Wakatoliki waaswa kushiriki kifo na Ufufuo wa bwana yesu kwa kutubu dhambi zao.
Hayo yalisemwa na Paroko parokia ya Mtakatifu Bikira Maria MODEKO Fr Macha, jumapili iliyopita mjini Morogoro wakati akiadhimisha Jumapili ya Matawi au Mitende ikiwa ni ishara ya kushangilia kuingia kwa bwana wetu yesu kristo (Masiha) Yerusalemu kwa shangwe, huku akienda kukamilisha ukombozi wa dhambi zetu sisi wanadamu.
"Ndugu zanguni wapendwa katika bwana, leo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kuingia kwa kristo mfalme katika mji wa Yerusalemu kukamilisha ukombozi wetu, Matawi hayo mliyoyabeba ni ishara ya furaha kumpokea bwana yesu moyoni mwenu na kushiriki naye kikamilifu katika juma hili linaloanzia kesho jumatatu kukamilisha utukufu wake." alisema Paroko.
Licha ya kwamba bwana wetu yesu kristo alikuwa akiingia mara kwa mara yerusalemu, lakini awamu hii ilikuwa ni ya kipekee katika kukamilisha tukio maalumu la mateso yake kwa kusulubiwa kuvikwa taji la miba, kuchomwa mkuki katika ubavu wake na kupigiliwa misumari katika msalaba wake na hatimaye kifo chake baada ya kutokea kwa giza kuu kwa masaa matatu na ilipotimu saa 9 akakata roho.
Kumbuka mpendwa mkristo kutubu dhambi katika kipindi hiki cha mateso ya bwana yesu kwa kushiriki naye kikamilifu katika kifo na ufufuo wake kwa kufanya kitubio na malipizi na kukusudia kuacha kabisa dhambi huku ukiandaa moyo wako ukiwa safi kumpokea bwana na mwokozi wa maisha yako kufufuka naye.
Wakristo wengi duniani wamekuwa hodari kuandaa mavazi mapya na kuandaa sherehe kubwa kwa ajili ya sherehe hiyo huku wakiwa hawajajiandaa kiroho kumpokea bwana wetu yesu kristo kwa kutubu dhambi zao na kuacha kabisa kutenda dhambi.
Aidha pamoja na kuwa na ibada katika juma kuu wakristo hao wameaswa kufunga na kuimbea Tanzania dhidi ya ishara za macahafuko ya kidini ambayo yamejitokeza katika sehemu mbalimbali nchini kama vile kuuawa kwa wachungaji,kuchoma moto makanisa na vifaa na kutishia maisha kwa baadhi ya watendaji wa makanisa na kuishinikiza serikali kutoa msimamo wake dhidi ya kutochukua hatua za makusudi kuzuia mpasuko huo.
No comments:
Post a Comment