ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Monday, November 12, 2012

Uchafu ndani ya Manispaa ya Iringa wazidi

Chomo cha kuhifadhi takataka kikiwa barabarani maeneo ya msikitini Kihesa.
Ikiwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiueleza umma kuwa wanawajibika katika suala la usafi, hali ya usafi bado inadorora.

Licha ya kuweka baadhi ya vifaa vya kuhifadhia takataka maarufu kwa jina la madampo, yamekuwa yakikaa kwa muda mrefu bila kuhamishwa kwenda kumwaga uchafu huo na kusababisha usumbufu kwa wananchi wa maeneo yanayolizunguka dampo husika.

Moja ya dampo ambalo kila wakati husahauli kubwebwa kwenda kutupwa uchafu huo ni lle ambalo lipo maeneo ya msikitini Kihesa ambalo huutumiwa na kila mtu wakiwemo wapitanjia.

Licha ya kusahaulika, dampo hilo liko barabarani hali inayoweza kusababisha ajali wakati wowote kwa wananchi wanaotembea kwa miguu au magari wakati wa kupishana.

Mtandao huu ulimkariri Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alikisema kuwa hali ya usafi katika Manispaa inaridhisha kwani wamejipanga vizuri kwa ajili ya usafi.

Pamoja na kujidai kuwa halmashauri imejipanga vizuri kwa ajili ya usafi, Mwamwindi kila wakati amekuwa akilalamika kuwa Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa amewaachia kazi hiyo.

Kwa upande wake Mch. Msigwa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa, kazi ya usafi katika Manispaa mipango yote inatakiwa kufanywa na Meya kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri.(Story from www.GUSTAV CHAHE.blogsport.com)

WAKALI WA MIC, TWANGA PEPETA, WAFUNIKA DAR LIVE


Washiriki wote wakiwa pamoja kabla ya kuanza shindano hilo.
Mmoja wa washiriki akionyesha hazina yake katika sanaa hiyo.
Washindi  wa tano bora.
Luiza Mbutu (kushoto) wa Twanga Pepeta akiimba na mwanamuziki mwenzake.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakiwa kazini.
Majaji Ally Baucha, (kulia) John Dilinga na Abdalah Mrisho (kushoto) wakifuatilia shindano hilo.
Mshiriki akikamua kwa madoido.
Kinadada wakifuatilia shindano hilo.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mpambano kati ya Chelsea na Liverpool ukumbini humo.
SHINDANO la kumtafuta mkali wa ‘maiki’, The Mic King,  lililoendelea na kufanyika jana  Jumapili  katika ukumbi wa kisasa wa burudani wa Dar Live ulioko Mbagala jijini Dar es Salaam,  na kusindikizwa na Bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’,  lilitoa burdani ya aina yake kutokana na vijana washiriki kutoka wilayani Temeke kuonyesha umahiri mkubwa katika muziki wa kufokafoka.
Story by www.francisgodwin.blogspot.com

Sunday, October 21, 2012

TUNAIPELEKA WAPI DUNIA , MAKANISA YANAANZISHWA KAMA BAR ZA POMBE ZA KIENYEJI




Shalom!
Wapendwa naomba tusimame katika kuomba huruma ya Mungu na atupe Roho wake Mtakatifu tuogope kabisa kumfanyia Mungu mzaha. Tuko katika wakati mgumu sana nyakati hizi za mwiso, wapo “watumishi wa mungu” wanaohubiri kwa kutumia Maandiko Matakatifu/Biblia lakini nguvu wanazotumia ni za kununua/za giza! Wameusoma upepo uliopo sasa kuwa watu wamejawa na matatizo mengi na tabu nyingi, sasa mahubiri yanayohubiriwa yamebakia kuwa ya upande mmoja tu! MAZURI. Watu wanahubiriwa kupata nyumba, magari, biashara kubwa, watoe/wapande mbegu wapate baraka tele za kusukwa sukwa (mtu kabeba chuki na mtu moyoni mwake miaka hajaachilia) nk. Mambo mengine ya msingi kama kusamehe waliokukosea, kupenda na kuwaombea maadui, kutoa kwa makundi mbalimbali ya wahitaji nk hayaelezwi. Jinsi ya kujenga uhusiano mzuri na Mungu ili kuweza kukabiliana na mitihani ama changamoto mbalimbali za maisha ya ndoa, kazi, imani nk havifundishwi.
Watu wanapatwa na changamoto hizi kwa vile watumishi wa Mungu hawafundishi waumini wao namna ya kukabiliana na mateso mbalimbali kadiri ya maandiko na mifano mbalimbali ya watu walivyoshinda changamoto katika Biblia kwa kumtegemea Mungu. Kwa sababu yakutokufundishwa hayo utakuta watu wana giveup na kuona suluhu ni kuhamahama makanisa kutafuta watakapopata miujiza ama suluhu ya matatizo yao na bado hawapati. Na watu wakipata utajiri ama mazuri wanarudi kumsifu na kumshukuru/kumsifu mtumishi na mtumishi anakuwa “very proud” kwa sifa hizo. Haturudishi Sifa Shukrani na Utukufu kwa Mungu.
Kwa kweli Tunahitaji kuomba, kanisa limeyumba! Halina baba mlezi wa kukemea mambo, sasa kuanzisha makanisa imekuwa kama kuanzisha biashara. Kila leo kanisa jipya na kila mmoja anasema kwake ndiko bora. Hebu tuombe kwa ajili ya wimbi hili wapendwa!

Saturday, October 20, 2012

BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA TANZANIA

1. Acha kukuna makovu ya mende (Kichaga)
Maana yake ni kwamba uache kukumbuka taabu ya wakati uliopita. Methali hii itafahamika vizuri kama tukielewa kwamba hapo zamani katika jamii zetu, mende walikuwa wanaonekana kwa wingi katika nyumba. Nao mende ni hodari wa kuuma watu wakati wa usiku wakiwa wamelala. Na pale walipouma hubaki kovu ambalo hukuna. Lakini pia ambaye ameshaumwa na mende hao itakuwa ni kazi bure kama atakalia kuyakuna makovu hayo.
Methali hii hutumika kwa kuwaonya watu wasikalie kufikiria makosa au taabu za wakati uliopita.

2. Afadhali kuchakaza nguo kuliko akili (Kipare)
Maana yake ni kuwa hakuna kitu bora kama akili (hekima). Mtu ambaye hana hekima ya uchi kuliko uchi wa aina yoyote ile. Kuwa uchi kinguo, mtu anaweza kununua zingine. Lakini mtu anapokuwa uchi kiakili, hakuna maarifa.
Methali hii hutumika kwa kumhurumia mtu ambaye ameharibikiwa na akili na anafanya majambo isivyotakiwa katika jamii.

3. Amekufa hata Mwakafwile aliacha mwana alipokufa (Kinyakyusa)
Methali hii inatokana na mila za kibantu kukosa mrithi ni mwisho wa ukoo na jina la ukoo. Mtoto wa kiume huendeleza ukoo. Ni jambo la kusikitisha sana kutokuwa na mwana mrithi.
Maana ya methali hii ni kwamba mtu anayehusika hana msaada wowote kutoka kwa ndugu, jirani au mahali penginepo.
Hutumika na mtu binafsi aliyezama ndani ya kilindi kikubwa cha matatizo, wala hana mtoto au mtu wa karibu naye ambaye angeweza kumsaidia. Ni methali ya watu maskini na wanyonge katika kuhurumiana shidani. Kama kuunguliwa nyumba, kufiwa nk.

4. Anayetaka usawa mwisho wake uchawi (Kikerewe)
Methali hii ina maana kwamba tukubali kuwa binadamu budi kutofautiana. Fulani kapata baiskeli – lazima nami nipate, fulani kapata nyumba – lazima nami nipate nk. Maneno kama haya mwishowe humsukuma mtu kutumia hila mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile uchawi.
Methali hii hutumika katika kuwaonya wanopenda kujikweza.

5.Fimbo ya jirani haiui nyoka (Kiiraqw)
Ujirani ni jambo jema lakini si vizuri kutegemea misaada yote toka kwa majirani. Methali hii inafundisha umuhimu wa kujitegemea na si kutazamia kupata misaada kila uhitajipo.Pia, ni lazima ieleweke kwamba hakuna sheria inayomfanya jirani atoe msaada hata kama anaweza, yote hutegemea matakwa yake na huwezi kubashiri ni lini atakataa kutoa msaada.

6. Fungo alikosa mkia kwa kulala (Kizigua na kinguu)
Ipo hadithi katika hadithi za Kizigua na Kinguu isemayo kuwa kwa sababu ya usingizi wake Fungo alikosa au aliupoteza mkia wake. Methali hii inaonyesha hasara ya uzembe na kuchelewa mara nyingi. Hali hii inaweza kumkosesha mtu mambo mengi mazuri au kupoteza maslahi yake ambayo yangemfaa baadaye. Hutumika kama onyo kwa wazembe.

7. Anayelala na mgonjwa ndiye anayejua miugulio (Kisambaa)
Maana yake ni kwamba huwezi kujua undani wa mtu mpaka uwe naye karibu katika uhusiano. Hutumika kwa mtu anayejitia kujua sana mambo ya ndani ya wengine kuliko wenyewe wanaohusika.

8. Hohehahe hakosi siku yake (Kiha)
Maana yake ni kuwa kila mtu ana bahati yake. Hata maskini ana siku yake ya bahati. Hutumika kama onyo kuwa inafaa kuthamini watu kwa utu wao na wala si kwa mali walizonazo. Mtu ni utu.

9. Kondoo wa madoadoa hawako katika jamii ya wanadamu (Kimasai)
Wanadamu wote hawahitilafiani sana kwa maumbile yao, na ndio maana tunaweza kusema, binadamu wote ni sawa. Tusikiapo kitu kisicho cha kawaida kuhusu mtu tunaweza kutumia msemo huu kumaanisha kwamba tumestaajabishwa na habari hizo. Msemo huu unatumika pia katika kukanusha habari zisizoaminika.

10. Kucheka chongo ya mwenzio na hali yako umefunika (Kisukuma)
Maana yake ni kuwa si vizuri kucheka makosa ya wengine kwani huenda ukafanya makosa yale yale na pengine una udhaifu wako ambao wengine wanakucheka. Hutumika katika kuwaonya watu wanaocheka dosari au udhaifu wa watu wengine na pengine watu wanaocheka wenzao waliopatwa na maafa k.m. kufilisika.

11. Mbwa mwenye mnofu mdomoni hapigi kelele (Kifipa) Maana yake ni kama methali ya kiswahili isemayo:- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Methali hii hutumiwa kwa kuwasema watu ambao wana kitu na huwasahau wale ambao hawana kitu. Zaidi, huweza kutumika kwa kuwaonya viongozi wanaosahau kuwatetea wenzao baada ya kupata madaraka na shibe.

12. Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha (Kikwere) Mwenda usiku hapa ni sawa na mtu ayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi. Lakini mwishowe jambo hilo lilipoonyesha mafanikio ndipo watu wakaanza kumsifu. Hutumika kwa mtu anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekeo hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.

13. Nguo ya mzee haikosi chawa (kimeru) Maana yake, mzee hakosi akiba. Maana ya methali hii itafahamika zaidi si kwa vile hali ya uchafu ndiyo iletayo chawa, bali kwamba kwa mzee huwa na akiba za aina aina nayo maana yake ni ile nzuri. Methali hii hutumika wakati mtu anapozungumzia utajiri wa mtu mzee. Ni kama njia ya kuwakoga wengine kwamba wakati wote utazamie kumkuta mzee katka hali nzuri, anayo akiba yake ambayo ameihifadhi.

14. Usidharau wakunga uzazi ungalipo (Kibena) Wakunga ni watu wenye kuheshimiwa sana kwa sababu ya ufundi na ujuzi wao wakati wa kuzalisha. Kwa kuchukua umuhimu wao huo, wanawake hushauriwa kutowadharau maadamu wangali wanazaa, isijeikawa wakti wa kujifungua wakakosa msaada. Matumizi ya methali hii ni kuwaonya watu kwa ujumla wasiwe na dharau kwa kitu ambacho kitawafaa katika maisha yao. Zaidi kwamba, kitu kilichokusaidi wakati uliopita usikidharau kwa vile hukitumii kwa wakati huu.

"Tubadilishane dogo"

"Tubadilishane dogo" pengine ndivyo asemavyo CDF Davis Mwamunyange akiwa ktk foleni na baadhi ya vijana wake walioko kambini Msata ambao wanatarajiwa kuelekea Sudan kilinda amani, maana yawezekana ni siku nyingi hajatumia mustin.
Hii inafurahisha sana, mustin zanikumbusha mbali sana hizi. 
by rwebangira blog

JWTZ laingia kudhibiti maandamano haramu Dar






Katika kudhiirisha kauli ya Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolise Suleiman Kova, kuwa “uvumilivu sasa basi” kwa mara ya kwanza nchini askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wameonekana mitaani kusaidiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wafuasi wanaosemekana kuwa ni wa Sheikh Issa Ponda, ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali, walikuwa wanaandamana kuelekea Ikulu kushinikiza kuachiwa kwake bila masharti.
Si kawaida kwa JWTZ kuingia katika vurugu za maandamano, lakini bila shaka “UVUMILIVU UWA UNA MWISHO”, labda huu ni mwanzo wa enzi mpya, Muda tu ndio utaamua.  Picha kwa hisani ya Happiness Mnale
story by rwebangira blog

UNAKUMBUKA? WIMBO WA TANZANIA!!!


1, Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.
2. Tanzania Tanzania,
Ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu,
Biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi,
Mambo mema ya kwetu kabisa,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.
3. Tanzania Tanzania,
Watu wako ni wema sana,
Nchi nyingi zakuota,
Nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia,
Ngome yako imara kweli wee,
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa.
4. Nchi nzuri Tanzania,
Karibu wasio kwao,
Wenye shida na taabu,
Kukimbizwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha,
Mpigane kuime chema wee,
Yanzania Tanzania 
Mola awe nawe daima.