kauli ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown katika harakati zake za kuisaidia Afrika.

Alisema (namnukuu katika tafsiri hii isiyo rasmi) “pasipo kuongeza jitihada za kusaidia, itazigharimu baadhi ya nchi za Afrika zaidi ya miaka 150 kufikia tulipofikia sisi (Waingereza).”

Lakini kwa mwenendo huu wa ‘sifa tusizostahili’ basi yayumkinika kubashiri kuwa inaweza kutuchukua hata milele kufikia demokrasia ya kweli yenye kuruhusu uhuru wa kweli wa vyombo vya habari.

Waandishi na serikali: Nani anaingilia mahakama



BAADHI ya wahariri na waelekezaji wengine katika tasnia ya habari, wamekuwa wakikariri kuwa jambo au shauri likiwa mahakamani, basi mwandishi hastahili au hapaswi kuandika lolote juu yake. Hili limetesa waandishi wengi walioamini kuwa kwa kuandika lolote watakuwa wanaingilia mahakama. Ndimara Tegambwage ni mmoja wa waelekezaji katika tasnia hii. Yafuatayo ni maoni yake kama yalivyochotwa kutoka mtandao wa Mabadiliko juu ya mgomo wa madaktari na juhudi za serikali kufunga akili na midomo ya wananchi.
NIMEKUWA nikieleza na hata kuelekeza, tofauti na baadhi ya wenzangu katika uandishi, kwamba jambo lililoko mahakamani linaweza kuandikwa. Kwa nini?
Kwamba jambo liko mahakamani, hakuzuii mambo mengine kutendeka juu ya hilohilo na nje ya mahakama. Dunia haisimami kwa kuwa jambo liko mahakamani.
Mwenendo wa kilichosababisha kuwa mahakamani hausiti au kufutika eti kwa kuwa tayari kuna shauri mahakamani. Hamu na haki ya kujua haviondoki eti kwa kuwa jambo liko mahakamani. Hapana!
Sheria haikuzuii na hasa haipaswi kukuzuia kuandika mlolongo wa matukio nje ya mahakama unaohusu watu wenye shauri lililoko mahakamani.
Matukio nje ya mahakama yaweza kutoa nuru zaidi juu ya wahusika katika shauri na hata juu ya shauri lenyewe. Taarifa juu ya matukio haya zaweza kuwa za msaada kwa wakili wa utetezi na wakili wa upande wa mashitaka.
Wakati (taarifa hizo) zinaweza kumpa mmoja nuru zaidi juu ya kilichotendeka, zaweza pia kumpa mwingine nuru juu ya kujenga ngome.
Hakimu au jaji anahitaji hoja mshibano na ushahidi mwanana (kama inavyowasilishwa mahakamani na siyo kama inavyosimuliwa nje). Uamuzi wake haupaswi kuongozwa au kutawaliwa au kufungwa na taarifa za magazeti, redio, televisheni au chombo chochote kile cha kutoa taarifa au habari.
Umadhubuti wa hakimu au jaji; hekima, uaminifu wake kwake binafsi na kwa kazi yake juu ya kesi iliyoko mbele yake, havipaswi kupanguliwa na taarifa za nje ya hoja zilizoko mahakamani kwa madai kuwa "zimeathiri maamuzi."
Tuna ushahidi ambako baadhi ya mahakimu na majaji madhubuti wamepuuza na kutupilia mbali madai ya kuathiriwa na vyombo vya habari wakiuliza, "Una uhakika na unaamini kuwa mimi siwezi kufanya kazi hii; siwezi kuwa na maoni na siwezi kuona haki mpaka niambiwe na vyombo vya habari?"
Hili lina maana kwamba kupogoka; kuangalia sheria kwa makengengeza na hata kutoa upendeleo wa waziwazi na uliofichika, ni shabaha, tena ya makusudi, ya hakimu au jaji na siyo kuathiriwa na taarifa za chombo cha habari.
Twende kwa serikali. Taarifa ya serikali ambayo iliahidiwa (juu ya mgomo wa madaktari); kama ingekuwepo, isingeingilia shauri lililoko mahakamani.
Haikuwepo au kuna kilichoingia katikati na kusababisha wasiitoe, ambacho ni wao pekee wanaokijua. Kwamba serikali haitatoa taarifa kwa kuwa imegundua shauri lake na madaktari liko mahakamani, ni sababu ya kizembe mno kutolewa na mamlaka.
Na kama serikali inaweza kusahau ilichofanya juzi tu, basi hii ni barua kwa umma ya kuomba kuaga ikulu.
Sheria haizuii wala kufunga, kwa mfano serikali, kutoka na taarifa inayosema: "Tumepata fedha za kutosha. Sasa madaktari watalipwa nusu ya wanachodai. Hapa tutapata pa kupumulia na kuendelea na majadiliano."
Sheria ipi itazuia hili. Sheria yaweza kununa iwapo serikali itatoka na kusema, "Mtakoma. Msimamo wetu ni uleule, liwalo na aliwe!"
Hili halikubaliki mbele ya hekima, achilia mbali mahakama. Huwezi kwenda mahakamani kuomba nafuu; ukarudi kesho yake kukaza nguvu ya amri ya kukupa nafuu; na kesho yake ukatoka kifua mbele, kwa kutumia nafuu ileile, kuwakomalia wale uliozuia, na isivyo haki, lakini ilivyo halali kisheria.
(Hapa) utakuwa umetumia nguvu ya mahakama kujinufaisha binafsi na utakuwa unajigamba kana kwamba umeweka "mahakama mfukoni."
Inawezekana serikali "imegundua kweli" kuwa inakwenda kufanya madudu. Ikaacha kutoa taarifa. Imejichanganya kwa kuwa imechanganyikiwa.
Hiyo ilikuwa  Alhamisi 28 Juni 2012, wakati nikijadili mtandaoni. Lakini nililoandika la kutumia “nguvu ya mahakama kujinufaisha binafsi…kana kwamba umeweka ‘mahakama mfukoni,” ndilo lilitokea baadaye.
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imekwenda mahakamani. Ikaomba nafuu. Ikapewa. Ikatoka mbele. Ikawakomalia madaktari. Ikaanza kuwashambulia. Kuwafukuza kazi kabla ya kile ilichoita “shauri kuu kusikilizwa na kumalizwa.”
Haya basi, siyo matumizi sahihi ya nafuu ya mahakama. Serikali ilikuwa na uwezo wa kufanya iliyofanya bila kutumia nguvu ya mahakama. Haikuhitaji ruhusa ya mahakama kufukuza madaktari.
Kwahiyo, serikali imeonyesha jinsi ilivyohitaji mahakama kufunga mikono, miguu na midomo ya madaktari, ili yenyewe (serikali) ipate nafuu na kuweza kuwacharaza wagomvi wao. Huku ndiko kuingilia mahakama.
Hapa ndipo vyombo vya habari vinajikuta vimetwishwa jukumu la kupaza sauti za wananchi na madaktari; na hata sauti ya mahakama – kupinga  matumizi mabaya ya mhimili mwingine wa dola (mahakama); tena kwa sababu dhaifu.

HISTORIA ya mabunge duniani inaliumbua bunge la Jamhuri. Ni kwa sababu, bunge hili limegeuza taasisi ya Bunge kuwa sehemu ya kuminya demokrasia. Limejisahau. Limejifunga mnyororo.

Ni tofauti na Bunge lililopita lililokuwa chini ya Spika Samwel Sitta.

Ni jambo la kusikitisha kuona ushahidi ukijionesha kiwango cha uwajibikaji serikalini kikishuka, Bunge likitumika kuiokoa.

Hakuna asiyejua kuwa serikali imeshindwa kuafikiana na madaktari. Bunge linagoma kujadili suala hilo. Kiongozi wa madaktari ametekwa, kujeruhiwa na sasa yuko kwenye matibabu nje ya nchi, bunge linafungwa mdomo kujadili.

Mauaji ya ovyo ya raia yanazidi kuonge; Bunge halijadili. Utawala bora unatukanwa, huku wawekezaji na matajiri wakitwaa ardhi ya wananchi, bunge linafungwa mdomo. Huu ni uzembe.

Ndiyo maana tunashuhudia utamaduni mpya ukiibuka bungeni; ili hoja ya mbunge ijadiliwe inategemea ni mbunge gani, na hasahasa, wa chama gani.

Kama ni asiyependeza kiti, hapewi nafasi. Kama alipewa kwa kutegwa kwa kuwa spika hakujua atakachokisema, akiibuka mbunge wa watawala na kumhoji, anaridhiwa. Yule anaambiwa “huna hoja.”

Waongoza bunge wametafuta lugha wanazoona nzuri kumbe wanakandamiza haki za wabunge kusema bungeni. Wanataka wabunge wakasemee wapi?

Kisingizio cha kuingilia mahakama hakina nguvu. Kutaja tukio ambalo limefika kwenye mahakama hakuna maana kuwa unaingilia uhuru wa bunge.

Tunasihi waongoza bunge warudi kwenye mstari. Wakiamini hawajakosea wala hawajaudhi au kuwaangusha Watanzania, basi hiyo ni hatari.

Tanzania ipo ndani ya mfumo wa vyama vingi ambao una utamaduni wake. Chini ya mfumo huu, bunge lazima kuwa wazi na huru.

Tungependa waongoza bunge watumie mamlaka waliyonayo kuiwajibisha serikali iliyoamua kukataa kuwajibika. Kama yenyewe haitaki, inalindwa vipi?