ADVERT 1

ADVERT 1
Kilio na kimbilio la wanahabari Tanzania

Tuesday, March 26, 2013

Waziri Kagasheki Awasha Moto katika wizara yake 


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki (pichani) amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza wajibu wa kutekeleza kazi kwa ubunifu na uadilifu huku wakizingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia utendaji kazi.
Balozi Kagasheki alitoa rai hiyo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jijini Dar es Salam.
Mhe. Waziri aliwataka wajumbe wa wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa Baraza ni chombo muhimu kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. 
“Tumieni vema nafasi mlizonazo kuhakikisha kuwa haki na wajibu wa Mwajiri na Mtumishi vinapewa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa kulinga maslahi ya pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa zima.
“Moja ya changamoto mliyonayo kama Baraza hili ni kuhakikisha watumishi wanazingatia nidhamu na maadili katika utumishi wa umma. 
 Ninafahamu mazingira ya kazi na hasa katika vituo vyetu si ya kuridhisha, lakini ni vyema tukahimiza watumishi kufuata kikamilifu Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi”, anasema Kagasheki.

Anasema wajumbe wakitekeleza wajibu wao  kama Wajumbe wa Baraza, watarahisisha kazi ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara. 
Aidha, aliwataka katika utekelezaji wa majukumu yeao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kwa uwazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi.

Wakatoliki waaswa kushiriki kifo na Ufufuo wa bwana yesu kwa kutubu dhambi zao.

Hayo yalisemwa na Paroko parokia ya Mtakatifu Bikira Maria MODEKO  Fr Macha, jumapili iliyopita mjini Morogoro wakati akiadhimisha Jumapili ya Matawi au Mitende ikiwa ni ishara ya kushangilia kuingia kwa bwana wetu yesu kristo (Masiha) Yerusalemu kwa shangwe, huku akienda kukamilisha ukombozi wa dhambi zetu sisi wanadamu.

"Ndugu zanguni wapendwa katika bwana, leo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kuingia kwa kristo mfalme katika mji wa Yerusalemu kukamilisha ukombozi wetu, Matawi hayo mliyoyabeba ni ishara ya furaha kumpokea bwana yesu moyoni mwenu na kushiriki naye kikamilifu katika juma hili linaloanzia kesho jumatatu kukamilisha utukufu wake." alisema Paroko.

Licha ya kwamba bwana wetu yesu kristo alikuwa akiingia mara kwa mara yerusalemu, lakini awamu hii ilikuwa  ni ya kipekee katika kukamilisha tukio maalumu la mateso yake  kwa kusulubiwa kuvikwa taji la miba,  kuchomwa mkuki katika ubavu wake  na kupigiliwa misumari katika msalaba wake na hatimaye kifo chake baada ya kutokea kwa giza kuu kwa masaa matatu na  ilipotimu saa 9  akakata roho.

Kumbuka mpendwa mkristo kutubu dhambi katika kipindi hiki cha mateso ya bwana yesu kwa kushiriki  naye kikamilifu katika kifo na ufufuo wake kwa kufanya kitubio na malipizi na kukusudia kuacha kabisa dhambi huku ukiandaa moyo wako ukiwa safi kumpokea bwana na mwokozi wa maisha yako kufufuka naye.

Wakristo wengi duniani wamekuwa hodari kuandaa mavazi mapya na kuandaa sherehe kubwa kwa ajili ya sherehe hiyo huku wakiwa hawajajiandaa kiroho kumpokea bwana wetu yesu kristo kwa kutubu dhambi zao na kuacha kabisa kutenda dhambi.

Aidha pamoja na kuwa na ibada katika juma kuu wakristo hao wameaswa kufunga na kuimbea Tanzania dhidi ya ishara za macahafuko ya kidini ambayo yamejitokeza  katika sehemu mbalimbali nchini kama vile kuuawa kwa wachungaji,kuchoma moto makanisa na vifaa na kutishia maisha kwa baadhi ya watendaji wa makanisa na kuishinikiza serikali kutoa msimamo wake dhidi ya kutochukua hatua za makusudi kuzuia mpasuko huo.
 






Monday, March 25, 2013

Dunia ikiwa inasonga mbele kimaendeleo hali ya wananchi kiuchumi nayo inaongeza kasi

Mtoto Gladyness Ugulumo mtoto wa mmiliki wa blogu hii akiwa katika harakati ya kujifunza matumizi ya kompyuta lakini kutokana na upeo wake kuwa mdogo anachoweza ni kucheza gemu na kuangalia katuni, ni mtoto ambaye amekuwa mdadisi wa mambo mbalimbali hasa ya kutaka kuijua zaidi kompyuta hali ambayo inampa faraja mama yake na pia baba yake kuona kwamba mtoto huyu yawezekana akawa ni mtaalamu katika mambo hayo ya sayansi ya kompyuta, anaiweza kuifungua na kuiwasha na hata kufikia kipengele ambacho mara kwa mara nimekuwa nikimruhusu kufikia bila wasi wowote namshukuru sana mungu.