ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Tuesday, March 26, 2013

Waziri Kagasheki Awasha Moto katika wizara yake 


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki (pichani) amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza wajibu wa kutekeleza kazi kwa ubunifu na uadilifu huku wakizingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia utendaji kazi.
Balozi Kagasheki alitoa rai hiyo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jijini Dar es Salam.
Mhe. Waziri aliwataka wajumbe wa wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa Baraza ni chombo muhimu kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. 
“Tumieni vema nafasi mlizonazo kuhakikisha kuwa haki na wajibu wa Mwajiri na Mtumishi vinapewa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa kulinga maslahi ya pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa zima.
“Moja ya changamoto mliyonayo kama Baraza hili ni kuhakikisha watumishi wanazingatia nidhamu na maadili katika utumishi wa umma. 
 Ninafahamu mazingira ya kazi na hasa katika vituo vyetu si ya kuridhisha, lakini ni vyema tukahimiza watumishi kufuata kikamilifu Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi”, anasema Kagasheki.

Anasema wajumbe wakitekeleza wajibu wao  kama Wajumbe wa Baraza, watarahisisha kazi ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara. 
Aidha, aliwataka katika utekelezaji wa majukumu yeao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kwa uwazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi.

Wakatoliki waaswa kushiriki kifo na Ufufuo wa bwana yesu kwa kutubu dhambi zao.

Hayo yalisemwa na Paroko parokia ya Mtakatifu Bikira Maria MODEKO  Fr Macha, jumapili iliyopita mjini Morogoro wakati akiadhimisha Jumapili ya Matawi au Mitende ikiwa ni ishara ya kushangilia kuingia kwa bwana wetu yesu kristo (Masiha) Yerusalemu kwa shangwe, huku akienda kukamilisha ukombozi wa dhambi zetu sisi wanadamu.

"Ndugu zanguni wapendwa katika bwana, leo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kuingia kwa kristo mfalme katika mji wa Yerusalemu kukamilisha ukombozi wetu, Matawi hayo mliyoyabeba ni ishara ya furaha kumpokea bwana yesu moyoni mwenu na kushiriki naye kikamilifu katika juma hili linaloanzia kesho jumatatu kukamilisha utukufu wake." alisema Paroko.

Licha ya kwamba bwana wetu yesu kristo alikuwa akiingia mara kwa mara yerusalemu, lakini awamu hii ilikuwa  ni ya kipekee katika kukamilisha tukio maalumu la mateso yake  kwa kusulubiwa kuvikwa taji la miba,  kuchomwa mkuki katika ubavu wake  na kupigiliwa misumari katika msalaba wake na hatimaye kifo chake baada ya kutokea kwa giza kuu kwa masaa matatu na  ilipotimu saa 9  akakata roho.

Kumbuka mpendwa mkristo kutubu dhambi katika kipindi hiki cha mateso ya bwana yesu kwa kushiriki  naye kikamilifu katika kifo na ufufuo wake kwa kufanya kitubio na malipizi na kukusudia kuacha kabisa dhambi huku ukiandaa moyo wako ukiwa safi kumpokea bwana na mwokozi wa maisha yako kufufuka naye.

Wakristo wengi duniani wamekuwa hodari kuandaa mavazi mapya na kuandaa sherehe kubwa kwa ajili ya sherehe hiyo huku wakiwa hawajajiandaa kiroho kumpokea bwana wetu yesu kristo kwa kutubu dhambi zao na kuacha kabisa kutenda dhambi.

Aidha pamoja na kuwa na ibada katika juma kuu wakristo hao wameaswa kufunga na kuimbea Tanzania dhidi ya ishara za macahafuko ya kidini ambayo yamejitokeza  katika sehemu mbalimbali nchini kama vile kuuawa kwa wachungaji,kuchoma moto makanisa na vifaa na kutishia maisha kwa baadhi ya watendaji wa makanisa na kuishinikiza serikali kutoa msimamo wake dhidi ya kutochukua hatua za makusudi kuzuia mpasuko huo.
 






Monday, March 25, 2013

Dunia ikiwa inasonga mbele kimaendeleo hali ya wananchi kiuchumi nayo inaongeza kasi

Mtoto Gladyness Ugulumo mtoto wa mmiliki wa blogu hii akiwa katika harakati ya kujifunza matumizi ya kompyuta lakini kutokana na upeo wake kuwa mdogo anachoweza ni kucheza gemu na kuangalia katuni, ni mtoto ambaye amekuwa mdadisi wa mambo mbalimbali hasa ya kutaka kuijua zaidi kompyuta hali ambayo inampa faraja mama yake na pia baba yake kuona kwamba mtoto huyu yawezekana akawa ni mtaalamu katika mambo hayo ya sayansi ya kompyuta, anaiweza kuifungua na kuiwasha na hata kufikia kipengele ambacho mara kwa mara nimekuwa nikimruhusu kufikia bila wasi wowote namshukuru sana mungu.

Monday, January 14, 2013

KAMWENE MNOGAGE - unalijua hili  



Marehemu Chifu Mkwawa enzi za uhai wake

WAHEHE ni kama yalivyo makabila mengi ya kibantu yaliyomo Tanzania walikula majani, mizizi na matunda ya pori vitu ambavyo vilirithiwa vizazi na vizazi vilivyofuata na hatimaye kuwa vyakula vya kawaida kama mizizi, miti, matunda na majani.

Mzizi wa mti wa “MTONO” huliwa ungali bado mchanga ambao huitwa “ISONGI” unaochimbwa wakati wa masika au mahali palipo na unyevunyevu huliwa kama muwa kwa kumenya maganda.

Mti wa “AMAKINGILIGITI” huzaa matunda yaliyo na sura kama “golf” matunda haya yakiliwa ladha yake ni kama limao ingawa ulimao huo haujafananishwa kisayansi lakini hufanana na dawa za vitamini “B Complex” majani yake huliwa na mbuzi mwitu (aitwae kwa kihehe INGULUGULU) na mbegu zake huliwa pia.

“MUTOWO” huzaa matunda wakati wa kiangazi ambapo matunda yake huwa na nyuzi nyuzi wakati wa kutafuna mithili ya mtu atafunaye bigijii na zikitafunwa hutoa utomvu mzito wenye sukari nyingi, hazimezi kwa sababu zinawasha sana kwenye koromeo na huweza kuleta kikohozi cha muda mrefu.

Aidha mtu akila huweza kupatwa na hamu ya kiu ya kunywa maji hasa akiwa na kazi ngumu na pia huweza kuandaliwa kwa kuchemshwa na kudumu kwa muda wa miezi sita bila kuoza.

Matunda “MUNYWEWA” huwa katika ganda gumu ambalo ndani yake kuna maji matamu yanayonywewa na yanapunguza kiu yanafanana kabisa na mti wa MTANGADASI ambao hauna maji ila una nyama nzito ambayo ni chakula kizuri cha nyani na ngedere.

“AMAMBEDEE” hujulikana kama tango, mmea huu hutambaa kama mmea wa maboga hupendelea kuota zaidi kwenye mbolea ya samadi na walaji wakuu ni wenyeji wa mkoa wa Iringa na pia huliwa na wanyamapori hada digidigi.

“MAGUHU” mti wake ni mwepesi sana ukifananisha na MSONOBALI (CYPRESS) hustawi sana katika mbuga za mwinuko.Wahehe huita “MUWUBAMBA” ambao hauwezi kutumika kama kuna nishati ya kupikia kwa sababu ya wepesi wake huwaka mfano wa karatasi, matunda yake huwa mekundu na ndani yake huwa na uji wa rangi ya njano na ndiyo huliwa, linazo mbegu mbili zinazofanana sana ni laini lakini haziliwi.

Upo mti mwingine ujulikanao kama “MUFUDU” ambao huzaa matunda ya MUFUDU ambayo huliwa baada ya kukomaa lakini yakiwa hayajakomaa yanakuwa ya kijani huwezi kula machungu, matunda haya yana rangi nyeusi tii mithili ya kiwi, nyama yake huwa nyeusi pia na mbegu yake hailiwi hutupwa.

Haifahamiki pia ni kwa nini Wahehe walio weusi tii hufananishwa na MUFUDU.

Inaelezwa kuwa Mtwa GUNGIHAKA TOVELA PATELI mdogo wa Mtwa MKWAWA alikuwa mweusi tii lakini weusi wake ulifananishwa na weusi wa NYATI wakimwita ”WUTITU WA MBOGO” na “MUFUDU” wakimananisha ni mweusi kama NYATI na MUFUDU.

“MUSAULA” ni mti unaofanana na miti ya MINYWEWA, MUTANGADASI, MUTUNDWA na MUGUHU ambao huota nyanda zilizoinuka na hukomaa kiangazi tu kwa hiyo ni tunda la msimu kati ya mwezi Mei, Juni na Julai ni chakula cha NYANI pia huliwa na watoto wadogo zaidi.

“MUSANSAWUKI” ni aina ya majani ambayo huota msimu wa masika tu, huzaa matunda yenye miba mingi sana. Matunda hayo hutoa maua mengi yenye rangi nyekundu na haya maua mekundu huwa na utomvu ambao ukifyonza ni mtamu. Utomvu huo huitwa Wununu ambao pia huliwa na vipepeo na nyuki na watoto (binadamu).

Mizizi, majani na matunda machache yaliyoainishwa hapo juu yalikuwa na pengine bado yanaliwa na Wahehe kutoka siku za kale. Nia na makusudi ya kuandika makala haya ni kukielimisha kizazi cha sasa kuwa wazazi wao walikula vyakula hivyo vya porini ambayo vilisaidia kushinda magonjwa mbalimbali mwilini kwa sababu vilitoa kiwango madhubuti mwilini.

Vijana wengi wa siku hizi ambao hawataki au hawajui vyakula vya porini vipo, wamekuwa kivutio kikubwa kwa magonjwa mbalimbali kwa sababu ya kukosa kinga ya ziada
 

Monday, November 12, 2012

Uchafu ndani ya Manispaa ya Iringa wazidi

Chomo cha kuhifadhi takataka kikiwa barabarani maeneo ya msikitini Kihesa.
Ikiwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiueleza umma kuwa wanawajibika katika suala la usafi, hali ya usafi bado inadorora.

Licha ya kuweka baadhi ya vifaa vya kuhifadhia takataka maarufu kwa jina la madampo, yamekuwa yakikaa kwa muda mrefu bila kuhamishwa kwenda kumwaga uchafu huo na kusababisha usumbufu kwa wananchi wa maeneo yanayolizunguka dampo husika.

Moja ya dampo ambalo kila wakati husahauli kubwebwa kwenda kutupwa uchafu huo ni lle ambalo lipo maeneo ya msikitini Kihesa ambalo huutumiwa na kila mtu wakiwemo wapitanjia.

Licha ya kusahaulika, dampo hilo liko barabarani hali inayoweza kusababisha ajali wakati wowote kwa wananchi wanaotembea kwa miguu au magari wakati wa kupishana.

Mtandao huu ulimkariri Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alikisema kuwa hali ya usafi katika Manispaa inaridhisha kwani wamejipanga vizuri kwa ajili ya usafi.

Pamoja na kujidai kuwa halmashauri imejipanga vizuri kwa ajili ya usafi, Mwamwindi kila wakati amekuwa akilalamika kuwa Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa amewaachia kazi hiyo.

Kwa upande wake Mch. Msigwa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa, kazi ya usafi katika Manispaa mipango yote inatakiwa kufanywa na Meya kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri.(Story from www.GUSTAV CHAHE.blogsport.com)

WAKALI WA MIC, TWANGA PEPETA, WAFUNIKA DAR LIVE


Washiriki wote wakiwa pamoja kabla ya kuanza shindano hilo.
Mmoja wa washiriki akionyesha hazina yake katika sanaa hiyo.
Washindi  wa tano bora.
Luiza Mbutu (kushoto) wa Twanga Pepeta akiimba na mwanamuziki mwenzake.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakiwa kazini.
Majaji Ally Baucha, (kulia) John Dilinga na Abdalah Mrisho (kushoto) wakifuatilia shindano hilo.
Mshiriki akikamua kwa madoido.
Kinadada wakifuatilia shindano hilo.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mpambano kati ya Chelsea na Liverpool ukumbini humo.
SHINDANO la kumtafuta mkali wa ‘maiki’, The Mic King,  lililoendelea na kufanyika jana  Jumapili  katika ukumbi wa kisasa wa burudani wa Dar Live ulioko Mbagala jijini Dar es Salaam,  na kusindikizwa na Bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’,  lilitoa burdani ya aina yake kutokana na vijana washiriki kutoka wilayani Temeke kuonyesha umahiri mkubwa katika muziki wa kufokafoka.
Story by www.francisgodwin.blogspot.com

Sunday, October 21, 2012

TUNAIPELEKA WAPI DUNIA , MAKANISA YANAANZISHWA KAMA BAR ZA POMBE ZA KIENYEJI




Shalom!
Wapendwa naomba tusimame katika kuomba huruma ya Mungu na atupe Roho wake Mtakatifu tuogope kabisa kumfanyia Mungu mzaha. Tuko katika wakati mgumu sana nyakati hizi za mwiso, wapo “watumishi wa mungu” wanaohubiri kwa kutumia Maandiko Matakatifu/Biblia lakini nguvu wanazotumia ni za kununua/za giza! Wameusoma upepo uliopo sasa kuwa watu wamejawa na matatizo mengi na tabu nyingi, sasa mahubiri yanayohubiriwa yamebakia kuwa ya upande mmoja tu! MAZURI. Watu wanahubiriwa kupata nyumba, magari, biashara kubwa, watoe/wapande mbegu wapate baraka tele za kusukwa sukwa (mtu kabeba chuki na mtu moyoni mwake miaka hajaachilia) nk. Mambo mengine ya msingi kama kusamehe waliokukosea, kupenda na kuwaombea maadui, kutoa kwa makundi mbalimbali ya wahitaji nk hayaelezwi. Jinsi ya kujenga uhusiano mzuri na Mungu ili kuweza kukabiliana na mitihani ama changamoto mbalimbali za maisha ya ndoa, kazi, imani nk havifundishwi.
Watu wanapatwa na changamoto hizi kwa vile watumishi wa Mungu hawafundishi waumini wao namna ya kukabiliana na mateso mbalimbali kadiri ya maandiko na mifano mbalimbali ya watu walivyoshinda changamoto katika Biblia kwa kumtegemea Mungu. Kwa sababu yakutokufundishwa hayo utakuta watu wana giveup na kuona suluhu ni kuhamahama makanisa kutafuta watakapopata miujiza ama suluhu ya matatizo yao na bado hawapati. Na watu wakipata utajiri ama mazuri wanarudi kumsifu na kumshukuru/kumsifu mtumishi na mtumishi anakuwa “very proud” kwa sifa hizo. Haturudishi Sifa Shukrani na Utukufu kwa Mungu.
Kwa kweli Tunahitaji kuomba, kanisa limeyumba! Halina baba mlezi wa kukemea mambo, sasa kuanzisha makanisa imekuwa kama kuanzisha biashara. Kila leo kanisa jipya na kila mmoja anasema kwake ndiko bora. Hebu tuombe kwa ajili ya wimbi hili wapendwa!