ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Wednesday, February 5, 2014

KILELE MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM YAFANA MBEYA, JK AMSIFU KINANA NA TIMU YAKE KWA UCHAPAKAZI

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi  alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya leo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. JK aliimpongeza Kinana kwa kuonesha  njia na kutoa mfano kuhusu kufanya kazi ya chama ndani ya umma. Katika ziara zake mikoani akifduatana na baadhi ya makatibu wa Sekretarieti na viongozi wengine wa CCM, amekuwa  anafanya kazikubwa na nzuri sana . Na kwamba ziara zake zinakijenga chama na kutoa tawsira nzuri ya chama katika jamii. Pia alisema ziara za Kinana zinahuisha uhai wa chama.

Ndugu Kinana amekuwa anafanya  mambo  ambayo hayajazoeleka kufanywa. ametembelea maeneoa ambayo si viongozi wengi hufika. Wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha wengi. Hukaka na wananchi, anakula nao na kufanya nao kazi. Na kubwa zaidi amekuwa anatoa fursa kwa wananchi kuelezea matatizo yanayowasibu, manung'uniko yao na kero zao.. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho, ambapo alisisitiza kuendeleza utaratibu alionao wa chama hicho kuwa karibu na wananchi, pamoja na kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
 JK akionesha mfano wa Jembe na Nyundo alama za chama hicho zinazomaanisha kwamba nchi inaongozwa na wafanyakazi na wakulima.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini, baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama hicho, wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya
 Kinana akiwapiga picha wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers) waliokuwa wakipiga picha ya paoja na Rasi Kikwete baada ya maadhimisho kumalizika.
 Wafuasi wa CCM waliotimiza miaka 37, wakirusha njiwa 37 ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
 Msanii Ummy Wenslaus (Dokii), akionesha vimbwanga vyake alipokuwa akitumbuiza kwa wimbo wake wa CCM wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rungwe,  Richard Kasesera (kulia) wakicheza ngoma ya ling'oma wakati wa maadhimisho hayo.
 Kundi la TOT likiongozwa na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa likifanya mambo wakati wa maadhimisho hayo
 Wasanii wa muziki na filamu wakiwapungia mikono wananchi baada ya kujiunga na CCM leo
 Seehemu ya umati wa wananchi ukiwa katika sherehe za maadhimisho hayo
 JK akimkabidhi nyaraka mlemavu wa mikono ambayo alimwahidi akiawa ziarani Mbeya siku zilizopita
 JK akitimiza ahadi kwa kumkabidhi Bajaji mlaemavu wa miguu
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (katikati) akipiga gita alililinunua kwa ajili ya kumpatia msaada msanii (kuia) wa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini, baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama hicho, wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya
 JK akikabidhi gitaa hilo, iiwa ni kutimiza ahadi aliyomwahidi msanii huyo mwaka jana
 Msanii huyo akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa gitaa hilo
JK  na Kinana wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa vyuo vikuu waliojiunga na chama hicho

MWENYEKITI WA CCM,RAIS JAKAYA KIKWETE APIGA PICHA YA PAMOJA NA MA-BLOGGER - KATIBU MKUU KINANA NDIYE MPIGA PICHA


 Mwenyekiti wa wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na ma-bloggers wakubwa wa Tanzania wakati wa kiadhimisha sherehe za miaka 37 za uhai wa CCM uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana hapo chini...

Sunday, November 17, 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA DKT MVUNGI ,MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAONGOZA WATANZANIA

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akitoa salamu za Rais Jakaya Kikwete wakati wa  Ibada  ya kuuaga   mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu  Dk. Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu  Dk. Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Edmond Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu  Dk. Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam .


Rais Mstaafu wa  Serikali ya Awamu ya tatu Benjamin Mkapa  akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk. Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.



Mwenyekiti wa  Chama cha Wananchi(CUF)Profesa Ibrahim  Lipumba   akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.


Mwenyekiti wa  Chama cha  NCCR -Mageuzi  James Mbatia     akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.






Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa  mwili  wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.
Watoto wa marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Natujwo (kushoto) na  Neema (kulia)  wakinadi shairi lakuelezea baba yao alivyojasiri  heshima kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.
Mke wa marehemu Dk.  Sengodo Mvungi , Anna Mvungi (katikati)  akiwa katika ibada hiyo kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji,Francis  Mutungi akizungumza katika msiba huo .
Waziri wa Habari ,Vijana , Michezo na  Utamaduni  Dk. Fenella  Mukangara  akiuaga  mwili.

Profesa Palamagamba Kabudi ambaye ni rafiki wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba  marehemu Dk.  Sengodo Mvungi  akitoa heshima kwenye viwanja vya Karimjee leo jijini Dares Salaam.

  Monsinyori Deogratius Mbiku (wa pili kulia ) akiongoza ibada na wenzake .


Familia ikiwa katika msiba.

Dk. Salim Ahmed Salim  akiaga mwili huo . (Picha  Fullshangwe blog na Magreth Kinabo)

Babu wa Loliondo atangaza watu kumiminika upya, Apata maono mengine.

millard
Millard Ayo wa Clouds FM Alipokua akifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila maarufu kama Babu wa Loliondo
Hivi karibuni mtangazaji maarufu Millard Ayo katika kipindi chake cha Ampifaya alifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila na kuelezea kwa urefu mwanzo wa huduma yake ya kikombe, changamoto, walioiga kutoa vikombe, vipingamizi pamoja na waliokufa, ambao hawakupona hawakufuata masharti ya dawa.
Mwishoni mwa mahojiano Babu wa Loliando akasema kuhusu mafuriko mapya yatakayotokea hivi karibuni huko Samunge, alizungumza hivi
Siwezi kusema moja kwa moja kwamba ni mwezi wa tatu, ingekuwa pengine mpaka sasa tungeanza kupata watu wengi, na inawezekana ikawa mwezi huo wa tatu, au kabla au baada, mimi siwezi kusema moja kwa moja kwasababu kuna vipingamizi vingi tu, ambavyo Mungu anasubiri vitimie ndipo kazi hiyo ianze, Kuna miujiza mingi imeandikwa ndani ya biblia kitabu cha Mwanzo, Zaburi, Ezekiel, Ufunuo yapo maajabu mengi ambayo Mungu ameyaandika hayakutimia katika nchi ya Israel yatatimia hapa, Samunge, kwahiyo mafuriko ya watu watakaokuja si kwa ajili ya kunywa dawa tu lakini ni kwa ajili ya mambo mbali mbali kuja kuona miujiza ya Mungu itakayofanyika
Alipoulizwa ni maajabu gani yatakayofanyika akasema
“Si vizuri, sijamwambia mtu yeyote ba hata hapa kwako sitasema, isipokuwa mimi nimeyaona mengi tu nimeyaona tayari lakini Mungu hajaniambia tangaza napewa (Maono) kila wakati linakuja hili, linakuja hili napewa kila wakati lakini si zaidi ya labda nusu mwaka sasa
Ili kulinganisha habari ndipo mtangazaji Millard Ayo alipomuuliza Mchungaji Onesmo Ndegi ni maajabu gani hayo ya kwenye biblia
Mchungaji akasema “Hakuna muujiza ambao haujatendeka zaidi ya ule muujiza wa unyakuo, miujiza mingine yote iliyotabiliwa ilishatendeka kwa mfano ukisoma muujiza mkubwa sana ambao Mungu aliuzungumza kutoka Mwanzo 3:15 biblia inasema hivi nami nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake huo utakuponda kichwa na wewe utauponda kisigino, sasa hapa alikuwa anazungumzia juu ya ujio wa Kristo na ushindi wa Kristo dhidi ya nguvu za giza au shetani na ilishatokea na tunaishi katika kipindi hicho, Yesu Kristo alishakuja akazaliwa, na uwezo wake ukadhibitika ushindi dhidi ya shetani ulionekana pale msalabani, kwa hiyo hakuna muujiza mwingine ambao utasema kuanzia mwanzo haujatimia sasa kuna mtu anataka kuutimiliza, hakuna muujiza wa namna hiyo
Babu wa Loliondo alipoulizwa tena ana ushauri gani kwa Serikali juu ya maajabu  hayo makubwa yatakayotokea hivi karibuni akajibu
Nilitaka kusema kwa upande wa Serikali, nitasema ya kwamba Serikali iwe makini kupokea watu watakaokuja maana ni wengi, ni mafuriko kwa hiyo wawe makini”
Hata hivyo babu amewasamehe watu wote waliomsema vibaya “Kisasi ni kwa Bwana” alisema
–Millard Ayo

Ibada ya Kukabidhiana Msalaba wakati wa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Jimbo kuu la Dar es Salaam

Na: Kizito Ugulumo

Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Msalaba unachukua maana ya pekee katika maisha ya waamini, kwani wanatumwa na kuchangamotishwa kuwa ni mashahidi amini wa Kristo na Kanisa lake: kwa maneno na matendo. Msalaba ni kielelezo cha mapendo, neema, sala, msamaha na matumaini yasiyodanganya kamwe!

Ndiyo maana, Kanisa linaona fahari juu ya Msalaba wa Kristo kwa kuutembeza katika nyumba za waamini, ili wapate nafasi ya kusali na kulitafakari Fumbo la Msalaba, ishala ya mateso na alama ya wokovu wa binadamu; mahali ambapo hekima ya Mungu imetundikwa juu yake! Ni mwaliko wa kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu. Ifuatayo ni Ibada ya kukabidhiana Msalaba katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Vikundi vya pande zote mbili: wanaokabdhi na waokabidhiwa wanasimama mbele ya Msalaba. Padri wa kikundi kinachokabidhi msalaba anaanza ibada:

Padri: Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...
Wote: Amina.
Padri: Bwana awe nanyi..
Wote: Na awe rohoni mwako.

Padri anaeleza madhumuni ya kukutana:

Padri: Ndugu zangu, tumekutana hapa ili kukabidhiana Msalaba wa Mwaka wa Imani, ambacho ni chombo alichotumia Bwana wetu Yesu Kristo kutukomboa. Tunafanya tendo hili la ibada ya kuuheshimu Msalaba ili Mungu azidi kutujalia neema ambazo Kristo alitustahilisha kwa mateso, kifo na ufufuko wake. Tunawakabidhi Msalaba huu ili muupokee kama kumpokea Kristo mwenyewe katika parokia yenu. Uwe ishara ya ujio wake Kristo katika Mwaka huu wa Imani. Wakati wote utakaokuwa parokiani kwenu utunzwe na kuheshimiwa kama chombo kitakatifu kilicholeta wokovu. Ishara ya Msalaba huu iwaletee wingi wa neema za Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Wote: Amina.

Sasa tusikilize somo linalotueleza kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu:

Somo: Yohane (3:14-21)

Inafuatia tafakari fupi

Sala za Waamini:

Padri wa kikundi kinachopokea Msalaba anaongoza Sala za Waamini:

Padri: Ndugu zangu, Yesu Kristo amemtolea Mungu Baba maisha yake Msalabani ili ampatanishe na wanadamu. Ee Baba wa huruma uyasikie maombi yetu...
Wote: Bwana utuongezee imani

    Msalaba utukumbushe mapendo makubwa ya Kristo; Msalaba uamshe shukrani mioyoni mwetu...
    Msalaba uwe bendera ya Wakristo na alama ya ushindi wao; Msalaba ututie nguvu katika mateso, vitisho na hatari...
    Msalaba utufanye tuwe imara katika imani yetu, uwe nguvu yetu ya kuwafukuza pepo wabaya na washawishi...
    Msalaba uwe nguvu yetu ya kututoa katika dhambi na mazingira ya dhambi, ili sisi sote tuweza kuingia katika ufalme wa Mungu...
    Kwa ishara ya Msalaba tuwabariki wana familia zetu; tufanye ishara ya Msalaba maishani na kifoni...

Ee Mungu, umeweka Msalaba uwe ishara ya ukombozi wetu na alama ya huruma na mapendo yako. Twakuomba utupe neema ya kuuchukua Msalaba wetu pamoja na Mkombozi kwa mapendo makubwa. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Wote: Amina.

Wanakabidhiana Msalaba Mtakatifu, huku ukiimbwa wimbo ufaao...

Wednesday, November 13, 2013





Je waijua bendera ya Tanganyika iliyokuwa ikipepea kabla ya Uhuru!

 



















Hiii ndiyo bendera ya Tanganyika ambayo kimsingi yapaswa kupepea tena baada ya kuundwa kwa serikali tatu.






 Na hii ndo bendera ya ndugu zetu itakayokuwa nchi jirani endapo muundo wa serikali tatu uliomo katika rasimu ya katiba utapitishwa




 Na endapo yote hayo hapo juu yasipotokea basi tutaendelea kupepea na bendera hii ambayo mpaka sasa ndo utambulisho wetu baada ya kuunganisha bendera hizo kuu za nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.



JE WAJUA MKWAWA ALIVYOWATEKETEZA WAJERUMANI KWA DAKIKA 15 TU!!!



HUU ni mfululizo wa Makala ya Uchunguzi kuhusiana na historia ya kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, kama yanavyoandikwa na Mwandishi Wetu, ambaye amefanya uchunguzi kwa takriban miezi mitatu sasa katika kuhimiza utalii wa ndani na kuhifadhi historia yetu. Endelea na Sehemu hii 

HADI wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake
“…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, nilimsikia Sajini Tiedemann akisema alikuwa ameumia kabla hajafyatua risasi. Haikuwa rahisi kuona zaidi ya umbali wa hatua tano msituni kutoka pale njiani. Pia hakuna ambaye aliweza kunusurika kwa sababu Wahehe walikuja kwa kasi… Ni wazi walipanga kutushambulia baada ya kufika katikati msitu. Kuvurugika kwa mipango yao kulichangiwa hasa na kitendo cha Luteni von Zitewitz kufyatua risasi…”
Muanzilishi wa Himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki, Carl Peters, baadaye Novemba 23, 1891 alimwandikia Gavana von Soden akisema kwamba, katika mapambano mengine na makabila mbalimbali ya Tanganyika, ilikuwa ni bahati tu kwao kutoweza kupata madhara kama waliyopata Wajerumani pale Lugalo, kwani mafunzo yao ya vita yalikuwa yanalenga zaidi kupigana wakiwa wamejipanga pamoja kwa mbinu maalum. Hawakuwa wamejifunza kupigana kila mtu kwa uwezo wake, bali walitegemea zaidi kushambulia kwa pamoja.
Iliwachukua Wahehe dakika 15 tu (kuanzia saa 1:15 hadi 1:30 asubuhi) kuwafyeka Wajerumani na majeshi yao. Von Zelewiski aliuawa kwa kupigwa nyundo kichwani akiwa amepanda punda wake wakati akijiandaa kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Mkwawa. Kabla hajadondoka akachomwa mkuki ubavuni.
Hii ndiyo asili hasa ya jina la ‘Nyundo’ kutokana na kamanda huyo wa Wajerumani kuuawa kwa nyundo!
Kuhusiana na kifo cha Kamanda von Zelewiski, kama Mjerumani Tom von Prince alivyoandika baadaye, “Kama nilivyosimuliwa baadaye… na Wahehe walioshuhudia, alijitetea mwenyewe kwa kutumia bastola yake kubwa na kuwapiga risasi watu watatu, wakati kijana mmoja wa Kkihehe alipomchoma na mkuki ubavuni. Kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 16 tu na alizawadiwa ng’ombe watatu na Mkwawa kwa kitendo hicho.”
Luteni von Pirch na Dk. Buschow pia waliuawa wakiwa juu wa punda wao ambapo majeraha yao yalikuwa makubwa mno. Karibu askari wote wa Kikosi cha 7, Kikosi cha Silaha, Kikosi cha 5 na baadhi ya askari wa Kikosi cha 6 waliuawa kabla hata hawajajua wafanye nini.
Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi pamoja na askari 20 hivi ndio waliofanikiwa kukimbia kutoka eneo hilo la mapigano na kukimbilia upande mwingine wa mlima na kuweka ngome wakijilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahehe. Wapiganaji hao wa wajerumani walijificha kwenye pagala moja la tembe lililokuwa limetelekezwa mlimani. Askari mmoja Msudani ndiye aliyekiona kibanda hicho.
Lakini von Heydebreck aliishuhudia vita hiyo katika kipindi cha dakika mbili au tatu tu kabla ya kupoteza fahamu. “Kulingana na ushuhuda wa Wahehe walioshiriki mapigano yale, vita hivyo havikumalizika mapema kama ambavyo Wazungu wa mstari wa nyuma walivyotegemea, badala yake askari walionusurika waliendelea kupambana hadi saa 4:30 asubuhi na kuwaua maadui wengi (Wahehe).”
Askari wa mwisho wa kikosi cha Luteni von Tettenborn ndio hawakupata madhara makubwa ya mashambulizi ya Wahehe, washukuru kutokana na makosa ya ishara, vinginevyo wote wangeangamia katika kipindi hicho cha dakika 15 tu. Von Tettenborn, Feldwebel Kay na askari kama 20 hivi Wasudani wakahamia upande wa kushoto wa eneo la mapigano na kutengeneza nusu duara kwa ajili ya mashambulizi huku wakiwa wameumia. Wakiwa hapo walipandisha bendera ya Ujerumani juu ya mti na kupiga mbinja ili kuwaita manusura wengine.
Wakati huo Wahehe waliendelea kuwakimbiza manusura na kushambulia kila waliyemuona mbele yao. Mkanganyiko ukaongezeka baada ya kuwasha nyasi.
Mnamo saa 2:30 asubuhi hiyo, Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi wakiwa na askari wao 12 walipenya na kuungana na kikosi cha von Tettenborn. Von Heydebreck alikuwa anavuja sana damu kutokana na majeraha mawili makubwa ya mikuki. Kwa kuwatazama tu watu hao, von Tettenborn akatambua kwamba vikosi vyao vyote vilikuwa vimesambaratishwa na kikosi cha silaha kutekwa, ambapo Mkwawa aliteka bunduki 300. Askari wa jeshi la Wajerumani waliouawa siku hiyo walikuwa zaidi ya 500.
Ilipofika saa 3:00 Luteni Usu Thiedemann, akiwa na majeraha makubwa ya moto aliingizwa kwenye kikosi cha Luteni von Tettenborn akiwa amebebwa na askari waliokuwa wanafanya doria. Nyasi zilizokuwa zinaungua sasa zilimtisha von Tettenborn na manusura wengine.
Hadi kufikia saa 10:00 jioni Luteni von Tettenborn alikuwa amewakusanya majeruhi wengi na kuokota baadhi ya mizigo yao. Wahehe waliokuwa wamepagawa kwa hasira pamoja na moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuteketeza msitu viliifanya kazi ya kuwatafuta majeruhi wengine kuwa ngumu, hivyo wengi waliteketea kwa moto. Von Tettenborn akaamua kuanza kurudi nyuma kabla hajazuiwa na Wahehe.
Wakati wa usiku wa manane kikosi kilichokuwa na Luteni von Tettenborn kikapiga kambi ng’ambo ya pili ya mto tofauti na mahali walipolala kabla ya kuanza mapambano. Kikosi chake sasa kilikuwa na yeye mwenyewe na Luteni von Heydebreck, ma-NCO watatu wa Kijerumani (ingawa Luteni Usu Thiedemann alikufa baadaye njiani), maofisa wawili wa Kiafrika, ma-NCO 62 wa Kiafrika, wapagazi 74 na punda 7. Kutoka hapo wakaanza kutembea hasa nyakati za usiku kurudi nyuma ambapo walifika Myombo Agosti 29.
Hakuna takwimu halisi za idadi ya Wahehe waliokufa kwenye vita hiyo ingawa makadirio ni kati ya 260 hadi 700. Kwa ujumla, Wajerumani walikuwa wameshinda vita dhidi ya wakoloni, ushindi ambao ni wa kihistoria kwa mtawala yeyote wa Kiafrika wakati huo dhidi ya Wazungu. Haya yalikuwa matokeo mabaya zaidi kwenye vita katika historia ya ukoloni wa Wajerumani.
Jeshi la Wahehe halikuwa na haja ya kuhitimisha ushindi wake kwa kuwafuatilia Wajerumani waliosalia ili kuwaangamiza kabisa. Badala yake, kuanzia wakati huo wakaendelea kuishambulia misafara yote ya Wazungu.