KAMWENE MNOGAGE - unalijua hili
Marehemu Chifu Mkwawa enzi za uhai wake
WAHEHE
ni kama yalivyo makabila mengi ya kibantu yaliyomo Tanzania walikula majani,
mizizi na matunda ya pori vitu ambavyo vilirithiwa vizazi na vizazi vilivyofuata
na hatimaye kuwa vyakula vya kawaida kama mizizi, miti, matunda na
majani.
Mzizi
wa mti wa “MTONO” huliwa ungali bado
mchanga ambao huitwa “ISONGI” unaochimbwa wakati wa masika au mahali palipo na
unyevunyevu huliwa kama muwa kwa kumenya maganda.
Mti
wa “AMAKINGILIGITI” huzaa matunda yaliyo na sura kama “golf” matunda haya
yakiliwa ladha yake ni kama limao ingawa ulimao huo haujafananishwa kisayansi
lakini hufanana na dawa za vitamini “B Complex” majani yake huliwa na mbuzi mwitu (aitwae kwa
kihehe INGULUGULU) na mbegu zake huliwa pia.
“MUTOWO”
huzaa matunda wakati wa kiangazi ambapo matunda yake huwa na nyuzi nyuzi wakati
wa kutafuna mithili ya mtu atafunaye bigijii na zikitafunwa hutoa utomvu mzito
wenye sukari nyingi, hazimezi kwa sababu zinawasha sana kwenye koromeo na huweza
kuleta kikohozi cha muda mrefu.
Aidha
mtu akila huweza kupatwa na hamu ya kiu ya kunywa maji hasa akiwa na kazi ngumu
na pia huweza kuandaliwa kwa kuchemshwa na kudumu kwa muda wa miezi sita bila
kuoza.
Matunda
“MUNYWEWA” huwa katika ganda gumu ambalo ndani yake kuna maji matamu
yanayonywewa na yanapunguza kiu yanafanana kabisa na mti wa MTANGADASI ambao
hauna maji ila una nyama nzito ambayo ni chakula kizuri cha nyani na
ngedere.
“AMAMBEDEE”
hujulikana kama tango, mmea huu hutambaa kama mmea wa maboga hupendelea kuota
zaidi kwenye mbolea ya samadi na walaji wakuu ni wenyeji wa mkoa wa Iringa na
pia huliwa na wanyamapori hada digidigi.
“MAGUHU”
mti wake ni mwepesi sana ukifananisha na MSONOBALI (CYPRESS) hustawi sana katika
mbuga za mwinuko.Wahehe huita “MUWUBAMBA” ambao hauwezi kutumika kama kuna
nishati ya kupikia kwa sababu ya wepesi wake huwaka mfano wa karatasi, matunda
yake huwa mekundu na ndani yake huwa na uji wa rangi ya njano na ndiyo huliwa,
linazo mbegu mbili zinazofanana sana ni laini lakini haziliwi.
Upo
mti mwingine ujulikanao kama “MUFUDU” ambao huzaa matunda ya MUFUDU ambayo
huliwa baada ya kukomaa lakini yakiwa hayajakomaa yanakuwa ya kijani huwezi kula
machungu, matunda haya yana rangi nyeusi tii mithili ya kiwi, nyama yake huwa
nyeusi pia na mbegu yake hailiwi hutupwa.
Haifahamiki
pia ni kwa nini Wahehe walio weusi tii hufananishwa na MUFUDU.
Inaelezwa
kuwa Mtwa GUNGIHAKA TOVELA PATELI mdogo
wa Mtwa MKWAWA alikuwa mweusi tii lakini weusi wake ulifananishwa na weusi wa
NYATI wakimwita ”WUTITU WA MBOGO” na “MUFUDU” wakimananisha ni mweusi kama NYATI
na MUFUDU.
“MUSAULA”
ni mti unaofanana na miti ya MINYWEWA, MUTANGADASI, MUTUNDWA na MUGUHU ambao
huota nyanda zilizoinuka na hukomaa kiangazi tu kwa hiyo ni tunda la msimu kati
ya mwezi Mei, Juni na Julai ni chakula cha NYANI pia huliwa na watoto wadogo
zaidi.
“MUSANSAWUKI”
ni aina ya majani ambayo huota msimu wa masika tu, huzaa matunda yenye miba
mingi sana. Matunda hayo hutoa maua mengi yenye rangi nyekundu na haya maua
mekundu huwa na utomvu ambao ukifyonza ni mtamu. Utomvu huo huitwa Wununu ambao
pia huliwa na vipepeo na nyuki na watoto (binadamu).
Mizizi,
majani na matunda machache yaliyoainishwa hapo juu yalikuwa na pengine bado
yanaliwa na Wahehe kutoka siku za kale. Nia na makusudi ya kuandika makala haya
ni kukielimisha kizazi cha sasa kuwa wazazi wao walikula vyakula hivyo vya
porini ambayo vilisaidia kushinda magonjwa mbalimbali mwilini kwa sababu vilitoa
kiwango madhubuti mwilini.
Vijana
wengi wa siku hizi ambao hawataki au hawajui vyakula vya porini vipo, wamekuwa
kivutio kikubwa kwa magonjwa mbalimbali kwa sababu ya kukosa kinga ya ziada